Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

Rais Samia Suluhu: Kusanyeni kodi kwa kutumia akili, sio nguvu

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,284
Reaction score
38,364
Mheshimiwa Rais Mama Samia amemuonya Waziri wa wizara ya Fedha kuacha kutumia nguvu kwenye kukusanya kodi badala yake watumie akili.

Mama Samia ameonya tabia ya Watendaji wa Serikali kutumia nguvu kukusanya kodi, kufungia biashara zao, kunyang'anya fedha kwenye akaunti kisa Sheria inawaruhusu.

Ameongeza kuwa Kitendo hicho kinasababisha wafanyabiashara kufunga biashara zao na kukimbilia nchi Jirani na hatimaye Serikali kukosa mapato.

Mama amenikosha sana.

Kumbe walikuwa wanatumia mabavu hadi kukwapua hela za watu kwenye account zao za benki.

Kama analoongea ndo alilokusudia kulisimamia basi sekta hii ya biashara na uwekezaji itaanza kustawi tena.
 
bora kasema maana huyo waziri wa feza anaweza kuagiza wafanyabiashara wanaodaiwa kodi wamwagiwe tindikali.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] daaaah
 
Mheshimiwa Raisi Mama Samia amemuonya Waziri wa wizara ya Fedha kuacha kutumia nguvu kwenye kukusanya kodi badala yake watumie akili.
Sisi wananchi wenyewe kulipa kodi bila kusukumwa ni mtihani!! Ukisema leo waje kwa kulemba kwenye kodi aaah hawapati ata bilion 1 kwa mwezi. Wakwepa kodi wengi wanajua kama wanakwepa kodi na wanafanya hivo ili faida ipige maradufu.
 
Kweli...

Ndio maana TRA wakiwa around na center flani..kila mtu Nduki.

Kuna mambo ukibembeleza bembeleza hayaendi kamwe!
 
Mama amenikosha sana.

Kumbe walikuwa wanatumia mabavu hadi kukwapua hela za watu kwenye account zao za benki.

Kama analoongea ndo alilokusudia kulisimamia basi sekta hii ya biashara na uwekezaji itaanza kustawi tena.
Benki zimekwapuliwa sana pesa za watu kwa nguvu Kama jambazi tu nchi ilikuwa kwenye mpasuko mkubwa sana hii
 
Sijawahi kupata amani hata moja nikiwa naenda kufanyiwa makadirio yangu au kupeleka hesabu zangu za mwaka TRA ,

Ni kama hawakosi kitu cha kukutuhumu na mbaya sasa watu wengine tunajitahidi kufata sana sheria na kulipa inavyo takiwa shida ni hizo ‘penalty’ zao kama mara hauja file makadirio mara sijui ‘withholding tax’ imefanyaje yaani wanajikuta wanaishi na kukamua watu kwa hizo ‘penalty’ zao ambazo hata elimu ya kodi hawajaitoa vya kutosha kwa walipa kodi ni kama wanakutegea ukwame ili wakukamue kwa maslahi yao na wakiona una msimamo wanajifanya kusimamia sheria ( ambayo hata hawajatoa elimu ya kutosha) ili kukukomoa tu
 
Back
Top Bottom