Rais Samia Suluhu piga chini daraja la Kigongo - Busisi haijalishi lilipofikia

Rais Samia Suluhu piga chini daraja la Kigongo - Busisi haijalishi lilipofikia

Tuliowahi kupata adha ya kuvuka pale wakati mwingine hadi saa sita usiku mko Busisi Ferry imeloga, tunaona umuhimu wa hilo daraja
Achana na hawa pinga pinga, huo mradi uko ndani ya ilani ya chama cha Mapinduzi. Kutokamilika kwa hili daraja maana yake Ccm itakuwa imeshindwa kutimiza ahadi yake halafu 2025 mje hapa kulalamika.
 
Halina Tija kwa Taifa, limejengwa kwa utashi wa MTU binafsi.Kuna miradi mingi ambayo Mh.Rais wa JMT Madame President SSH na viongozi wenzake lazima waifanyie mapitio kama inafaa kweli kuendelea?Fikiria Chato Stadium, Airport, Referral Hospital,Kigongo Busisi Bridge,Salender Bridge etc.
Nchi hii ni yetu sote,tunapoijenga tuweke vipaumbele.Tukamilishe JKN Hydro Electric Dam na sgr ili tuweze Ku recover tulichowekeza.Tuhakikishe chuma na Coal vinachimbwa tujenge sgr kuunganisha mikoa yote mpaka Zanzibar kwa treni na kuzalisha gas na kuisambaza majumbani kama nishati mbadàla.Miradi kama hiyo hata ikikopewa fedha ni sawa,lakini daraja la Kigongo Busisi?
Hiyo ni roho ya kichwawi.. Huduma ya mwendokasi inamsaidia nini mwananchi wa busisi, ubungo interchange je,daraja la kigamboni je!?

Hiyo miradi mingine nakubaliana nawe, ila daraja la busisi lina umuhimu kule, kawaulize wakazi wa kule watakueleza.
 
Daraja la Kigogo Busisi ni halina maana yoyote ile. Matumizi mabovu mno ya fedha ambayo yangeelekezwa pengine.

Nakusihi Rais Samia Suluhu. Piga chini huu mzigo. Hakuna fedha zinazotolewa kama takrima. Eti kisa sijui kina fulani wanatokea hapo ndiyo iwe kigezo. Piga chini mama.

Lingine kwenye taasisi karibu zote za umma angalia sana viongozi wake. Kuna kigezo kimetumika kuwaweka pale. Kwa sasa nikupe muda ufanye kazi huku nikikuangalia kwa umakini mkubwa.
Yeah wakurugenzi wengi wa mashirika ya umma waliwekwa kindugu mfano ni wale pale waliovunjiwa ubungo sijui
 
Ukisoma mawazo ya wafuasi wa CHADEMA ktk matukio kama haya ndio utaelewa kwa nini ruzuku zote hutafunwa kwa amani. Nadhani mfumo umetuokoa kutawaliwa na mbumbumbu wa nchi hii. Ni vizuri vyama vya maana vianze na kuachana na wapuuzi hawa.
Ivi wanachama wa chadema kwanini huwa hawahoji ruzuku inafanya kazi gani paka wanachangishwa michango eti kiongozi yuko ndani wanaanza kuchangshwa?
 
Hilo jambo halipo leo wala halipo kesho wala keshokutwa, lakini pia hongera kwa kutoa ushauri amabao chimbuko lake ni chuki binafisi.
 
Halina Tija kwa Taifa, limejengwa kwa utashi wa MTU binafsi.Kuna miradi mingi ambayo Mh.Rais wa JMT Madame President SSH na viongozi wenzake lazima waifanyie mapitio kama inafaa kweli kuendelea?Fikiria Chato Stadium, Airport, Referral Hospital,Kigongo Busisi Bridge,Salender Bridge etc.
Nchi hii ni yetu sote,tunapoijenga tuweke vipaumbele.Tukamilishe JKN Hydro Electric Dam na sgr ili tuweze Ku recover tulichowekeza.Tuhakikishe chuma na Coal vinachimbwa tujenge sgr kuunganisha mikoa yote mpaka Zanzibar kwa treni na kuzalisha gas na kuisambaza majumbani kama nishati mbadàla.Miradi kama hiyo hata ikikopewa fedha ni sawa,lakini daraja la Kigongo Busisi?
Yawezekana hili daraja lina umuhimu kiuchumi lakini namna ambavyo Magufuli alianza kujenga ilikaa kiukabila na kikanda ndiyo maana wachangiaji wengi wanalipiga vita.

Ninachokiona Ni kwamba Magufuli hakuwa na busara kwenye priorities. Pengine alipaswa kujenga daraja la Busisi kwanza kabla ya Chato Airport, Regional referral Hospital na hayo mavitu mengine aliyoyajaza Chato.

Kama ukiangalia takwimu za uchumi utaona kuwa Magufuli alikuta deni la Serikali ni Tsh 35 Trillion, lakini mpaka anakufa deni limefika Tsh 60 Trillion kwa miaka 5 sawa na ongezeko la Tsh 5 Trillion kwa mwaka. Na matumizi makubwa ya mkopo ni miradi mikubwa aliyo ianzisha kwa mkupuo.

Rais SSH hata naamini ili aende vizuri kwenye Utawala wake lazima apunguze kukopa na aweke vipaumbele. Inabidi atekeleze miradi kadri ya Ilani ya CCM na approval ya Bunge, la sivyo atakwama.

