Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Jaribu kumfahamu JK, historia yake na namna anavyofanya mambo yake. Umuhimu wake nchini na ushawishi wake katika majeshi.
 
Mleta mada chuki yako wewe kwa Mama Samia kuwa Rais wa Tanzania mwenye asili ya Unguja hakuifanyi CCM ife kwa unabii wako feki.

Samia ataondoka na watakuja wengine watachukua nafasi yake.
 
Hizo ni fikra tu ambazo mtafiti yeyote anaweza kujenga kichwani mwake. Siyo utabiri na wala hakuna hesabu katika yote haya.
Sijatabiri. Ila wapo waliokwisha prophesize huko nyuma..

Kwa hiyo uchambuzi, mtazamo na mawazo yangu haya yako based on that prophecy...

Anyone (including you) unaweza kuyapinga kwa kuyajengea hoja au kwa reference ya prophecy nyingine unayojua wewe..
 
Sawaaa...ila usikimbiee huu uzi wako ifikapo mwisho wa mama samia..mana manabii kama nyie mpo siku zote
 
Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja..toeni kauli zenu za utenganishi kwa kuchuchumilia madarakaa...hakuna kitu kama hichoo..huu muungano ni wa moja kwa moja..wala msitegemee chochoteee...hayo madaraka mnayoyalilia hamtakaa muyapatee hakikaa
 
Mleta mada chuki yako wewe kwa Mama Samia kuwa Rais wa Tanzania mwenye asili ya Unguja hakuifanyi CCM ife kwa unabii wako feki.

Samia ataondoka na watakuja wengine watachukua nafasi yake.
Point of correction...

Kwanini niwe na chuki na Rais Samia Suluhu Hassan...??

Umesoma kweli andiko langu kuu lote kwa umakini na kuelewa mantiki (logic) ya hoja yangu..?

Mimi nimetoa maoni na mtazamo wangu tu, sijatukana mtu wala kumsimanga mtu..

Lakini katika kutoa maoni juu ya nchi yangu hii, utawezaje kutoitaja CCM na Rais wa sasa Ndg Samia Suluhu Hassan ili kuweka mizani sawa ya maoñi/uchambuzi...?

Mimi nasema, kwa namna ninavyoona na kwa namna mambo yalivyo na kwa kuitazama critically historia ya nchi yetu, kuna kila dalili kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ndiye alama ya mwisho ya utawala wa CCM katika siasa za Tanzania...!!

What's wrong with that? Unaweza kunipinga, wala sina tatizo kabisa mimi...

Karibu
 
CCM sio ya kufa leo wala kesho mkuu. Ipo sana tu.

Kama kufa ingekufa awamu ya nne ya Kikwete walipolazimika Kinana na Migiro kwenda kwa wananchi kwa lengo la kurudisha imani.

Ni chama ambacho kipo chini kabisa kikifanya siasa muda wote tofauti na vyama vya msimu vya wapigaji wa pesa za wafadhili.

Ni chama ambacho wanachama wake wapo kivitendo tofauti na hizi mbwembwe za threads za humu jukwaani.
 
Sawaaa...ila usikimbiee huu uzi wako ifikapo mwisho wa mama samia..mana manabii kama nyie mpo siku zote
No, sitakimbia

Tuliyasema ya Magufuli. Mlibisha sana. Mkaanza kuandaa mpaka sherehe. Mkaanza kumtengenezea mpaka utaratibu wa kuwa Rais wa milele...

Leo yuko wapi?

Hawakuweza kutambua alama za nyakati. Yaani maarifa na akili zenu zilifunukwa na KULA na KUNYWA kwenu bila kuona hatari iliyokuwa mbele yenu. Dunia yenu imeishia hapo kwenye kula na kunywa...

Hamkujua kabisa kuwa huyo mtu alikuwa anatengeneza njia za anguko kuu la utawala wa siasa za CCM hapa Tanzania..!

Ndugu, tulia. Sisi wengine tulishauona mwisho hata kabla ya....
 
