Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

Unaharibu kila kitu, unapo tuletea Polepole kwenye mada za maana!
hapana, Samia anajua kiingereza, sio kama wengine wale. anakifahamu na alishafanya kazi katika organisation ya kimataifa. sawa tu na polepole, hajaishi ulaya ila ile kufanya kazi na wazungu kwenye maNGO anao uwezo mkubwa sana kujieleza kwa kiingereza. so is Samia.
 
Ningeshangaa sana kama Uzi huu usingevamiwa na wasiokijua ' Kiingereza ' na najua mtajitokeza wengi tu.

Ninachojua tu ni kwamba duniani kuna Lugha nyingi na nzuri ila hakuna ambayo hadi hivi leo imeweza kuwa ni Kiungo ' Kikuu ' cha Mataifa yote duniani iwe Kiuchumi na hata Kidiplomasia kama cha Kiingereza.

Kama Mchina, Mrusi, Mjerumani na Mchina pamoja na Jeuri zao zote za kuwa ' Super Powers ' ulimwenguni na Lugha zao pia ni Kubwa lakini bado hao hao wanakizungumza Kiingereza Wewe Mpuuzi Mmoja wa Kiswahili usiye na mbele wala nyuma ni nani ukipinge?

Itatuchukua muda mrefu sana na huenda pia hata isitokee kwa Mataifa mengi duniani Kuachana na Lugha ya Kiingereza kwani kama kuna Mafanikio makubwa ambayo nchi ya Uingereza ilipata tokea Kipindi cha ' Colonialism ' ni kuhakikisha Lugha yao si tu inaendelea kutumika bali pia inapendwa na kuendelea Kuaminiwa na Vizazi na Vizazi.

Kama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere pamoja na kutowakubali Wazungu ( hasa kwa Sera zao na Matendo yao kwa Waafrika ) lakini Mwenyewe kwa Mdomo wake ( na Clips zipo Mitandaoni ) alikiri kuwa Kiingereza ni Lugha muhimu, siyo ya Kuepukwa duniani na ya Kibiashara zaidi.
wewe binafsi kiingereza kimekusaidia nini katika maisha yako
 
Tunaacha kutumia Kiswahili tunashangilia lugha ya wakoloni.
Swala siyo kuwa tumeacha kuongea Kiswahili. Swala ni kuwa unashindwa vipi kuongea Kiingereza, lugha uliyojifunza toka darasa la tatu, na lugha uliyofanyia taaluma toka sekondari hadi digrii ya juu kabisa ya uzamivu?
 
Wewe Generalist ni mshamba na muathirika wa neo colonialism, unaona kuongea kiingereza ni dili, kwani ngeli na kizaramu zina tofauti gani? Zote si lugha tu tunajifunza?
Mbona hao wengine hawakuweza kujifunza? Kiongozi mkubwa asiyeweza kujieleza mbele ya wezake kwa lugha aliyoanza kuitumia toka Form I lazima kuna tatizo upstairs. Tusifiche ukweli.
 
Back
Top Bottom