Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Ccm ni ile ile,tunahitaji katiba mpya tu,kama kweli mama anatujari sisi wanyonge
 
Nilidhani yeye anakwenda kufanya yale atakayoagizwa na Rais kuyafanya, je ilikuwa sawa kuahidi yale aliyoyaahidi kufanya kabla ya kujua muelekeo wa boss wake?
Boss wake alishasema kuwa naye ataendeleza zote yale mwendazake alipania kuendeleza!! Mpango hakusema kitu tofauti na Rais aliyoisha yasema; acheni fitina!!
 
Kwani katukana MTU?. Tafuteni picha za Dr Shein Yuko airport baada ya kuteuliwa Makamu WA Rais alikuwa analia. Huyu kajitahidi Sana.
 
Kama ilivyokuwa 2015 kwa JPM ,sasa hivi tena Chadema wako bize kumsifia, kumfundisha na kumpa maelekezo mbalimbali Rais Samia bila kujua kuwa huyo ni rais anayetokana na ccm na anatekeleza ilani ya ccm.

Godbless Lema ,Tundu Lisu hawazungumzii kabisa maendeleo ya chadema wao ni bize kumpangia cha kufanya rais Samia. !

Tundu Lisu ni kaimu mwenyekiti wa chadema lakini hutakaa usikie akiiongelea wala kuitangaza chadema popote. Kwani haoni kaimu mwenyekiti wa ccm Philip Mangula anavyokinadi chama chake?

Tundu Lisu ni mtanzania lakini hutakaa usikie popote akizungumzia mazuri ya nchi yake ,yeye ni kuchafua tu nchi yake.
Acha afagie uchafu uliokithiri Kwanza ukiisha atazungumza mazur ya Tz
 
na nakumbuka atcl walitoa gawio.takriban kama 28b.
my question ile ilikuwa hoax.
campain? ama smoke screen kufurahisha legacy yake?
kwa maana yoyote ile alidanganya, evn though naamini ukweli aliujua.
Pale huwezi kusema kuwa alidanganywa,no ilikuwa planned kabisa
 
Hii si ndio ile nafasi ya kutembea na mikasi? Muda mwingi shughuli kubwa ni kufungua majengo na makongamano tu? Naona mchumi kaja kupumzika huku!
 
Nilidhani yeye anakwenda kufanya yale atakayoagizwa na Rais kuyafanya, je ilikuwa sawa kuahidi yale aliyoyaahidi kufanya kabla ya kujua muelekeo wa boss wake?
Kuna mchezo sio wa bahati mbaya ila swala la kila wakati watu sifia marehemu Kama vile mpaka muda huu hatuna serikali mpya, sio mzuri naweza sema Kuna agenda ya kikundi flani na haya yanatoka karne hii, hivi mbona kipindi kile Mwl. Nyerere ameacha kiti mrithi wake, au Mkapa KWA mrithi wake hatukusikia, na je ni kwamba mh kikwete alitenda mema zaidi mzidi mtangulizi wake au mh Mwinyi alitenda zaidi mzidi Mw Nyerere, kola uongonzi na Zama zake,KWA siku hizi Chache Kama anasimama na kuona marehem bado ni zaidi ya uongozi uliokabidhiwa nchi ni muogopen Kama ukoma na ni lazima ashughulikie haraka, anachofanya ni kuaribu psychology ya viongozi walio madarakani,

Kusifu kuabudu pia KWA Muhimili yetu hakusaidi lolote na hatuwezi songa Kama taifa ,hivi inakeje bunge lenye wabunge 300 et mteule vp anapata asilimia 100 ,kwamba katika wabunge wote fikra zenu ni level sawa, ndio kupitia sio tatizo ila why kuaminisha dunia kitu ambacho hakiwezekaniki? Hata baba ndani ya familia sio kila Jambo anaweza sema likaungwa mkono KWA asilimia 100 sembuse bunge lenye watu tofauti,sifa tofauti, hii ni aibu,

Tumeona nchi mfano SA hata Rais mda mwingine anawekewa ungangari je ili TZ KWA bunge letu Lina weza kweli pale panapo stahili. Nilitoa wazo hapa jf ili kupata bunge la kumsaidia Rais na nchi bila kujali ghalama livunjwe, ni vichekesho,maana watu au nchi dunian wanatushangaa nakuona kila mtanzania thinking capacity ni sufuli,
 
CCM haitakuletea ajira hata siku moja mkuu, haya maisha pambana kivyako tu make kila mtu yupo hapo madarakani kutimiza ndoto zake.

Pambana kutimiza ndoto zako. Wengine tumaini letu tunahtaji haki iliyopotea kwa miaka 5 irejee ili tuzipambanie familia zetu.
 
Muonee tu huruma! Athari za ule ugonjwa bado hazijaisha mwilini mwake kwa 100%
Alijuaje kama kura za kumpitisha kuwa makamu zitatosha hadi awe na uhakika wa kuhutubia bunge kwa uhakika vile?
 
Hajahutubia Mkuu..

Ameliaga tuu bunge Chief

Ndo maana amesema atalimiss sana bunge!..sasa ulitaka aondoke kimya kimya ilihali wameshirikiana wote kule Bungeni kwa kipindi chote? How?
Aliliaga bunge kabla ya kujua kama kama wabunge watampitisha au la..
 
Kwani ameahidi nini zaidi ya kupambana na umasikini na kuendeleza miradi iliyopo (ambao ndiyo mueleleo wa serikali ya ccm)? Hakuna ahadi mpy aliyotoa zaidi ya kupima mulemule alipopita Mama.
Kuendeleza miradi iliyopo au la ni baada ya kukutana na Rais au Baada ya Rais kuhutubia na kuufahamu mwelekeo wake. Anajuaje kama Rais hana mpango wa kuendelea na miradi hiyo kama ilivyo? Inawezekana kuwa Amepre-empty hotuba ya Rais. The cat before the horse.
 
Sasahivi hakuna ahadi. Ahadi ziliisha mwaka Jana .
Saivi utekelezaji wa ilani
Mbona kuna Rais ambae aliwahi kusemaga kuwa ilani aliyopewa haitekelezeki, alifanywa nini? Hakuna mtu yeyote anaweza kumlazimisha Rais Samia atekeleze ilani na ahadi za JPM kama ilivyo. Maana baadhi ya ahadi inawezekana nyingi zililalia upande mmoja tu wa nchi. Mh. Rais hawezi kuwa mtumwa wa ahadi za mtangulizi na ilani.
 
Ata hivo,katika kumnukuu kwangu kila alichokua anakihaidi alikua anaweka maneno kwa kumshauri na kusaidiana na mh Rais wa Tanzania maan yake hapo anajua nan amby yup juu yake na yy kama kiongozi mkuu wa pili wa nchiii hii baada ya mh Rais
Nenda karudie tena kusikiliza alichokisema mara ya kwanza na mara ya pili alipopewa fursa ya kuhutubia
 
Back
Top Bottom