Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Rais Samia Suluhu amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko

Inaonekana ile Tume iliyoundwa na PM ilipotosha. Sasa hii inawezekana ilisababishwa na "Hadidu za Rejea". Aliyeandaa zile hadidu naye inabidi ajitathimini.Inawezekana hadidu ziliandaliwa kwa style ya kumlinda mtu fulani kwa maslahi ya mtu fulani.

Nadhani uchunguzi wa ufisadi pale bandari alioagiza mheshimiwa Raisi utaichunguza pia ile tume,hasa yale matokea ya ule uchunguzi.

Nadhani tunakokwenda ni kuzuri.
 
Inasikitisha sana!

Yaani wakati watumishi wa umma wanadai haki zao za malimbikizo yao ya mishahara ambayo haifiki hata bilioni 1, lakini kuna watu wachache wanachota fedha za umma kama maji!!!

hii sio haki kabisa. Mungu anawaona.
 
PM alifanya lilikokuwa kwenye uwezo wake na alisema ambao wako juu ya uwezo wake anamwachia rais...PM asingeweza kumtumbua DG wa TPA wakati hajamteua yeye.
ngoja uchunguzi ufanyike ,tuone matokeo,halafu tutajua ni kipindi kipi Yule bwana,alianza kufilisi shamba,la bwana shamba bora.ninawasiwasi huenda kipindi Cha miez 3 iliyopita.
 
Hivi kama alivyosimamishwa mkurugenzi wa TPA je ataendelea kupokea mshahara?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama amesimamishwa maana yake uchunguzi unafanyika, hapo anawekwa nje ya payroll mpaka uchunguzi uishe, akithibitika hana kosa baada ya kuhukumiwa na kamati ya nidhamu atajaza form ya madai kudai mishahara yake ya miezi yote ya uchunguzi

Sasa hapo ni kama protocal hizo za kiutumishi zitafuatwa ila inategemea zaidi na maamuzi ya Rais aliyemsimamisha.
 
..Kwa ngazi aliyofikia anaweza kuteuliwa kuwa balozi.

..Watangulizi ktk nafasi hiyo walipelekwa ubalozini au ukurugenzi ktk taasisi za serikali.
Amekuwa Mkurugenzi pale kijiweni Habari na Maelezo,😃😃
 
Kuna mtu tunahitaji kumfundisha adabu kabla ya April 26...ujinga aliofanya tar 13 usiku kuamkia 14 hauvumiliki..
Je unamaanisha E.kwandikwa aliekua Waziri wa ulinzi!!?
Nasikia "meza hizi halafu lala pale" nilisikia Toka Kwa jamaa fulani baada ya hapo akalala jumla au!!?
 
Back
Top Bottom