Rais Samia Suluhu ashangaza wengi kasi ya Ukuaji Uchumi Tanzania

Rais Samia Suluhu ashangaza wengi kasi ya Ukuaji Uchumi Tanzania

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029

IMG-20220129-WA0014.jpg

====​

Rais Samia aifikisha Tanzania ukuaji wa Uchumi wa 5.2% kutoka 2.1%,Heko Tanzania,​


According to National Bureau of Statistics (NBS) Pato la Taifa yaani Tanzania Gross Domestic Product- GDP limekua kwa kasi ya ajabu katika kipindi hiki kifupi cha Rais Samia Suluhu Hassan,

Pato letu Watanzania limekua na kufikia asilimia 5.2 robo ya tatu ya mwaka kutoka asilimia 4.1 robo ya kwanza,

Mtakumbuka wakati Rais Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani yaani kuanzia tarehe 19|03|2021 ukuaji wa Pato la Taifa ulikuwa asilimia 4.1,

Kwa lughal rahisi tunaweza kusema Rais Samia Suluhu Hassan kwa miezi hii michache amekuza Pato la nchi kwa ukuaji "Chanya" wa Uchumi,

Rais Samia Suluhu amekuza uchumi wa Tanzania kwa asilimia 5.2 wakati huu huu ambao majirani zetu wengi wakishuhudia ukuaji "Hasi " wa Uchumi katika nchi zao,

Mtakumbuka,hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2019 pale ambapo AfDB waliikadiria Tanzania Pato lake kushuka kutoka wastani wa ukuaji wa asilimia 7 hadi ukuaji wa asilimia 2.1 mwaka 2019|2020 na sababu ikiwa ni Covid 19,

Wakati huohuo baadhi ya nchi za Africa Mashariki walishuhudia ukuaji hasi wa Uchumi Tanzania chini ya Rais Samia mambo ni Safi,

Kwamfano,Rwanda ilirekodi ukuaji hasi wa asilimia 3 & 6 huku Kenya wao wakishuhudia ukuaji hasi wa asilimia 2.1 katika robo ya pili ya mwaka 2021,

Wakati wenzetu wakirekodi ukuaji hasi Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan tulirekodi ukuaji Chanja wa asilimia 4.4 katika kipindi kama hicho,

Kuimarika kwa kasi kwa Utalii na uwekezaji mkubwa toka nje pamoja na kilimo vimetajwa kuwa ni sababu za kukua kwa kasi kwa Uchumi wa Tanzania hasa katika robo ya tatu ya mwaka 2021,

Ukuaji huu wa uchumi ulifikia TZS 32 trilioni kutoka TZS 30.3 trilioni katika robo ya tatu ya mwaka 2020.

Katika robo ya tatu ( Q3 ) mwaka 2020 Tanzania ilipokea Jumla ya Watalii 72,147 pekee,

Hali ni tofauti katika kipindi kama hicho mwaka 2021 kwani Tanzania imepokea Jumla ya Watalii 243,565 sawa na ongezeko la Watalii wapya 171,418 ambao ni sawa na asilimia 338

Utalii katika robo hii ya tatu ( Q3 ) umechangia asilimia 18.1 kwenye Uchumi wa Taifa na hii inachagizwa zaidi utengenezaji wa "Royal Tour Film " itakayozinduliwa rasmi 22|04|2022 huku kilimo kikichangia asilimia 15,
 
Tanzania post 5.2 percent economic growth in Quarter 3


Dar es Salaam.

===
The latest economic growth report by the National Bureau of Statistics (NBS) for the third quarter of 2021 (July and September) shows Tanzania’s Gross Domestic Product (GDP) rebounded to 5.2 percent from 4.4 percent recorded in the second quarter.

According to the figures, Q3 GDP increased to Sh32 trillion in 2021 from Sh30.3 trillion in 2020.

Some of the key factors that buoyed the national economy as highlighted in the report include tourism which saw an increase of tourists visiting the country in Quarter 3 to 243,565 compared to 72,147 tourists in the corresponding period in 2020, construction has contributed about 18.1 percent of the growth followed by agriculture which stood at 15.1 percent .

Other East African countries also registered positive GDP results following a contraction in Quarter 2. Rwanda has recorded growth of about 10.1 percent from negative growth of 3.6 percent, whereas Kenya recorded growth of 9.9 percent from negative growth of 2.1 in quarter two of 2021.

Tanzania is projected to maintain positive growth in Q4 stemming from the continued economic recovery efforts in different sectors.


Souce : The Citizen
 
>>>>Pia Soma hapa <<<<<

 
Siku Tz ifikie tu hata uchumi wa Kenya, kuna watu mtatembea uchi huku mkisifia watawala waliopo

Eti 5.2, yaaani tathimini mjifanyie nyingi na mawazili na wakuu wa mikoa halafu useme tuko vizuri kiuchumi?

Umewahi fika vijijini wewe? Utatokwa machozi jinsi wananchi wanavyoshinda njaa siku nzima bila kula
 
Mama habari nyingine,!!

Haya mambo ndio yanazua #2025FEVER

KAZIIENDELEE MAMA😀😀😀
 
Simu eti Tz ifikie tu hata uchumi wa Kenya, Luna wtu mtatembea uchi huku mkisifia watawala waliopo

Eti 5.2, yaaani tathimini mjifanyie nyingi na mawazili na wakuu wa mikoa halafu useme tuko vizuri kiuchumi?

Umewahi fika vijijini wewe? Utatoka machozi jinsi wananchi wanavyoshinda SKU nzima bila kula
Mkuu hapa tunazungumzia Ukuaji wa Uchumi sio kiwango Cha Uchumi,
 
Mtoa hoja ningependa nikualike uje huku Lingusenguse,halafu uniambie hizi number zako za ukuaji wa uchumi zinawiana vipi na hali halisi on the ground,pls karibu huku
 
Mtoa hoja ningependa nikualike uje huku Lingusenguse,halafu uniambie hizi number zako za ukuaji wa uchumi zinawiana vipi na hali halisi on the ground,pls karibu huku
Hiyo Sehemu iko wapi mkuu?

Na inashida gani zaidi?

#KAZIIENDELEE
 
Back
Top Bottom