Rais Samia Suluhu umeanza kuwa Dikteta mapema kuliko hayati John Pombe Magufuli

Hapana kwa maswali yote mawili, uhuru unaozungumzwa ni ule wa kumuonyesha mama kuwa hapa umependeza au hapa nywele hazijakaa sawa- rekebisha. vyama vya upinzani ni kioo kinachoongea, usikiogope eti kwa kuwa kitasema hapa hapako sawa

Amesema mumkosoe ila sio kwa matusi
Sasa chadema kukosoa mtu bila kumtukana au bila kugoma hamuwezi

Mwambien hii bajet mbovu na nyie mtoe bajet mbadala,

Sio mambo ya kila siku kuita watu tu
 
Kweli wewe ni Ukwaju...sijui kama hata unajitambua! Huu uongo wako unakusaidia nini? Hivi unajua hii ni JF? Unapata wapi ujasiri wa kuandika huu upumbavu ndani ya JF? If only idiocy was painful...

NB: Halafu waone hawa wajinga wenzanko waliokupa like...
Reactions: Petition, Beef lasagna, mwakiri and 15 others



 
Amesema mumkosoe ila sio kwa matusi
Sasa chadema kukosoa mtu bila kumtukana au bila kugoma hamuwezi

Mwambien hii bajet mbovu na nyie mtoe bajet mbadala,

Sio mambo ya kila siku kuita watu tu

..chama kisichotendewa haki au kinachoonewa hakiweza kuwa na lugha nzuri dhidi ya watesi wake.

..lugha mbaya na kutukanana ni kwasababu kuna upande mmoja unaonea upande mwingine.

..tukitaka siasa zetu ziwe za kistaarabu na lugha safi basi ni lazima tuweke sheria na taratibu zinazotoa haki sawa kwa vyama vyote vya siasa.

..kuhusu wapinzani kukosoa bajeti hilo lilikuwa linafanyika wakati wa bunge, lakini spika na ofisi yake walikuwa wanazuia bajeti mbadala za kambi ya upinzani kuwasilishwa.
 
Mkuu,

Yamekuwa hayo tena? Ebo!!!
 
Bado nina imani na mama! Pengine kapotoka kidogo lakini hajaharibu kabisa. Tumpe muda zaidi naye ni binadamu si mkamilifu. KUKOSEA KUPO!

Ninakubaliana nawe. Katika uzi huu:


ninakazia
 

Kudai na kuipata katiba inataka strategies zaidi ya zile za chess au draft.


Uvumilivu, ukomavu, malengo na mwelekeo wa kuchukua ni muhimu sana.

Simba mwenda kimya ndiye mla nyama. Na hapa ndipo bwana Aikaeli anapo wa outsmart wengi.
 

Kama mama samia unamsingizia ni dikteta, je watangulizi wake! Nyerere na Magu tusemeje yani!!! Au ulikua haujazaliwa!
 
Kapotoka kidgo, kwani haijui katiba?

Mama kama binadamu hapaswi kuwa na maoni na hata kuyashirikisha?

 

Kwanini tusiache kuwa manabii. Tukaiweka kwenye majaribio. Kuwa kuna hoja 2:

1. Katiba si kipaumbele
2. Katiba ni kipaumbele

Tukabiliane na mama kwa hoja badala ya kumhukumu moja kwa moja?

Way forward itokane na kushawishiana kwa hoja.
 
Wataalamu wa nguvu za giza wanakuambia bora ukutane na mchawi wa kiume kuliko wa kike!!!!!
 
Nimeamini hata ufanye nini hapa duniani huwezi pendwa na kila mtu
Na wale unaodhani unawapenda ndiyo wa kwanza kukuvunja moyo...Mama acha kutishwa Katiba inakupa haki ya kuamua wewe kama Rais pasipo mashinikizo...

Rais hajakataza mikutano kakataza vurugu za siass kuanza kusema eti kakataa mikutano ni kumlisha maneno na kutaka kumshinikiza kwa mambo ambayo wala si ya watanzania bali kundi la watu wa jamhuri ya twiter ambao hata 5% hawafikia....
 
Wengi wanaotushajiisha katiba mpya, mikutano ya hadhara lengo ni ikulu wala siyo maslahi ya wananchi...

kila mtu, taasisi, au nchi ina vipaumbele.... unavyong'ang'ania katiba mpya iwe agenda ya kwanza kuna madaraja, ajira mpya, miundombinu ya afya, elimu, maji inatakiwa kuimarishwa ni sawa? tukumbuke juzi 2019 serikali za mitaa, 2020 uchaguzi mkuu, 2022 sensa, 2024 serikali za mitaa na 2025 uchaguzi...

hebu tumpe mama muda aweke mambo sawa
 
Mmmh
 
hebu tumpe mama muda aweke mambo sawa
Mama aliapa kuihifadhi, kuilinda na kuitetea Katiba, mbona mapema sana anaisigina?
Kama ameshindwa hata kuheshimu kiapo chake, je tutegemee nini mbele ya safari?
Kama madaraka yake yanatokana na Katiba, kauli yake mbona inapingana na Katiba?
Kama kuminya uhuru ni kuchochea uchumi, dhana ya kupigania uhuru ni dhana potofu?
Kama Katiba hii ya sasa inamkwamisha, kuna ugumu gani kuifanyia ukarabati kwanza?
Kama msingi wa nyumba una nyufa, kwa nini kipaumbele kiwe ni kupaka rangi ukuta?
Hapana,
Tuache utani jamani, mama kapotea stepu na tukinyamaza hata mawe yatapaza sauti!
Mdharau mwiba mguu huota tende...leo ni kauli, lakini tusije tukasahau kauli huumba!
Mwendazake alianza hivi hivi kwa kauli lakini yaliyojiri tusiombee yatokee tena asilani!
Aliyeumwa na nyoka akiona ung’ong’o hushtuka!
 
Bado nina imani na mama! Pengine kapotoka kidogo lakini hajaharibu kabisa. Tumpe muda zaidi naye ni binadamu si mkamilifu. KUKOSEA KUPO!
Mi nahisi kuna watu anawaogopa ndani ya chama chake.
Lakini hatakiwi kuogopa kwani hata mtangulizi wake hakuwa na uoga wakati wa kuharibu. Sembuse yeye anajenga, asiogope, wananchi tupo nyuma yake,, lakini kama kaamua kuponya aponye kweli aache uoga.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…