Rais Samia Suluhu kuzungumza na Wazee wa Dar es Salaam Ijumaa Mei 7, 2021

Mama waongezee wazee Penseni na Bima ya Afya ya ukweli.
Ni kweli. Kama mishahara imeshindikana basi walao hao wazee wachache waliobaki na wanapokea pension kupitia hazina awaongezee kiwango maana ni aibu kuwa pamoja na kujitolea kizalendo wanachopewa sasa hivi ni pension kichekesho
 
Saa ngapi itakuwa
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es salaam katika UKUMBI wa mlimani city kuanzia saa 8:00 mchana anatarajia kukutana na wazee wawakilishi zaidi ya 900.

Matarajio makubwa kwa wazee hao kuwa Rais anakwenda kuangalia namna Bora ya kutatua Changamoto mbalimbali za wazee nchini ikiwemo maswala ya Matibabu bure kwa wazee, kuboresha nyumba za kuelekea wazee pamoja na maswala ya mafao ya uzeeni.

Pia kuliombea taifa amani na utulivu wakati wote.

View attachment 1776089
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takriban 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, Tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.”

"Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima," amesema.

Itakuwa ni saa ngapi ?
 
Wakuu hapa sijaelewa vizuri kwa vile tumeambiwa jiji la Dar ni ILALA tu, na leo Mh Rais Samia anakutana na Wazee ila sijajua kama ni wa makoa wa Dar au jiji la Dar, mwenye kujua atujuze
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 7, 2021 anatarajia kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika mkutano utakaofanyika ukumbi wa Mlimani City na kuhusisha wazee takriban 900.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 6, 2021 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge aliyebainisha kuwa kulikuwa na utaratibu maalum wa kuwapata wazee hao na kwamba wengine wanapaswa kufuatilia mkutano huo kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

"Tunaomba sana waliopata mwaliko wahudhurie mkutano huu, Tunatarajia ikifika saa nane kamili wazee wote watakuwa wameshafika. Na utaratibu wa jinsi ya kufika utatolewa kwani kutakuwa na magari yameandaliwa.”

"Tunamshukuru Rais kwa kuchagua Mkoa huu kwa sababu angeenda Mkoa wowote lakini amechagua Dar es Salaam. Ninaamini kuongea na wazee hao atakuwa ameongea na wazee wa Tanzania nzima," amesema.

Saa ngapi
 
Baada ya kuongea nao mheshimiwa rais atawaandalia futari wazee wa dar es salaam.
Kisha watapatiwa usafiri wa kurudi makwao
Wazee wa dares salaam Wana hesvima Yao,hata nyerere.mwinyu,mkapa wote walikua wanatambua.
Wewe unaehoji kwa Nini wasiongee na wazee wa chato, sijui,dodoma au Tanga kawaulize mkapa na jk ni kwa Nini wazee wa DSM tu.
Wazee wale waliokuwa na heshima zao wote wameshafariki waliobaki kidogo corona ikamalizia hawa waliobaki wahuni wajana ila leo wamezeeka tu lakini sio original. wazee original wameisha.
 
Tumefuka ukumbini toka saa saba na nusu mpaka muda huu hakuna lolote linaendelea.

Mpaka muda huu mama hajafika ukumbini na hakuna taarifa yoyote ile. Mwisho wa siku tumeanza kuongelea Dabi ya kesho tu. Wahusika kama mpo humu nawaambie hamtutendei haki kabisa
 
Kwani nawe ni miongoni mwa wazee wadar.
 
Tumefuka ukumbini toka saa saba na nusu mpaka muda huu hakuna lolote linaendelea.

Mpaka muda huu mama hajafika ukumbini na hakuna taarifa yoyote ile. Mwisho wa siku tumeanza kuongelea Dabi ya kesho tu. Wahusika kama mpo humu nawaambie hamtutendei haki kabisa
Umekaa Kona ipi mzee mwenzangu?
 
Back
Top Bottom