Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Rais Samia Suluhu Hassan ampendekeza Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lamthibitisha kwa 100%

Kama ulimsikiliza alisemaje juu ya upinzani? Angalia hata Gazeti la Mwanachi la leo 31/013/2021 ukurasa wa kwanza. Au huwa hujui namna ya kumsikiliza msemaji. Usiwe unachati wakati unasikiliza hotuba muhimu.
sawa, ndo mana nikasema kama ameiongelea upinzani kwenye namna tofauti (mbaya) hapo alikosea lakini kwenye maelezo haliyoyatoa. yalikuwa ni kushilikiana na Mh. Raisi katika kusimamia na kuliendeleza taifa..

Usitembee na tafsili zako mzee.
 
Katiba yetu hairuhusu hivyo unavyotaka, Rais kwa mujibu wa katiba yetu ni kila kitu na hakuna chombo kinachoweza kumpangia cha kufanya wala cha kusema. Alichofanya Mh. Mpango kama angekuwa amenfanyia JPM hivyo sasa hivi tungekuwa tunaongea habari nyingine. Kama unadhani katiba inatakiwa iruhusu hivyo huna budi kuibadilisha kwanza ili iruhusu hiko.

Binafsi sina tatizo na Dkt Mpango kwakuwa ni miongoni mwa viongozi wenye afadhali kwenye serikali iliyopo. Hana makundi na ana hofu ya Mungu, lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba baada ya kupitishwa angeishia kulishukuru bunge na Rais kwa uteuzi na kuahidi kumsadia Rais kikamilifu kwenye majukumu atakayopewa na boss wake. Ikumbukwe kuwa mama Samia halazimiki kufanya kama alivyofanya JPM hasa kwenye mambo ambayo hayavunji katiba. Mfano, Rais Samia halazimiki kuwaachia machinga wachafue mazingira ya mitaa, stendi, masokoni, na kila pahala kama alivyofanya JPM. Mama Samia halazimiki kuacha kuangalia hali ya kipato cha wafanyakazi kama alivyofanya JPM kwa miaka 6. Lazima atatafuta viatu vyake vinavyomtosha yeye kama yeye. Hivyo, usitegee kuwa atafanya kila kitu alichofanya JPM, alichoahidi JPM na kila kilichomo kwenye ilani. Ziko ilani ambazo hazitekelezeki kwa 100% bila ya kuathiri sehemu nyingine muhimu pia. Rais inalazima kuifuata katiba kwa 100% lakini sio ilani (manifesto), hata Rais Mkapa alilisemaga hilo la ilani isiyotekelezeka. Kama ilani zingekuwa zinatekelezwa kwa 100& tangu 1961 sasa hivi kusingekuwa na kijiji Tanzania kisichokuwa na maji, umeme, kituo cha afya, barabara, shule na kilimo cha jembe la mkono.

Tusimbebeshe Rais Samia zigo la JPM ambalo pengine lilikuwa linatekelezwa ndivyosivyo, lazima tathimini ifanyike kwanza ili kuona lipi liendelee na lipi liahirishwe na lipi liachwe kabisa na lipi liliachwa lakini lifufuliwe na sababu zitolewe. Mfano, Mama Samia atalifanyia haki taifa lake kama ataanza kwa kukamilisha uandikaji wa katiba mpya. Hata mafanikio yanayopatikana lazima yalindwe kwa Katiba na sio kwa kulia machozi ya kumuenzi kiongozi. Katiba ndiyo itoe muelekeo wa taifa kwa kila kiongozi anayepokea kijiti na sio kwa kutumia huruma, machozi, utashi, nyimbo za maombolezo, ukanda, mizengwe, udini na ukabila wa kundi fulani.
Katiba yetu hairuhusu mtu anayependekezwa kuwa Makamu wa Rais kusema priorities atakazozisimamia ni zipi?

Unaelewa ile ilikuwa ni interview kabla ya kupewa kazi?

Unataka mtu apewe kazi bila kufanyiwa interview?

Yani kama Dr. Mpango anataka kuua watu, unataka asipewe nafasi ya kusema ataua watu ili wabunge wajue huyu hafai na kumkataa?
 
