Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Nilidhani yeye anakwenda kufanya yale atakayoagizwa na Rais kuyafanya, je ilikuwa sawa kuahidi yale aliyoyaahidi kufanya kabla ya kujua muelekeo wa boss wake?
Kwani ameahidi nini zaidi ya kupambana na umasikini na kuendeleza miradi iliyopo (ambao ndiyo mueleleo wa serikali ya CCM)? Hakuna ahadi mpya aliyotoa zaidi ya kupima mulemule alipopita Mama.
 
Philipo Mpango anaongeaga kama padri, ni mtaratibu na mpole, hana kiherehere, hana tamaa za madaraka na anajua kusimamia kazi yake kwa utimilifu na utaalam wa kiwango cha hali ya juu.

Pia sio mtu wa kujionesha wala sio mtu wa kujipendekeza na kujikomba ili apewe cheo, yeye haombagi wala hatafutagi vyeo na kazi bali vyeo na kazi ndo humtaftaga yeye.

Wanasiasa, wabunge na watu wote mjifunze na kutoa mfano kwa Phillipo Mpango
 
Hata hivyo, katika kumnukuu kwangu kila alichokuwa anakiahidi alikua anaweka maneno kwa kumshauri na kusaidiana na mh Rais wa Tanzania, maana yake hapo anajua nani ambaye yupo juu yake na yeye kama kiongozi mkuu wa pili wa nchiii hii baada ya mh Rais
 
Sifa no.1 ya Rais wa JMT ninae mtaka, Mawazo yake Watu wasiweze yatabiri

JPM alikua rais wa Ndoto zangu,sasa Sifa no.1 niliyoitaka na sasa naiona kwa

Mama,nilijisemea moyoni "endapo Mama ata pendekeza 1 ya majina niliyokua

nayasikia huku mitaani yakizunguka,ningeachana na CCM na kubaki sina chama"

kwa pendekezo hili,amenionyesha kwamba ana sifa.no 1 ya Rais ninae mtaka "Unpredictable"
 
Alipaswa aseme ataongea zaidi baada ya uapisho

Vipi Kama Rais akiamua Leo usiku kubatilisha uteuzi wake kwa sababu fulani fulani.

Unless wawe washaongea

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Tushawastukia nyinyi sukuma gang sasa hivi ndiyo mmeanza kuomba msamaha kwa wa Tanzania baada ya kuona mama Samia kaingia madarakani...
Let's say afuate mawazo yako achukie hao wasukuma kama wewe..hizo kura za kuendelea kuongoza 2025 atazitoa wapi? Au umesahau kanda ya ziwa ndio ina kura ya turufu ya Urais?
 
Wewe ndio katika lile kundi la watu wasioijua njaa,🤲eti tusiombe kuongezewa mishahara.Nyie ipo siku mtaijua njaa Kwa Uwezo Wa Muumba Mbingu na Ardhi.
Mimi ningekuwa wa kwanza kuwaunga mkono ili muongezewe mishahara kama mngekuwa mnafanya kazi yenye matokeo chanya yanayopimika,kwa sababu nalipa kodi kwa lengo hilo. Sitaki kujua wewe uko ofisi gani au Idara ipi, ila naomba unitajie Idara moja tu huko Serikalini unayoamini kuwa watumishi wake wanajituma hadi kustahili nyongeza ya mshahara..... Hakuna! Sasa mnaomba kuongezewa mishahara kwa kazi gani mnayoifanya?.
 
Kwani ameahidi nini zaidi ya kupambana na umasikini na kuendeleza miradi iliyopo (ambao ndiyo mueleleo wa serikali ya ccm)? Hakuna ahadi mpy aliyotoa zaidi ya kupima mulemule alipopita Mama.
Kwa nini aseme nchi ina masikini wengi????
Ufafanuzi please!
 
Muonee tu huruma! Athari za ule ugonjwa bado hazijaisha mwilini mwake kwa 100%
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM, sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni Rais anayetokana na CCM na anatekeleza ilani ya CCM.

Godbless Lema, Tundu Lissu hawazungumzii kabisa maendeleo ya Chadema, wao ni bize kumpangia cha kufanya Rais Samia.!

Tundu Lissu ni kaimu mwenyekiti wa Chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza Chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa CCM Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lissu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake, yeye ni kuchafua tu nchi yake.
 
Let's say afuate mawazo yako achukie hao wasukuma kama wewe..hizo kura za kuendelea kuongoza 2025 atazitoa wapi? Au umesahau kanda ya ziwa ndio ina kura ya turufu ya Urais?
Hizo ni akili za kichaa
 
Back
Top Bottom