ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,643
- 51,642
Video iko wapi? Wataalamu mnaniangusha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu unaitwa ni 'mhemko au mahaba'.... their Excellencies Samia na Liberata (the ladies) wanawakilisha taifa vizuri sana! Kongole kwao.
... nyota njema?Huu unaitwa ni 'mhemko au mahaba'.
Bado sana kuwapa sifa..tunawasubiri angalao kwa siku mia moja mbele.
Makubwa!!!"Kutia dole"
Kutia dole
Viongozi wenu wanapozungumza kwenye hotuba ,mnatakiwa muwe watulivu sana sana ,unasikiliza mstari baada ya mstari na ndio utaelewa kwa kina,na hata maneno yanayochomekewapia uyagundue,maana mengine yananogesha,nimeirudia na uona hata walinzi wa kike nao waliingia kwenye mkumbo kusikia lile neno,kiswahili kina ufundi kukizungumza,Samia kweli nae alipigilia msumari kivyake.
Yaani wamshukuru sana Mungu ,watu wazima wangeliadhirika, Uhuru Kenyata alicheka na kufurahi kindanindani mpaka mabega yakaanza kurukaruka kisa Rais Samia kalitamka neno,najiuliza mbona alipolitamka yeye Rais wetu Samia hakucheka.
Samia nae alijikaza kisabuni lakini alikuwa tiyari ameshachukuliwa na mkondo wa lile neno,akameza mate.
Sikucheka ila nimefurahi kuona Maraisi wetu wapendwa wamo ndani ya furaha ya pamoja,kama walikuwa maskani vile na mastori ya hapa na pale na kiswahili kikataka kuwaponza mbele ya kadamnasi,kweli yajayo yanafurahisha.
Uzuri wa Magufuri alikuwa apendi unafiki,Wewe unawajua vizuri hao Wakenya? tafuta history toka enzi za Nyerere,mala ya kwanza ndio walivunja jumuia ya africa Mashariki, Ukiona Mkenya anakujifanya anakupenda jiulize malambimbili,kuna kitu anakitafuta, Magufuri alikuwa mtu wa kazi,yeye alikuwa sio mtu wa maneno matamu, ndio maana wakati mwingine alipishana na wenzake kidogo.Uwe unajaribu kusoma between lines!!mtu kusema uhusiano ulidorora sio kama umekufa, ukitaka kulijua hilo nenda kagera pale mtukukura, ukaulizie kilichowakuta wafanya biashara wa kiganda!!hadi sasa bidhaa nyingi watu wa kagera wanafuata KATORO, Ulizia zile safari za aitcl kwenda uganda, ziliishia wapi!!wewe unakazania tu mala bandari kupitisha mizigo, kwani kiongozi wa nchi fulani kuja kwako ndio kuwa hakuna utofauti??KENYATA, alikuja mala ngapi Tz?lakini mbona ndio aliyekuwa muhanga mkubwa , na akaja hadi kumzika kabisa?!!
Hawafai kabisa...kabisa!?????????
Hawafai hata bure.....?????????
Mimi nimestaajabu hawa viumbe wapo JF wanajipenyeza kwenye maisha ya wa Tanzania kwa gharama yeyote!We ni mkenya?
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]Ile aliyonunua Mramba ni chombo cha masafa marefu, kinataka kuikata bahari kadhaa.
Ukisema aitumie ile ndege kwenda nayo Kenya ujue itapitiliza na kwenda kutoa Cairo huko Misri. Ile ndege Huwezi itumia kwa safari za East Africa
Yaani HAWAFAI hata kuwa majirani, eti ndugu[emoji849]Kiboko yenu alikuwa Magu (R.I.P)
Mkizingua alikwa anawazingua[emoji28]
Nyie ni majirani wa kuangalia kwa macho matatu.
Mgaa gaa na upwa hali wali mkavu na kisawe chake ni mwenda Bure sio sawa na mkaa Bure.Naona sasa ni mwendo wa kupukuchulia angani rasilimali za nchi yetu; sasa zile harakati za kupishana angani zinanyemelea baada ya kuzinduliwa rasmi pale kwa M7. Bi Mkubwa hasomeki, kurasa za hotuba na ahadi zake tifutifu & futefute zimefutika.
#Mtanikumbuka kwa mema, na wala si kwa mabaya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameondoka nchini leo tarehe 04 Mei, 2021 kuelekea nchini Kenya ambako anafanya Ziara Rasmi ya siku 2 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta.
#KaziIendelee
======
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amewasili nchini Kenya na kupokelewa uwanja wa ndege na Waziri wa Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Amina Mohammed. Rais Samia amefika eneo la VIP uwanjani hapo na punde anaenda Ikulu ya Kenya na leo atafanya mazungumzo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
Saa 11: 10 Asubuhi: Rais Samia Suluhu amefika Ikulu ya Kenya na kulakiwa na Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta kisha kumtambulisha kwa viongozi kadhaa ikiwemo wa Kijeshi na Polisi. Kinachoendelea sasa ni nyimbo za mataifa mawili.
11:16 Asubuhi: Sasa inapigwa mizinga 21 kwa Rais Samia Suluhu kama Rais mgeni aliyezuru nchi hiyo na baada ya tukio hilo atafanya mazungumzo na Rais wa Kenya.
