Rais Samia Suluhu Hassan kulihutubia Taifa - Desemba 8, 2021

Rais Samia Suluhu Hassan kulihutubia Taifa - Desemba 8, 2021

Asisahau kuitakia kheri timu ya Taifa Simba sport club siku ya jmosi itakapokuwa inakwaana na timu kutoka Mogadishu....
Timu za wanaume TZ shida tupu! Wanawake kila siku wanashinda, wanampiga hadi msouth kwao! Hadi walemavu nao wanashinda na kwenda kombe la dunia! Ila hii mijamaa akina Samatta, Bokko na wenzao shida tupu
 
Yule jamaa wa kigoma yupo kweli?

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
Leo timu yote unayoijua wewe (Wenye nchi) watakuwepo! Ndugu yangu Polepole atakuwa anachungulia kwenye kile kideo chake anachofundishia! BTW Mkigoma alikuwa Singapore two weeks ago, kapiga show moja matata sana
 
Anahutubia Taifa siku moja kabla ya sikukuu🤔🤔,kwann asisubiri kesho ili awachane vizur wanaomkosea!!Ni kuchanana tu hamna namna
 
Kuna nini, mbna taarifa ya ghafla Kama msiba?
huo utaratibu ndio sahihi.ni kama mkapa na jakaya walivyoasisi desturi ya kuhutubia taifa kila mwezi.

Desturi hii idumishwe.
sio kuongelea mambo serious ya nchi au ya kiserikali kwny nyumba za ibada au kwny mahafali..
masuala yakiserikali hayapaswi kusemwa kwa kuchomekwa-chomekwa
 
Uhuru wa TANGANYIKA DEC 9 ,1961
Na ule wa Zanzibae Dec. 10, 1963.
Mama Akitowa Hotuba Dec 8 atakuwa ameunganisha sherehe za uhuru wa nchi zote mbili ambazo awali zilikusudia kuunda Muungano wa Afrika.
Kwa vile hakuna nchi hata moja iliyokuwa tayari kuungana kwa muundo huu wa muungano wetu wa kuburuzana, tumeendelea kubaki Zanzibar na Tanganyika tuu kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hukukukiwa na Kero za Muungano lukuki na Muungano ukilindwa kwa nguvu za Kijeshi kwa maslahi ya Tanganyika.
Natarajia leo Mama taweza kufungua baadhi ya vizuizi na kuondoa kero zilizokwisha kubuhu za Muungano ili kuipa zanzibar nafuu ya Kiuchumi. Uchumi wa BLUU hauwezekani bila ya Zanzibar yenye mamlaka kamili ya kiuchumi.
 
Waandishi habari watakuwepo kuuliza maswali kama kwa Biden?
 
Hayupo kwenye TV kila siku, ni matukio anayohudhuria ndiyo yanamfanya awe kwenye TV kila Siku, And ukiacha TBC ambao ya Taifa, TVs nyingine pamoja na social medias wanarusha matukio yake bila kulipwa chochote, sababu zipo 3;1. Kuna ambao ni wazalendo wa nchi 2. Kuna wengine wanatafuta viewers and 3. Wengine wanajipendekeza kwa chama na serikali ili kakitokea kafursa wasiachwe!! MwanahalisiTV (Unawafahamu msimamo wao) kutwa kuchwa wanamfuata Rais anapokuwa kwenye matukio na kuyarusha live kwenye social medias zao, hao tafuta kundi la kuwaweka Bwana Tindo

Haijalishi anaonyeshwa na vyombo vyenye nia gani, lakini sisi wananchi huwa tunamuona kila mara, na hata yeye anapohutubua anajua tunasikiliza. Sasa kwa mtiririko wa hotuba zake zote, sioni akiwa na jipya zaidi ya cheap publicity.
 
Hata wakiwepo ni wa kupangwa. Tabia ya viongozi wetu ndio hiyo imehamishwa kwenye elimu yetu ya maswali ya multiple choice. Na yote hii imetokana na ccm kupoteza ushawishi kwa umma.
hi habari watakuwepo kuuliza maswali kama kwa Biden?
 
Hiyo public attention, hana kipya zaidi ya blah blah za siku zote, watu walishamchoka na yeye keshagundua hilo sasa, hivyo ni mwendo wa kutafuta kick.

Poor Samia!
 
Nafikiri arejee na huu utaratibu wa kuongea na taifa walau mara moja kwa mwezi aya mambo ya kuwa unaenda adi kufungua vyuo una ruka live hayafai
 
Back
Top Bottom