Kauli ya Rais Samia kuminya uhuru wa Raia na vyama vyao vya siasa kwa kutozingatia katiba na sheria ameingia kwenye rekodi mpya kama Rais Mwanamke wa kwanza Africa kuwa Dikteta
Siku ya 101 madarakani, Rais Samia Suluhu tayari ameanza kulewa sifa na mapambio. Ameamua kuendelea kuminya uhuru wa vyama vya siasa kufanya mihadhara kwa kutumia utashi wake na siyo katiba iliyomfanya Yeye awe Rais bila kupigwa kura za wananchi
Hakuna uchumi bila haki na uhuru wa watu, Tangu tupate uhuru kwa miaka zaidi ya ishirini na nne ya chama kimoja hakuna Uchumi wowote uliosimama, Uchumi ulianza kusimama wakati wa vyama vingi vya kisiasa na huu ni wakati wa Hayati Ben Mkapa, Hayati Ben Mkapa alisimamia uhuru na kujenga mfumo wa kitaasisi
Mama Samia ameanza kuonyesha sura yake halisi ya udikiteta mapema sana, Atambue na akumbuke hakuna aliyempigia kura kwenye sanduku kama Rais wa nchi bali amepata Urais kwa kufuata katiba ya nchi, Wananchi wa Tanzania ni waelewa ndio maana Mama alipoapishwa kwa kufuata katiba hakuna aliyelalamika kwenye mitandao ya kijamii, Kuanza kuvunja katiba siku ya 101 kisa umesifiwa sana Jiandae kisaikolojia kwa watu kukusema kimataifa kama mtangulizi wako na kitakachofuatwa ni wewe kuhojiwa maswali Magumu na vyombo vya kimataifa ukajikuta unadhalilika na kutafuta mchawi nani
Chuki ambayo umejenga kwa kauli yako ya kusema hakuna vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara umeitoa kwa kutumia sheria na katiba ipi? Wewe uliapishwa kwa kufuata katiba kwanini umeanza kuharibu na kupindisha katiba ya nchi?
Kauli yako ya kuminya uhuru wa siasa imekuharibia kila kitu na sasa mjadala umeanza kuwa mkali zaidi, Jiandae Kwa watu kukusema hovyo na kukudhalilisha zaidi ya mtangulizi wako
Kila kauli ina madhara yake, Kauli yako ya kuwa unajenga Uchumi, Hayati Magufuli alisema analeta Maendeleo. Leo hakuna anayemkumbuka Magufuli na habari zake za Maendeleo bali anakumbukwa kwa kuminya na kukandamiza haki za Raia
Serikali iwape watu uhuru wao, Kuna tetesi zilizagaa kuwa hata wewe watu walitaka usipewe Urais kwani waliona hutaweza lakini kuna kundi likasimamia katiba na ukaapishwa kuwa Rais, Kwanini wewe unavunja katiba?