"Ipo sana tu". Hadi lini ndugu? Je hadi 2022? Je hadi 2025? au hadi 2050...?

Anyway. Whatever. La muhimu ni kuwa that's what you believe...

Labda swali langu kwako ni hili;

What makes you believe that?

Ukiwa na muda na unapojibu swali, hili itapendeza sana kama utarejea hoja za msingi ktk mada yangu kuu...
 
CCM walichokifanya Oktoba 2020 ndio niliona bado tuna hali ngumu. Walipanga na wameweza kuchukua majimbo kiulaini sana.
Wasiwasi wangu kuwa si upinzani wala raia walikuwa wanaliona hilo kutokea. Katika nchi yenye waongo kweli mkapanga mpango haramu na kufanikiwa kwa kishindo si jambo la kubeza.
Sijaona upinzani wala wananchi wakiwa wamejipanga kushindana na nguvu hii. Hizi tunaandika mtandaoni tu.
 
Kuna watu watautafuta huu uzi after some years to come

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono maono haya adhimu. Wachache wataelewa, maana kwa sasa taifa liko kwenye hali ngumu na wakulaumiwa ni mama wakati uharibifu wa mambo umefanyika kitambo.
 
Kuitoa CCM madarakani ni ndoto za mchana. Wapinzani wana hoja nyepesi sana na wananchi wa kawaida ambao ndio majority hawajawahi kuwaelewa na wala hawawaungi mkono. Upinzani una nguvu mtandaoni na sio ndani ya jamii. Ninazo facts katika hili.

Namna pekee ya CCM kutoka madarakani ni Mgogoro wa ndani ya chama wa wenyewe kwa wenyewe, tena msuguano mkali utakofanya ipasuke vipande vipande.

Hata hivyo kutokana na CCM kuweka msingi imara tangu kuasisiwa mpaka leo kuwa taasisi kubwa yenye nguvu, hivyo dhana ya mgogoro utakaopelekea ipasuke inakuwa ndogo. Rejea Lowassa na Membe walivyojaribu kuivimbia CCM.

Hii ni kwa sababu hakuna aliye mkubwa ndani ya chama kama lilivyo jina la CCM. Na hakuna chama Afrika nzima kinachoheshimu katiba yake, miongozo na kanuni kama CCM.

CCM haina mwenyewe kama vilivyo vyama vya msimu. Ndio maana kiongozi mstaafu wa CCM anaheshimu uongozi uliopo hata kama aliwahi kuwa Mwenyekiti. Hii inaonesha ukomavu wa CCM.

Sikisifii sana chama tawala lakini nimejifunza mengi kwenye chama tokea nikiwa mtoto na nakifananisha na kanisa katoliki. Ni sawa na kifikiri kanisa katoliki litadhoofishwa na makanisa ya kilokole yanayoibuka yenye kumsujudu mtu mmoja (kiongozi mwanzilishi) kwa tegemeo la kuiangusha Roman empire ambayo ni taasisi iliyoshamiri kila kona.

Mleta post amka kumekucha. Ndoto za mchana sio nzuri. CCM haiwezi kung'oka kwa nadharia zako mfu.
 
Mama amezungukwa na manyang'au
Manyang'au ya Kwanza ni Yale yanamshauri mama atumia mbinu tofauti za kumpana na Corona,maana wanajua zitatupeleka tu kwenye lockdown Kama ilivyo Kwa Uganda na Rwanda kwa Sasa.
Hapo ndo shughuli itaanza kuwa pevu,maana kuvaa barakoa tu imekuwa ngumu pamoja na amri kutolewa.
 
Ungeujua upinzani na ukinzani uliopo miongoni mwa wanaccm tena wazito usingeandika ulichoandika,kama ni volcano basi imeshaanza kutoa mvuke mdogo mdogo. Muda ni Mwalimu mzuri sana.
 
😄🤣🤣🤣🤣CHADEMA hawataki kusikia ukweli huu.
Hivyi kwenye wenyeviti vya vyama vyao wameng'ang'ania ukiwapa Ikulu si watafia happy Kama kupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…