Watanzania leo kuanzia saa kumi jioni wanatarajia kupata hotuba ya kwanza ya serikali ya awamu sita itakayosomwa Bungeni, kupitia hotuba hii watanzania wanataraji kusikia marekebisho mengi ya uzandiki yaliyokuwa yanafanywa na awamu ya tano, baadhi ya uzandiki huo ni juu ya miashahara ya watumishi wa umma, ukandamizaji wa haki za binadamu, kubambikiana kesi zisizo na ukweli, mabadiliko ya sheria kandamizi kama vile sheria ya habari na mawasiliano, utekaji wa watu unaofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama,
Hotuba hii tunataraji pia itafungua milango ya ajira, kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma, hotuba itasema juu makosa ya kubambikiana na kufungiana biashara kwa kuongezeana kodi za uongo, kufungua akaunti za watu zilizofungwa bila ushahidi kwa kifupi wizi wa serikali.
Hii ni serikali tukufu sio kama ile ya awamu ya tano, yakina Sabaya na Sukuma Genge.
Mungu Ibariki Tanzania , Mungu Mbariki Rais wetu Mama Yetu.