Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Baada ya kuongea nao mheshimiwa rais atawaandalia futari wazee wa dar es salaam.
Kisha watapatiwa usafiri wa kurudi makwao
Wazee wa dares salaam Wana hesvima Yao,hata nyerere.mwinyu,mkapa wote walikua wanatambua.
Wewe unaehoji kwa Nini wasiongee na wazee wa chato, sijui,dodoma au Tanga kawaulize mkapa na jk ni kwa Nini wazee wa DSM tu.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takriban 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, Tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.”

"Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima," amesema.

Hiyo ndiyo akili sasa siyo yule Mwendazake alikuwa anaongea na Makonda na wachawi wa Gamboshi na Sheikh Zuberi Mufti
 
Wazee wajikite kwenye stahiki na maslahi yao, waombe waongezwe pensheni kiduchu wanazolipwa, pia bima za afya na uboreshwaji wa 'matibabu bure' kwa wazee.

Wasipoitumia fursa hiyo vizuri wakabaki tu kusifia watawala na kunywa kahawa na soda, imekula kwao.
 
Mama Samia ni Vyema sasa akaanza miradi yenye kuwagusa wananchi wa chini na kati Madaraja ni Miradi ya serikali zaidi.

Bima ya Afya kwa Wazee ianze mara moja bila kuchelewa.
Wazee wenye Umri zaidi ya miaka 70 wapewe bima za gharama nafuu zaidi ili wapatiwe matibabu yao bila kubaguliwa.

Ujenzi wa Nyumba za gharama Nafuu kwa watu wa chini kupitia NHC na Suma JKT.
Nyumna ni zile zile za mkoloni NHC wanachukua tu kodi kwa wahindi bila kujenga mpya .

National Housingi limekua ni shirika la kuwanufaisha matajiri wa kihindi peke yao huku wananchi wanaoitwa wanyonge wakiendelea kupanga kwenye makazi yasiyo na mipango bora kwa gharama kubwa.

Jiji jipya kama Dodoma limeanza vibaya kwa kuwaacha mabeberu na wezi kujitwalia viwanja ili wajenge majumba ya kuwanyonya watu wa chini kwa kuwapangishia kwa kodi kubwa badala ya Shirika la nyumba kujenga nyumba kwa kuzingatia vipato vya watu wa chini ili jiji lisiwe linakua kiholela.
Jiji jipya na miji yote sasa pawe na mkakati wa kujenaga makazi bora kupigia NHC ili watu wa vipato vya chini wazidi kufurahia utawala wa Mama Samia. Ujenzi holela mara nyingi unafanywa na watu wa vipato vya chini.

Nyumba zijengwe na NHC kwa ajili ya watu wa chini kulipa kodi nafuu kama wanavyofaidi wahindi na wakubwa wengine.
Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake
 
Yetu macho na masikio.
Maana jana wakati anatoka Kenya alisema ngoja arudi DODOMA akahangaike na bunge gear changed tena kwa wazee
 
Hao huwa wazee ccm ....wanakula 40 each usafiri bure jioni futari bureeee....acha mama afungue nchi
 
hata nyerere alikua na utaratibu wa kuongea na wazee wa Dar.. kama unafuatilia hotuba zake alishawahi kusema aliwa kuchinjiwa mnyama kuambiwa atambuke damu. hii ilikua kama tambiko kwa kijana wao wakati huo alikua na majukumu mazito ya kuirudisha tanzania kutoka kwa mkoloni...
Kwaiyo wazee wa Dar ndio ma genius?
 
Mama Samia usiache kuhoji Lisu na Lema wanarudi lini Tanzania.

Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake...
Kwani Lissu na Lema ni wazee?
 
Ningefurahi hawa wazee nao wakapewa nafasi hata ya muda mfupi na wao wakatoa mchango wao kuhusu wanavyoona/wanavyopenda mwelekeo wa nchi yetu utakavyokuwa. Lisiwe jambo la kwenda kumsikiliza tu aliyewakaribisha, bila ya wao kuchangia chochote.

Hawa wazee walishaona mengi, mazuri na mabaya. Uzoefu wao huo unaweza kuwa na manufaa kwa kumtahadharisha anakokimbilia bi mkubwa bila ya kuchukua tahadhari kubwa.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takriban 900...
Anaongea saa ngapi?
 
Mama Samia usiache kuhoji Lisu na Lema wanarudi lini Tanzania.

Walituaminisha wamekimbia nchi na kwenda kulelewa na wanaume wa kizungu kama wakimbizi kwa sababu hapa nchini walikuwa wanatishiwa maisha na mwendazake...
Kuna suala la kashfa ya wabunge wa Covid 19
 
Rais kaitisha mkutano wa wazee Dar ambao kimantiki nikama njia ya kuzungumza na Watanzania wote ilikuwapa ujumbe Rais aliokusudia.

Tumeona siku zote CCM jinsi inavyokuwa na kiherehere katika mambo ya kitaifa kwa kujimilikisha kuwa ni yao.

Kwa hali ilivyo sasa, hasa kwa machungu ya nchi yaliyopo ambayo bila kuficha ni kuwa yamesababishwa na mwendazake inapaswa kutenganisha sana shughuli za Rais na mambo ya chama ili kumpa hadhi kuwa ni Rais wa Tanzania.

Ila kuna jambo la kujiuliza kwa kina sana.

Rais makao yake yako Dodoma, inakuwaje maongezi yake ayafanye na wazee wa Dar? Au wa Dodoma hawana hekima kama alivyo Ndugai?
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takriban 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, Tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.”

"Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima," amesema.

Bado hamjatoa MAELEKEZO YA KUJIKINGA NA COVID-19.
Mnataka kuwafanya kafara hao wazee?
 
Leo Rais wa JMT mh Samia Suluhu Hassan atazungumza na Wazee wa Dar es salaam.

Mzee Mtulia ambaye ni mjumbe wa kamati ya Wazee amesema ilikuwa wao ndio wamualike Rais lakini yeye amewawahi hivyo wana furaha na matumaini makubwa sana na hotuba ya leo.

Mzee Mtulia anaamini hotuba ya leo ndio itakayoifungua Tanzania.

Runinga mbalimbali duniani zitarusha mubashara tukio hili wakiongozwa na ITV, Channek ten na TBC.

Ramadhan kareem!

Kazi Iendelee!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam katika UKUMBI wa mlimani city kuanzia saa 8:00 mchana anatarajia kukutana na wazee wawakilishi zaidi ya 900.

Matarajio makubwa kwa wazee hao kuwa Rais anakwenda kuangalia namna Bora ya kutatua Changamoto mbalimbali za wazee nchini ikiwemo maswala ya Matibabu bure kwa wazee, kuboresha nyumba za kuelekea wazee pamoja na maswala ya mafao ya uzeeni.

Pia kuliombea taifa amani na utulivu wakati wote.

IMG-20210507-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom