Yaani wamshukuru sana Mungu ,watu wazima wangeliadhirika, Uhuru Kenyata alicheka na kufurahi kindanindani mpaka mabega yakaanza kurukaruka kisa Rais Samia kalitamka neno,najiuliza mbona alipolitamka yeye Rais wetu Samia hakucheka.
Samia nae alijikaza kisabuni lakini alikuwa tiyari ameshachukuliwa na mkondo wa lile neno,akameza mate.
Sikucheka ila nimefurahi kuona Maraisi wetu wapendwa wamo ndani ya furaha ya pamoja,kama walikuwa maskani vile na mastori ya hapa na pale na kiswahili kikataka kuwaponza mbele ya kadamnasi,kweli yajayo yanafurahisha.