jitombashisho
JF-Expert Member
- Jun 11, 2020
- 667
- 2,245
Hayati Magufuli alikomesha pasi na ajizi maandamo ya aina yoyote tofauti na mtangulizi wake Mzee JK.
Hoja yake kubwa Hayati Magufuli kuhusu kuzuia maandamo ilikuwa ni muda wa kufanya kazi na haukuwa muda wa kuandamana. Aliweza.
Ndipo kipindi ambacho kwa takribanI miaka mitano si wanavyuo, vyama vya upinzani na pia wanaharakati si tu hawakuthubutu kuandamana bali pia waliufyata kwa sababu JPM alitisha na alisimamia vyema kila alichokiamini.
Sasa basi, kipimo sahihi cha uungwana wa huyo mama hasa kwenu mnaomsifia upo hapo mtakeni awaruhusu japo muandae maandamo ya kumpongeza kwa kuruhusu wafanyabiashara wabembelezwe, kwa kuruhusu madini yachimbwe kwenye mbuga za hifadhi ya Taifa na zaidi amekubali kodi kwa maana ya makusanyo hata ya kipungua hakuna tatizo.