Rais Samia Suluhu piga chini daraja la Kigongo - Busisi haijalishi lilipofikia

Hujui hata mradi ni wa kiasi gani unadanganya wajinga wenzako tuu... Mara nyingine ni busara kukaa kimya budah
 
Fika Kigongo-Busisi kwanza kakaae kama siku tatu uje uikane post yako.
Daraja lile uunganisha TZA na Uganda, Rwanda na Burundi. Itaeupusha mambo ya kukaa foleni kusubiria pantoni.
 
Daraja la Busisi ni muhimu sana ila la salenda ni White Elephant Project kwakuwa lishaanza no way inabidi limaliziwe tu maana kuliachia kati kati pia ni hasara.
Kuacha miradi ambayo ishakula pesaa zote ni hasara zaidi. Bora iendelee hata kwa awamu
 
Kamati ya fedha na mipango ya bunge ilipitisha... sheria mpya ya manunuzi ya serikali ya mwaka ...... kifungu ...... a na b na c

Fanya homework
Sawa mkuu. Pole sana kwa msiba mzito wa mpendwa Rais wetu.

Nakusihi usibadili ID ukajiita "Thesamialianz"....
Natumaini hii ID yako ya sasa haitapotea hapa jukwani ili tuzidi kuchagizana na kuleta malumbano yenye afya kwa nchi yetu.
 
Daraja lina umuhimu sana kwa wenyeji wa hapo maana wanatumia muda mwingi sana kuvuka hapo huo mradi ni wa muhimu sana kuliko daraja ambalo linajengwa hapo Dar karibu na Selender bridge
Huwezi jua umuhimu wa salenda bridge Hadi litakapokamilika, wakati mwingine tulimchukia bure mzee wetu ila ukikaa chini ukatafakari unauona ukweli
 
HAPANA. Mimi critic Mkubwa wa sera na uongozi wa jamaa huyu akiwa Rais...

Lakini miongoni mwa miradi inayotakiwa kuendelezwa mmojawapo ni huo ujenzi wa daraja la Busisi kuunganisha mikoa ya Geita & Kagera...

Projects zingine za kuendelezwa ni ujenzi wa reli ya SGR na Bwawa la umeme la Stigler Gorges...

Za kurekebishwa ni mradi wa ndege za shirika la ndege la taifa - ATCL. Waachwe wajiendeshe wenyewe kibiashara na washindane na mashirika mengine. Amelifufua, basi, inatosha. Serikali iache kabisa utaratibu wa kuwa ina dump pesa hapo badala ya wao ATCL kuzalisha pesa kwa biashara yao na kulipa kodi serikalini...
 

Rais akifanya tu utakavyo nitamdharau.
 
Hili daraja ni muhimu sana, daraja lisilo muhimu ni lile la kupita baharini Salenda
 
Mkuu baada ya kuangalia ile siku wanatoka Sengerema kwenda Chato kisha wakavuka kwa kivuko..naona kabisa Daraja lile lina maana.

Bora wasijenge Salenda bridge ila Busisi liendelee
 

Daraja wamalizie

Ila issue ya Chato kuwa mkoa haina tija na Rais Kajibu vema
 
Huu ni ujinga wa hali ya juu. Daraja lilijengwa kwa ajili ya watanzania na nchi jirani na siyo upogo na upotoshaji kuwa ni zawadi kwa wakwe. Haya ni mawazo mfu na hayasaidii. Wasipolimaliza watamalizwa kwenye uchaguzi ujao.
 
Tusipende kuangalia watu kulingana na sehemu walipotokea ila tuangalie ufanisi wao kwenye viti walivyokalia.

Vinginevyo na wewe ni Kaburu tu kama wale makaburi wa Afrika ya kusini.
 
Nadhani kabla ya kupendekeza kusitishwa kwa mradi wa daraja la Kigogo- Busisi, itakuwa vizuri madam akianza na mradi wa Tanzanite bridge. Sioni faida yake na linatumia pesa nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…