Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Huo ni upendeleo itabidi azunguke nchi nzima azungumze na wazee
 
Mama Samia ni Vyema sasa akaanza miradi yenye kuwagusa wananchi wa chini na kati Madaraja ni Miradi ya serikali zaidi.

Bima ya Afya kwa Wazee ianze mara moja bila kuchelewa.
Wazee wenye Umri zaidi ya miaka 70 wapewe bima za gharama nafuu zaidi ili wapatiwe matibabu yao bila kubaguliwa.

Ujenzi wa Nyumba za gharama Nafuu kwa watu wa chini kupitia NHC na Suma JKT.
Nyumna ni zile zile za mkoloni NHC wanachukua tu kodi kwa wahindi bila kujenga mpya .

National Housingi limekua ni shirika la kuwanufaisha matajiri wa kihindi peke yao huku wananchi wanaoitwa wanyonge wakiendelea kupanga kwenye makazi yasiyo na mipango bora kwa gharama kubwa.

Jiji jipya kama Dodoma limeanza vibaya kwa kuwaacha mabeberu na wezi kujitwalia viwanja ili wajenge majumba ya kuwanyonya watu wa chini kwa kuwapangishia kwa kodi kubwa badala ya Shirika la nyumba kujenga nyumba kwa kuzingatia vipato vya watu wa chini ili jiji lisiwe linakua kiholela.
Jiji jipya na miji yote sasa pawe na mkakati wa kujenaga makazi bora kupigia NHC ili watu wa vipato vya chini wazidi kufurahia utawala wa Mama Samia. Ujenzi holela mara nyingi unafanywa na watu wa vipato vya chini.

Nyumba zijengwe na NHC kwa ajili ya watu wa chini kulipa kodi nafuu kama wanavyofaidi wahindi na wakubwa wengine.
 
Kweli MSOGA style...

Kwaiyo tuamini ndio remote control holder?
hata nyerere alikua na utaratibu wa kuongea na wazee wa Dar.. kama unafuatilia hotuba zake alishawahi kusema aliwa kuchinjiwa mnyama kuambiwa atambuke damu. hii ilikua kama tambiko kwa kijana wao wakati huo alikua na majukumu mazito ya kuirudisha tanzania kutoka kwa mkoloni.
sio nyrere tu, mkapa alikua na utaratibu wa kuongea nao,mwiny hadi kikwete.
mwendazake tu ndio aliwazalau na kukumbatia wa chato kwao.na mbaya zaidi kahama bila ya kuwaaga'hivi hajajiuliza kwanini nyerere aliwaheshimu wazee wa pwani kuliko kwao ingawa alikua mtoto wa kichifu.
kuongea na wazee wa dar si kama unavyofikili tu mkuu.
 
Wazee ni HAZINA ya Taifa letu.

Wazee ni DAWA.

PALIPO NA WAZEE HALIHARIBIKI JAMBO.
 
Hv mzee Makamba yy haingii vikao kama hv!? Au yy ni mkubwa kuliko hv vikao!?
 
Mama Samia usiache kuhoji Lisu na Lema wanarudi lini Tanzania.

Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake...
Nasema hakuna namna lazima Lissu kuna kitu alikufanyia tu, sasa utake usitake lazima nikamshitaki Lissu ili ulipwe fidia yako, mkuu umeteseka sana juu ya Mwanaume huyo, inatosha sasa lazima haki yako ipatikane. Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…