MKuu katiba aitaki hivyo lakiini ujue?
huy ni wa kutumwa na kumnyenyekea Raisi wake tu.
Katiba imesema mtu anayeteuliwa kuwa Makamu wa Rais atafanyiwa confirmation na bunge.

Sasa wewe unafikiri confirmation inafanywa vipi?

Anawekwa mbele anaangaliwa sura kama ana tabasamu zuri au baya?

Confirmation maana yake anapewa job interview, yani hata kama akisema "Mimi mkinipa u Mkamu wa Rais, siku ya kwanza naenda kumuwekea sumu kwenye chai rais, afe, ili mimi niwe rais mara moja" ni sawa.

Kwa kusema hivyo ndivyo wabunge watajua anataka kufanya nini na kupata uwezo mzuri wa kumkubali au kumkataa.

Unataka kwenye confirmation process afiche anachoona ni priority?
 
Katiba yetu hairuhusu mtu anayependekezwa kuwa Makamu wa Rais kusema priorities atakazozisimamia ni zipi?

Unaelewa ile ilikuwa ni interview kabla ya kupewa kazi?

Unataka mtu apewe kazi bila kufanyiwa interview?

Yani kama Dr. Mpango anataka kuua watu, unataka asipewe nafasi ya kusema ataua watu ili wabunge wajue huyu hafai na kumkataa?
Kazi yake ni kumsaidia na pengine kumshauri tu Rais basi, Rais anaweza kuamua kuwateua wapinzani kwenye serikali yeye atafanya nini na keshasema wapinzani ni wabaya?
 
Kazi yake ni kumsaidia na pengine kumshauri tu Rais basi, Rais anaweza kuamua kuwateua wapinzani kwenye serikali yeye atafanya nini na keshasema wapinzani ni wabaya?
Sijakuuliza kazi yake ni nini.

Nimekuuliza katiba yetu imekataza mtu anayependekezwa kuwa Makamu wa Rais kueleza priorities zake ni zipi?

Unaelewa kwamba yule aliyesimama bungeni alikuwa Waziri wa Fedha bado alikuwa hajawa Makamu wa Rais kwa kuwa hakuwa confirmed na Bunge wala kuapishwa?

Wapi Katiba imesema mtu anayekuwa confirmed kuwa Makamu wa Rais asieleze priorities zake ni zipi?

Weka hicho kifungu cha katiba hapa tukijadili.
 
Sijakuuliza kazi yake ni nini.

Nimekuuliza katiba yetu imekataza mtu anayependekezwa kuwa Makamu wa Rais kueleza priorities zake ni zipi?

Unaelewa kwamba yule aliyesimama bungeni alikuwa Waziri wa Fedha bado alikuwa hajawa Makamu wa Rais kwa kuwa hakuwa confirmed na Bunge wala kuapishwa?

Wapi Katiba imesema mtu anayekuwa confirmed kuwa Makamu wa Rais asieleze priorities zake ni zipi?

Weka hicho kifungu cha katiba hapa tukijadili.
Unapopewa Kazi lazima ujue vision, mission, values na objectives za mwajiri wako kwanza kabla ya kusema priorities zako, priories za mwajiri ndiyo priorities zako vinginevyo labda uache Kazi.
 
Unapopewa Kazi lazima ujue vision, mission, values na objectives za mwajiri wako kwanza kabla ya kusema priorities zako, priories za mwajiri ndiyo priorities zako vinginevyo labda uache Kazi.
Sasa hao wabunge wanaopiga kura za kumkubali au kumkataa Mpango wangejuaje kama anajua vision ya muajiri wake bila yeye kujieleza?

Kuna priority gani aliyoisema Dr. Mpango ambayo ni tofauti na priority ya Rais na ilani ya CCM?
 
Jina hilo limepelekwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Kanali Nyamburi Mashauri, na kukabidhiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai akisoma ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema..

Mheshimiwa Spika, nawasilisha Bungeni Jina la Mheshimiwa Philip Isdori Mpango kwa Nafasi ya Makamu wa Rais Tanzania.

Soma >>Wasifu wa Dkt. Philip Isdor Mpango


Bunge lamthibitisha kwa kishindo
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemthibitisha Dkt. Philip Isdor Mpango kwa asilimia 100 kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kura zote 363 za wabunge waliopiga kura.