=======
Kenyatta: Tumepata nafasi ya kuongea mambo mbalimbali, tumekubaliana ya kwamba tutare-energize ile joint commission of cooperation kati ya nchi zetu mbili na mawaziri wetu wameambiwa kwamba wawe wanakutana mara kwa mara kuhakikisha ya kwamba wanaendelea kuzingatia uhusiano wetu na kuweza kutatua shida ndogondogo ambazo zinasumbua wananchi wetu wakati wanafanya biashara kati yao, wakati wanatembeleana kati yao.
Tumepata nafasi ya kuongea mambo mengi ya muhimu pia mambo ya usalama wa nchi zetu na watu wetu na vile tutasaidiana kuhakikisha tuko na usalama kati yetu, kati ya wananchi wetu hasw tukielekeza mambo ya kupambana na ugaidi katika sehemu zetu.
Tumekubaliana pia ya kwamba na kuweka mkataba haswa ya mambo kuhusu kujenga pipeline ya gas kutoka Dar es Salaam mpaka Mombasa na hiyo itarahisisha bei ya stima katika nchi yetu na itasaidia pia kuhakikisha ya kwamba viwanda vyetu industries zetu zinapata Stima na energy ambayo ni environmental friendly.
Rais Samia Suluhu: Tumepokewa vizuri sana njiani, muda mfupi uliopita tumetoka kufanya mazungumzo na Rais Uhuru Kenyatta, tuemjadili mambo mengi kama alivyosema mwenyewe. Ninalotaka kuliweka msisitizo ni lile linalohusu kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya mataifa yetu mawili na hili ndio jambo msingi.
Tanzania na Kenya sio tu ni majirani lakini ujirani wenyewe ni wa kindugu, alisema pia, ukiangalia mipaka inayozunguka Kenya, mpaka wao na Tanzania ndio mkubwa kuliko mipaka ya nchi nyingine zote lakini kwenye mpaka huo, wale wanaaoishi mipakani wako Tanzania, wako Kenya nao wote ni ndugu, kwahiyo uhusiano wetu ni wa kindugu.
Wakati wa mazungumzo yetu, nimemuarifu kaka yangu Rais Kenyatta kuwa Kenya inashika nafasi ya tano kwa uwekezaji ndani ya nchi ya Tanzania ikitanguliwa na mataifa mengi kutoka nje lakini ndani ya jumuiya ya Afrika mashariki, Kenya ni ya kwanza na kiulimwengu inashika nafasi ya tano ambapo imewekeza miradi 513 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 1.7 ambayo imetoa ajira zipatazo 51 elfu za watanzania.
Zipo kampuni 30 za kitanzania ambazo zimewekeza mtaji ndani ya Kenya wenye thamani ya shilingi za Kenya 19,330,000,000 na kutoa ajira kwa watu 2,640 lakini nikaweka ahadi kwamba Tanzania sasa tutakuja kwa nguvu yote Kenya kuja kuwekeza ili kukuza ujazo wa biashara.
Kwenye miaka mitano iliyopita wastani wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ni Shs trilioni moja za kitanzania ambayo bado sio kubwa na tumeweka ahadi kuikuza hivyo katika mazungumzo yetu tumekubaliana kuhusu namna ya kukuza biashara na uwekezaji kati yetu kama mnavyofahamu nchi zetu bado zina fursa nyingi sana.
Lengine aliliongoza mheshimiwa Rais nami nakubaliana nalo, ni kwa mawaziri wetu wa afya kukaa, kuangalia na kurahisisha mfumo wa kuingia na kuchekiwa kwenye mambo haya yaliyoingia ya Covid au Corona, watu wetu wapate huduma za haraka, Kupima na kuchekiwa ili waweze kupita na biashara ziendelee.
Tumegusia pia suala la ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa, huu ni mradi wa muda mrefu, tunashukuru leo tumeweka kidole na kilichobaki ni utekelezaji, tutakwenda kusimamia.
Mwisho ni kwa taarifa yenu waandishi wa habari, mwaka huu ifikapo mwezi December, Tanzania tunatimiza miaka 60 ya uhuru wetu na hivyo nimetoa mwaliko rasmi kwa Rais Uhuru Kenyatta awe mgeni rasmi katika maadhimisho yale ya miaka 60 ya uhuru wetu.
Highlight apo nliposemaKwa hivyo unamaanisha ya kwamba mama pia ni mhuni 😂?
kuna sehemu nimemtaja magufuli kwenye post yangu? kuhusu kutandaza hizo barabara ni kweli magufuli alitandaza kuanzia kipindi cha hayati mkapa hadi JK akiwa waziri wa miundombinu, au nitajie barabara moja tu aliyojenga magufuli ya kuunganisha mkoa na mkoa au za kitaifa akiwa ikulu.Wewe ndio mwenye chuki na Magufuri,uliyesema Magufuri alikuwa na uhusiano mbaya na wenzake wa africa Mashariki,nimekupa facts unaanza kusema hao walikuwa na wivu na Jk,nimekuuliza nitajie rais yupi Africa Mashariki ambaye ajafika Tanzania wakati wa Magufuri,unaanza kutaja wakina Bush,akina Bush walikuwa na biashara zao tu,sindio walikuja kuzindua mitambo yao ya Simbion pale ubungo?Hizo barabara unazosema Magufuri kazitandaza pasipo msaada wa hao Wazungu