Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Rais Samia Suluhu ateua Wabunge wapya watatu na kuteua Baraza la Mawaziri

Kwa hiyo jamaa yangu kaambulia kaUbunge tu!! Ama kweli dunia hii vagosha; yaani ka cheo wiki 3 tu hakapo iiiiiii
 
Wizara ya fedha inahitaji kuongozwa na a seasoned economist asiye na makando-kando ya ushabiki wa kisiasa kama mwigulu nchemba.

Waziri na naibu waziri wa fedha wa sasa, kwa maoni yangu hawatoshi.

I hope watakuwa chini ya uangalizi na usimamizi wa VP Dr.Mpango, vinginevyo tutayumba.
 
Ila nilivyomsikiliza na ninavyohisi ameona aibu kufanya mabadiliko makubwa na kuacha wengine (japo siyo dalili nzuri). Anaona kama akibadilisha na kuacha wengi ataeleweka vibaya. Akizoea hicho kiti anaweza kuja kufanya mabadiliko makubwa, may be. Ila kwa kumuweka Mwingulu fedha amechemka sana. Yule jamaa ni ''fix'' mmoja anayeishi kwa ujanja ujanja tu kama Kigwangala. sehmu ambayo amaepatia ni kumwondoa Kabudi wizara ya mambo ya nje. Na kwa Bashiru naona kuna kitu la sivyo asingebadilishwa ukitilia maanani kateuliwa juzi juzi tu.
 
Nakupongeza Dr, L. M. Mchemba kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Naamini elimu na weledi wako sasa utaulekeza katika fani ulio bobea.

Mungu akujalìe hekima na uadilifu wa maamuzi yako katika nafasi hiyo.
Hicho kigugumizi kiko wapi sasa! Mbona sikioni? Au umeshikwa na kigugumizi cha kutoamini kilicho tokea?
 
Mama kasema kumpa mchawi akulelee mtoto ndo huko Sasa..🤣🤣
 
ofisi ya Jafo

Uwekezaji imerudi chini ya ofisi ya waziri mkuu

Ummy mwalimu-tamisemi

Wizara ya fedha -mwigulu nchemba

Sheria- kabudi paramagamba

Mambo ya nje- balozi mulamula

michezo -naibu (gekulu) ulega amerudi mifugo

Afya- naibu wa pili Mwanaidi ally hamisi

Bashiru-mbunge wa kuteuliwa

Zingine zimebaki kama zilivyo.
yule dada wa znz aliyekuwa anakwama kuapa siku ile kaletwa sevlction ya wantotot

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mara ya 9+ leo unaandika kuchukizwa na uteuzi wa Mh. Mwigulu....hebu mpe nafasi kidogo tuone utendaji wake!
hafai mkuu niamini ndio mana jiwe alimuweka kando ili ajifunze ila ambition za mtu huwezi kuzizima sijui kaenda kuloga wapi ila atakwapua hela ajiandae na urais mi genge lake lote nalijua na watu wa usalama pia wanamjua vizuri kinachoniuma atamsumbua mama
 
Wabunge wapya walioteuliwa kuwa wabunge ni pamoja na Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Bashiru Kakurwa Ali, Mbarouk Nassor Mbarouk na Liberata Mulamula.

Rais Samia Suluhu akitangaza Baraza la Mawaziri amesema...

''Kuondoka kwa Mpango kumefanya nifanye mabadiliko kidogo kwenye Baraza la Mawaziri na nitatangaza hapahapa, zege halilali''

Baadhi ya Wizara zimefanyiwa Mabadiliko na nyingine zimebaki kama zilivyokuwa.

MAJINA YA MAWAZIRI WANAOUNDA BARAZA LA MAWAZIRI

Ummy Mwalimu - Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI

Mohammed Mchengelwa - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Selemani Jafo - Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais

Geoffrey Mwambe - Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji

Dkt. Mwigulu Nchemba - Waziri wa Fedha na Mipango

Profesa Palamagamba Kabudi - Waziri Wizara ya Katiba na Sheria

Balozi Liberata Mulamula - Waziri wa Mambo ya Nje

Prof Kitila Mkumbo - Waziri wa Viwanda na Biashara
Afadhali Bashiru kaondolewa ukatibu kiongozi. Asije akatuletea siasa zake hapa.
 
Back
Top Bottom