Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na Wahariri leo 28.6.2021

Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na Wahariri leo 28.6.2021

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
11,936
Reaction score
15,196
Wajumbe.

Rais Samia Suluhu anazungumzia na wahariri leo mnamo saa 9 alasiri. Tukio hilo linafuatia Rais kumaliza siku 100 akiwa madarakani.

JamiiForums kama mdau mkuu wa habari humu nchini tupendekeze hapa maswali ambayo tungependa wahariri kamuulize mama . Japo siyo hayo lakini yenye mlengo huo

1. Rais uliahidi kukutana na wapinzani, Je ni lini hasa wananchi watarajie mkutano huu?

2. Wewe ulikuwa makamu mwenyekiti wa BMK Mchakato huo haujafikia mwisho bado. Je unawaahidi nini wa watanzania ili mchakato huo uwezo kukamilika na kuwapatia wananchi katiba mpya?

Ongeza mengine

Karibu.
 
Habari mbaya sana kwa MATAGA.

Mama anaupiga mwingi mnoo akina na polepole na kakurwa wanateseka sana awamu hii.
FB_IMG_1624729470604.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mbona tunaishi Kwa kukariri? Yeye amekuwepo madarakani siku zote hizo,hizo Siku 100 Ni zipi? Kuna uhusiano gani kati ya Siku 100 na kuonekana kuwa atafaulu au hatafaulu katika Uongozi wake?

Kuna uhusiano gani kati ya Siku 100 na kuonekana kuwa anayo maono?Badala ya kuchapa Kazi yeye yuko busy na Siku 100! Maisha Yale Yale ya kukosa ubunifu au kutojitofautisha na wengine. Nani alisema kuwa lazima ueleze Yale uliyoyafanya kila Siku 100 zinapotimia ukiwa madarakani?
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta
Lisu alikuwa anampeleka gereji magufuli mara kwa mara wakati wa kameni. Na baada ya uchaguzi hali haijawahi kuwa nzuri kwa magufuli hadi umauti kumkuta
 
Swali hili pia ni muhimu, angeulizwa kuwa Kuna taarifa kuwa alitaka kujiuzulu kipindi cha uongozi wa Hayati JPM kutokana na katiba Mbovu na madaraka kuwa chini ya mtu mmoja, Je anafikiria lini ataleta mchakato wa katiba mpya.
 
Tutawapima wahariri kwa maswali yao maana tulipiga kelele sana juu ya waandishi wa habari makajanja / uchwara waliokuwa mara nyingi wanatumwa na wahariri wao ktk kushughuli muhimu kama hii ya leo kisha waandishi habari hao ama wakaondoka bila kuulizwa maswali au wakauliza maswali yasiyo na manufaa.



 
Hivi mbona tunaishi Kwa kukariri? Yeye amekuwepo madarakani siku zote hizo,hizo Siku 100 Ni zipi? Kuna uhusiano gani kati ya Siku 100 na kuonekana kuwa atafaulu au hatafaulu katika Uongozi wake? Kuna uhusiano gani kati ya Siku 100 na kuonekana kuwa anayo maono?Badala ya kuchapa Kazi yeye yuko busy na Siku 100! Maisha Yale Yale ya kukosa ubunifu au kutojitofautisha na wengine. Nani alisema kuwa lazima ueleze Yale uliyoyafanya kila Siku 100 zinapotimia ukiwa madarakani?
Acha makasiriko, siku 100 ni kipimo cha dunia nzima kupima uelekeo wa utawala mpya.
 
Back
Top Bottom