Rais Samia Suluhu piga chini daraja la Kigongo - Busisi haijalishi lilipofikia

Labda ungesema lile la salender linalopita baharini hapo ningekuelewa
 
Rais Samia ni JPM version two, sidhani kama anaweza kuwaza huu upuuzi ulioandika. Au umesahau, ukishachukua jembe kulima ni marufuku kugeuka nyuma?.
 
Kwa hiyo wanaopita pale ni wakwe wa Magufuli tu? Unajua ni watanzania wangapi watakao tumia daraja hilo?

Hii chuki inatoka wapi jamani?
Kuna watu wanachuki mpaka shetani anawashangaa. Mbowe & Co siku mkipata ikulu, watanzania wataomboleza.
 
Kama kun mradi mama SAMIA nakuomba anza nao ni huuu
 
Kwa kodi gani iliyotolewa mpaka mkajengewe hilo daraja
Mkuu kodi inayo zalishwa Geita hujui? Kama mkoa unapata zaidi ya billion 9 kwa mwaka je serikali kuu inapata ngapi kutoka GGM? Bado wachimbaji wadogo.
 
Unapoteza muda wako bure! Daraja hilo lazima likamilike pia miradi yote iliyoanzishwa na Jemedari Magufuli lazima itakamilika kama ilivyopangwa!
Miradi yote iliyoanzishwa na Jemadari ilipangwa ikamilike 2015 - 2020 mwenyewe akiwepo lakini hata robo haikukamilika, yetu macho ikamilishwe na mtu mwingine Jemadari akiwa amepumzika mita 2 chini ya Ardhi. Wishful thinking of a fool!
 
CHADEMA kutoka kuwa chama cha siasa hadi kuwa chama cha watu wenye roho mbaya wasiopenda maendeleo ya watanzania
 
Kwahiyo halipunguzi muda unaopotezwa na kivuko, halirahisishi chochote.. Ama ndio mnataka kumfukia marehemu na mambo yake!?
Mkuu, halina faida yeyote, unajenga mavitu ya hovyohovyo eti tu uwafurahishe wapiga kura wako,
Kuna maeneo mengi ya nchi hii hakuna barabara za maana, tunapaswa kuanzia hapo,
Hakuna hospitali vituo vya afya, tuanzie hapo,
Hospitali hazina madawa, vifaa tiba, tuanzie hapo,
hilo lidaraja ni anasa katika maisha ya mafukara, ukiweka madawa hospitalini utaokoa maisha ya maskini
 
Kwa hiyo wanaopita pale ni wakwe wa Magufuli tu? Unajua ni watanzania wangapi watakao tumia daraja hilo?

Hii chuki inatoka wapi jamani?
Hilo daraja ni mradi wa kijinga, sisi ndio tunaishi huku, tunayo mahitaji mengi zaidi ya hili lidaraja
 
Namnukuu hayati Dkt. John Magufuli "Nataka huu mradi wa daraja la Kigongo- Busisi ukamilike haraka kabla sijaondoka madarakani maana Rais ajaye anaweza asiendelee na mradi huu" Mwisho wa kunukuu.

Mheshimiwa Rais, ule mradi unagharimu kiasi cha Tshs. Bilioni 710. Ni nyingi sana kwa mradi kama ule. Mbaya zaidi ule mradi una lengo la ziada la kuwepo kwake.

Tafadhali naomba fanyia kazi huu ufisadi ili Mayanga na wenzake wawajibike. Ni heri nusu shari kuliko shari kamili.

Narudia tena. Bilioni 710 Tshs haziwezi kuelezeka kwa mradi kama ule!
 
Mtoa post karusha vitu, watu mnafanya attack ya mtu na si wazo. Kazungumzia mambo 2.
Daraja- lina tija kwa taifa.
Taasis- Ni kweli ziangaliwe kwa macho mawili mawili.
 
Pumbavu sana ww hata cjasoma upupu wako au kwa sababu ww hujui adha tunayo ipata huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…