Dk Philip Mpango alizaliwa July 14, 1957 alikuwa ni Waziri wa Fedha na Mipango katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Mpango ni mzaliwa wa Kigoma, baba yake ni marehemu Isidori Nzabhayanga Mpango, ambaye alizaliwa Kijiji cha Kasumo, Wilaya ya Kasulu. Dk Mpango alizaliwa hapohapo Kasumo na ni kaka mdogo wa Askofu mstaafu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanganyika Magharibi – Kasulu mkoani Kigoma, Dk Gerard Mpango.

Dk Mpango ni mchumi mwenye shahada ya uzamivu ya uchumi.

Kuanzia miaka ya 1990 hadi 2000, alifanya kazi akiwa mhadhiri mwandamizi wa uchumi katika kitivo cha Biashara (sasa Shule ya Biashara) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Alikuwa akifundisha “Microeconomics”,

“Macroeconomics” (kwa mwaka wa pili) na “Public Finance” kwa mwaka wa tatu na kozi za uzamili.

Amewahi kuwa Mchumi Mwandamizi wa Benki ya Dunia, Mkuu wa Kamati ya kumshauri Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuhusu masuala ya uchumi, Katibu binafsi wa Rais anayeshughulikia masuala ya uchumi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kabla ya kuhamishiwa Tume ya Mipango, Ofisi ya Rais. Nyadhifa hizi zote amezishika wakati wa utawala wa Kikwete.

Hayati Magufuli alipoingia madarakani alimteua kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na baada ya siku chache akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Dk Mpango ni kiongozi mwenye msimamo thabiti. Baadhi ya watendaji ambao wamewahi kufanya kazi chini yake kwenye ofisi ya Rais wanamuelezea kama mtu anayetaka waliomzunguka wazungumze kwa takwimu na ushahidi hasa katika masuala ya uchumi. Msimamo huo pia aliuonyesha alipokuwa mtaalamu wa Benki ya Dunia. Hakuwa mwoga kuieleza ukweli Serikali pale ambako ilikuwa haifanyi vizuri.

Mathalan, wakati wasomi wengi wa uchumi wakiwa wanapiga kelele za kuisifia Serikali juu ya ukuaji wa uchumi miaka ya mwanzoni ya 2000, Dk Mpango alieleza wazi kuwa lengo hilo la kukuza uchumi kwa asilimia 5.9 haliwezi kufikiwa kwa sababu katika miaka minne iliyopita, Serikali ilishindwa kulifikia.

Alisema: “Angalia kwa miaka minne hadi mitano iliyopita ambayo tulikuwa na sera nzuri za kibajeti, hakuna mwaka ambao ukuaji huo ulifikiwa, hizo ni dalili tosha kwamba hali hiyohiyo ndiyo itajitokeza mwaka huu.”

Born – July 14, 1957, Kasumo, Kigoma region

Education
*1993-1996 University of Dar, PHD Economics
*1990-1992 Lund University, PHD Course Work, Sweden
*1986-1988 University of Dar, Master in Economics
*1981-1984 University of Dar, BA Economics
*1976-1977 Ihungo High (A) Bukoba
*1974-1975 Itaga Seminary (O) Tabora
*1971-1973 Ujiji Seminary (O) Kigoma
*1968-1970 Munyama Primary Kigoma
× 1965-1967 Kasumo Primary Kigoma
*1964-1965 Kipalapala Primary Tabora

Mpango’s Career
*1980-1980 Public relations assistant, National Provident Fund
*1980-1981 Research assistant, Elimu Supplies Ltd
*1984-1988 Economist, Ministry of Labor
*1988-2002 Economics Lecturer Dar-es-Salaam University
*2002-2006 Senior Economist World Bank
*2007-2009 Economic advisor to the President, President’s Office
*2009-2010 Deputy Permanent Secretary, Ministry of Finance
*2010-2015 Executive secretary, President’s Office Planning Commission
*2015-2015 Acting Commissioner General, Tanzania revenue Authority
*2015 – Appointed Member of Parliament
*2015 – Minister of Finance and Planning

Mipango yupo wapi?
Naombeni namba yake ya watsup.
 
Back
Top Bottom