Hata angekuwa naye ni mkazi wa Chato kama akitaka kutenda haki, katika miradi ya KUSITISHA/ KUIAHIRISHA mitatu ya kwanza ni (1) Kuacha kununua Ma Dreamliners na pengine kukodisha au kuuza yale tuliyonayo (2) Kuachana na STIGLERS Gorge Electricity Project hata kama imefika 70% (3) Kuachana na Daraja la Busisi hadi hali ya fedha itakapokuwa njema

Naunga mkono hoja kwa G Sam
 
Perhaps my death won't lead some people to celebrate. I am trying not to wrong anyone on Earth. So that after I perish, I wont leave grudges behind.

you are a human, you make mistakes! the fact that your alive just know everyone has different view on you, Jesus himself did no wrong but still he went on massive hate, till today religions are still battling whether he will come again and take his people or when ua die thats when ua gone! and he is God remember that, imagine your own sistuation
 
Daraja la Kigogo Busisi ni halina maana yoyote ile. Matumizi mabovu mno ya fedha ambayo yangeelekezwa pengine.

Nakusihi Rais Samia Suluhu. Piga chini huu mzigo. Hakuna fedha zinazotolewa kama takrima. Eti kisa sijui kina fulani wanatokea hapo ndiyo iwe kigezo. Piga chini mama.

Lingine kwenye taasisi karibu zote za umma angalia sana viongozi wake. Kuna kigezo kimetumika kuwaweka pale. Kwa sasa nikupe muda ufanye kazi huku nikikuangalia kwa umakini mkubwa.
Uko vizuri,
Yafuatayo lazima yatekebishwe;
1. STIGLERS Gorge ni kuachhana nayo mara moja. Hatuwezi kupata Megawati 2100 pale hata tukimaliza kujenga. Umeme utegemeao mvua umepitwa na wakati. Tujitahidi kuwalipa Wakandarasi kwa like walichokifanya. Tunaweza kupata umeme wa gesi Megawati nyingi kuliko hizo kwa uwekezaji mdogo tu.

2. Ondoa Serikali Dodoma, Rudisha Dar es Salaam. Ule mji wa Serikali wa Mtimba ni matumizi mabaya ya fedha za umma. Quality ya nyumba HOVYO, barabara vumbi tupu. Chamwino ibaki Kama Ikulu ndogo. Waziri Mkuu, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Serikali za Mitaa zinaweza zikabaki

3. Kwenye SGR tuendelee lakini tukifika Nzega tueelwkee Mwanza ili tu Target mzigo wa Uganda unaokuja kwa Meli. Uganda Wana metric tons zaidi ya 3 Million za mizigo kwa Mwanza dhidi ya 800,000 za Rwanda

4. Uza Dreamliners zote baki na Airbus na Bombardie. Tujielekeze na usafiri wa ndani ya nchi na wa East and Central Africa

5. Daraja la Coco-Agha Khan limaliziwe

6. Daraja la Busisi kule Mwanza ni la kuachana nalo. Kivuko kinatosha

Miradi ya Magufuli ukiiendekeza utaishia kutolipa wafanyazi mishahara, kupandisha kodi za TRA, kuwanyanga'anya matajiri na wafanya biashara hela zao kwenye mabenki.

Tufanye tunayoyaweza kwa wakati, mengine watafanya wengine. Kwa kutaka kufanya yote ndiyo maana AMEKUFA

Daraja hilo ni muhimu sana aisee,
Mtatumia kivuko kinachotumika sasa. Kuna mambo muhimu mengi ya kufanya. Kwa mfano wafanyakazi wa Tanzania hawaja pewa increments zao. It was STUPID kwa Magufuli kusema eti siwaongezi mshahara najenga miundo mbinu.
 
Pu.mbavu kweli wewe!!!

Daraja linajengwa na huyafanya kitu!!!

Lbd daraja la Wami Ruvu ndio litasubiri, mtazunguka Dodoma kwenda DSM
 
Pu.mbavu kweli wewe!!!

Daraja linajengwa na huyafanya kitu!!!

Lbd daraja la Wami Ruvu ndio litasubiri, mtazunguka Dodoma kwenda DSM
Wacha matusi hata Kama wewe ni la 7. Kuwa mpole Msukuma, iko siku nitakurudisha kusoma hapa tena.
 
Daraja la Kigogo Busisi ni halina maana yoyote ile. Matumizi mabovu mno ya fedha ambayo yangeelekezwa pengine.

Nakusihi Rais Samia Suluhu. Piga chini huu mzigo. Hakuna fedha zinazotolewa kama takrima. Eti kisa sijui kina fulani wanatokea hapo ndiyo iwe kigezo. Piga chini mama.

Lingine kwenye taasisi karibu zote za umma angalia sana viongozi wake. Kuna kigezo kimetumika kuwaweka pale. Kwa sasa nikupe muda ufanye kazi huku nikikuangalia kwa umakini mkubwa.
Wewe jamaa punguza chuki na wivu dhidi ya wananchi wa kanda ya ziwa na kama hujui umuhimu wa hilo daraja basi tuulize, ni bora lidaraja la kigamboni libomolewe kwani sioni umuhimu wake zaidi ya kuunganisha mji na kijiji.
 
Back
Top Bottom