Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Rais Samia Suluhu Hassan ampa onyo Waziri wa OR-TAMISEMI, Selemani Jafo

Tibalikwenda

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
284
Reaction score
604
Mh. Rais amesema Wizara ya Tamisemi ina matumizi ya ovyo ya pesa za Serikali, yenyewe haikusanyi ni mwendo wa matumizi kwa kwenda mbele hivyo kamwagiza Waziri Jafo afuatilie vizuri matumizi ya wizara yake na kama akishindwa Basi asaidiwe(atumbuliwe)

TAMISEMI.JPG

Ushauri.

Mh Seleman Jafo jipange; Halmashauri, Hospitali,miradi ya ujenzi wa shule n.k hela zinapigwa sana, vituo vya afya EFD mashine hazitumiki vilivyo. Fuatilia Mama Samia hatakuhurumia atakutumbua shauri yako.
 
Yaani juzi tu wala maboga walibwatuka kuwa jiwe ni Rais pekee aliyeweza kuikoa Tanzania na genge la wezi.

Hata kabla hajaoza kaburini anaonekana ni mwizi. Tulisema mapema tukaonekana wasaliti kiko wapi sasa.

Cha ajabu wala maboga wanajinadi mtaani kuwa kimetoka chuma kimeingia chuma.

Acha kwanza nitafakari hizi kauli labda uwezo wangu wa kuwaza unaanza kuchoka.
 
Hii ni mara ya pili huyu waziri wa TAMISEMI anahonywa mbele ya hadhara kwamba abadilike katika utendaji wake.

Kwa kauli ya leo kutoka kwa Rais Samia Suluhu, Jaffo anatakiwa kujizuru nyazifa zake.

Kakini pia huyu Jaffo ana nini cha mno mpaka aendelee kupewa maonyo kila siku juu ya utendaji wake na usimamizi wa mali za umma?
Katika hili Jaffo unatakiwa utumie hekima na busara kuiacha TAMISEMI, kiuhalisia wizara hii kubwa imekushinda.
 
Praise and Worship gang walishasema Jaffo ni Rais wa JMT anayesubiri muda tu. Leo tena hafai, jamani!!!

Kumbe manyani ni sahihi kushangilia bila kuhofia kufa make kama njaa imetupiga miaka 5 bila kufa sembuse hii miaka 4 iliyobakia ya awamu 5.
 
Punguza speed ili uandike kitu chenye "CONTENT" Makosa ya kiuandishi yanaweza kuondoa credibility yako!!

"Anahonywa" sijui kiswahili gani hiki, huwa nakereka sana na watu msioweza kujua matumizi ya herufi"h"

Anyway, kujiuzuru ni rahisi kuizungumza, hata hivyo watajiuzuru wangapi? Kwakuwa amepewa nafasi nyingine ya yeye kufuatilia agizo hilo, tusubiri utekelezaji wake kisha tutahoji nafasi yake ya uwaziri!!

Ahsante!
 
Jafo mbona alikuwa busy sana kukagua miradi mbali mbali iliyo kuwepo tamisemi ..binafsi nahisi shida ipo ktk halmashauri na tawala za mikoa husika.

Pengine ukaguzi wa ndani unashida pia. Lakini binafsi naona bado Jaffo ana paswa awe na msaidizi mkali mwenye uzoefu zaidi kuliko wanaomsaidia sasa maa naTammisemi ni kubwa mnoooo. Pengine ipewe ma naibu mawaziri wawili
 
Huyo Jaffo aliwahi kumpiga mkwara yule Mhandisi wa watu wa barabara kule Arusha na kutaka ahamishwe mara moja, kisa tu hakuleta wananchi wengi kuja kushuhudia uzinduzi wa barabara!

Na kwa mtazamo wake, akaona huyo Mhandisi anamhujumu Rais wake eti kwa Wananchi! Maana yeye Jaffo angehutubia watu wachache! Hatari sana.
 
Kiukweli waziri wa tamisemi inafaa awe engineer wa kusomea kabisa maana ujenzi ni mwingi tizama mbezi stand BOQ ikasukwa kupigwa bil 15 sasa wamepiga ngapi nani anajua?? huyu bitozi masuti itamtesa apewe kawizara ka mazingira na usafi
 
Nimeshtushwa na tuhuma za rushwa za TAMISEMI, niliwahi kushauri na Sasa nashauri Mhe. Rais ajitenge na TAMISEMI amwachie Waziri Mkuu ili iwe raisi kwake kuimulika. Ikiwa chini yake ikatuhumiwa ametuhumiwa na nivigumu kumwajibisha maana baadhi ya nyaraka zao anakuwa kazipitisha yeye.

Wizi wizi wizi umekuwa mwiba kwa taasisi zetu, hakuna usafi inategemeana Nani yupo
 
Back
Top Bottom