Rais Samia Suluhu Hassan, Mwanademokrasia bora

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imekuwa mstari wa mbele kutekeleza kwa vitendo dhana halisi ya demokrasia hususan katika tafsiri ya demokrasia kuwa ni nguzo ya kisiasa inayoendesha serikali ya kidemokrasia.

Amekuwa kiongozi msikivu aliyekuja na mbinu mbadala ya kuwaweka watu pamoja na kuzungumzia maendeleo na amejitanabainisha ni muumini wa 4R ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya kiingereza.

Maneno hayo ni Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya), ambapo alisema yeye sio muumini wa tamhilia maarufu ya karne ya 19 ya lolanthe.

Tangu alipoingia madarakani ameweza kuwaweka pamoja wanasiasa wote na kufanya siasa kwa ustaarabu na uvumilivu na kama kuna vitendo vya ukiukwaji wa taratibu vinatoka kwao wenye na si serikalini.

Nchi inapumua na kila mmoja yuko huru kufanya siasa zake kwa sababu serikali imejielekeza katika kusaka maendeleo ya nchi na sio 'ku-deal' na kundi au makundi ya wanasiasa.

Kelele za uminywaji wa demokrasia zimepungua,w atu kukamatwa bila utaratibu au kuminywa uhuru wa kuzungumza nao hakuna tena. Rais Samia Suluhu anaisha katika demokrasia na kutekeleza kwa vitendo maono ya mwanazuoni Abraham Lincoln.

FZu1coQXkAIDcXu.jpg
 
Ila hela hatuna mifukoni wanazo viongozi wetu peke yao.
 
ok 👍

ila:

awamu ni ya 5 kipindi cha uongozi ni cha pili, rais tofauti...

yeye ni rais mlezi na kila kukicha ananionyesha kuwa yeye ni mlezi!

kiongozi zile siku 180 ndio zinanionyesha ni mtu wa aina gani. kwangu simdharau na simpambi nitabaki kumpa heshima ya mlezi wa kiti cha rais, mlezi wa katiba sema kazungukwa na watu wenye wazuri na wabaya na wote wana uzoefu sana katika hayo mazuri na mabaya!

Mungu amtangulie na amlinde katika shughuli zake!
 
Raisi wetu mpendwa tuondolee Tozo za Mwigulu.
 
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imekuwa mstari wa mbele kutekeleza kwa vitendo dhana halisi ya demokrasia hususan katika tafsiri ya demokrasia kuwa ni nguzo ya kisiasa inayoendesha serikali ya kidemokrasia.

Amekuwa kiongozi msikivu aliyekuja na mbinu mbadala ya kuwaweka watu pamoja na kuzungumzia maendeleo na amejitanabainisha ni muumini wa 4R ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya kiingereza.

Maneno hayo ni Reconciliation (Maridhiano), Resiliency (Ustahamilivu), Reforms (Mabadiliko) na Rebuilding (Kujenga Upya),
Naunga mkono hoja.
P
 
ok 👍

ila:

awamu ni ya 5 kipindi cha uongozi ni cha pili, rais tofauti...

yeye ni rais mlezi na kila kukicha ananionyesha kuwa yeye ni mlezi!

kiongozi zile siku 180 ndio zinanionyesha ni mtu wa aina gani. kwangu simdharau na simpambi nitabaki kumpa heshima ya mlezi wa kiti cha rais, mlezi wa katiba sema kazungukwa na watu wenye wazuri na wabaya na wote wana uzoefu sana katika hayo mazuri na mabaya!

Mungu amtangulie na amlinde katika shughuli zake!
Ndugu , tupo awamu ya 6.
 
Ati Rashda Zunde😆😆😂🤣 hii Id huwa inanifanya nicheke sana.
 
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,
Hapana, hii ni serikali ya awamu ya 5 na kama hata hilo halikuingii kichwani, hoja yoyote inayohusu demokrasia inakuzidi kimo.
imekuwa mstari wa mbele kutekeleza kwa vitendo dhana halisi ya demokrasia
Kama vile nilijua tu...hujui demokrasia ni nini wala umbo lake na hata kama ungekutana nayo uso kwa uso huna uwezo, sifa wala akili ya kuitambua
hususan katika tafsiri ya demokrasia kuwa ni nguzo ya kisiasa inayoendesha serikali ya kidemokrasia.
Rais Samia aliapa kuliheshimu, kuilinda na kuitetea Katiba ila kwa kuiogopa demokrasia, alichofanya ni kuisigina Katiba ili kuminya demokrasia.

SSH anaingia katika historia ya taifa hili kama Rais asiyejua jukumu lake kuhusu mfumo wetu wa demokrasia kama ulivyooainishwa kwenye Katiba.

Na kweli hajui ingawa anajitahidi kujiaminisha kuwa anajua na kwa namna hiyo haitatokea ajue kama ataendelea kupuuza ushauri wa wanaojua.
 
Rais Samia Suluhu huwa anasema "Tanzania ni yetu sote kwaiyo tuungane tujenge Tanzania moja" ndio maana amefanikiwa kurejesha democrasia nchini
 
Back
Top Bottom