Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

Rais Samia Suluhu, Waganda wamekupigia 'Salute' kwa Kiingereza chako kizuri japo huna PhD yoyote

Hayo sikusikia vizuri. Basi atakuwa kakosea sana endapo hata hayo hajui yanatamkwaje. La sivyo bora atumie Kiswahili ikiwa wapo wakalimani wazuri zaidi ya yule wa Dodoma
Wewe umesikia hayo maneno mawili tu??--- basi na wewe una masikio mabovu au matamshi yako ni mabovu katika baadhi ya maneno ya kiingereza.

Mfano neno World alitamka "wold" na neno Worth alitamka "woth", hukusikia??.
 
When mentally enslaved black people judge your efficiency by your ability to speak a foreign language.[emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517][emoji3517]
Hapa ndio nashindwa kuwaelewa wabongo,

hii ni lugha tuu kuiongea au kuindika ni ruksa, lakini,

kujivunia au kum jaji mtu juu ya ufahamu wa kiiingereza chake kuwa kizuri au kibaya ndio sawa na upeo wake wa akili ni vitu viwili tofauti.
 
Si kweli, cut ni kat sehemu zote AmE na BrE. Hayo unayosema hajakosea, kakosea. Hata katika Kiswahili huwezi kudai tafadhali ni sawa na tafazali au thamani sawa na samani. Ni makosa!

Mwalimu mzuri hatetei makosa bali huyasahihisha. Vivyo hivyo kwa mwanafunzi mzuri.
Mkuu matamshi ya kiingereza sio lazima yote yawe universal kwamba neno fulani ni lazima litamkwe namna fulani.

Mfano ni wamarekani na wabritish wanavyotamka baadhi ya maneno na considering wao ndio wenye lugha zao.

Mfano neno Can't utakuta mmarekani anatamka "kent" ila mbritish anatamka kama lilivyoandikwa "kant".
Neno lingine ni Cut vilevile utakuta mmarekani anatamka "Kat" na mbritish anatamka kama lilivyoandikwa "Kut".

Na at the same time wote wapo sahihi huwezi sema wamekosea.

Na hapo kwenye invitation mama samia ametamka invaiteshen sababu kuna I kwenye hilo neno so technically hajakosea.

So mama samia yupo vizuri na sahihi.
 
Alikosea matamshi (pronunciation) siyo lafudhi (accent). Lafudhi inabaki ileile kama ambavyo Mu7 anaongea lafudhi ya Kinyankole katika Kiingereza. Speaking kwa lafudhi ya Kinyankole wanatamka spikingi
Na maneno anayo yatamka ya kiswahili kwa lafudhi ya kizenji uwe unarekebisha mkuu ili tuweze kujifunza kutoka kwako mtaalamu wa lugha
 
Hiyo helufi i inatupaga shida sana kwenye matamshi ya kiingereza . Ili kuwa kuwa kuendana nayo vizuri inabidi upige mazoezi mengi ya kuongea maneno ya kiingereza kwa kurejea kwenye kamsi.

Kuna mengine mengi yanatupaga shida wabongo kama vile ; 1. Build~ inatamkwa bild na sio biulid. 2. Determine ~inatamkwa ditamin, sio ditamain. 3. Passed ~ inatamkwa pasit na sio pasid. 4. Burry ( maana yake ni mazishi) inatamkwa beri na sio bari. To mention few.
R na L pia zinatupa tabu katika matamshi na uandishi, mfano ni mwanzo wa hii reply, pia tufanyie kazi hili.
 
I have a dream, one day people will understand that English is a language and not a measure of intelligent.
Sijui aliye waaminisha ni nani, au ni agenda za wamiliki wa English medium?😂😂

Ndio maaana wakenya wana nufaika zaidi na kiswahili kuliko wa Tz.
 
Katika lugha hizo pronunciation na accent mnazo mjadili mtu ambaye sio ligha yake hazina msingi wowote.

kikubwa lugha imetumika kama chombo cha mawasiliano na ujumbe umefika inatosha.

Nimewahi kuongea na m Scottish kingereza chake kuanzia pronunciation + accent yake nitofauti sanaaa.. na mmarekani niliyeongea naye kutoka Kansas city Missouri.
 
Huyo mama anajua. Aliwahi kuwa mshereheshaji katika semina moja nami nilishiriki zamani wakati nasoma O level Lumumba sec school. Ana accent nzuri. By then she was young and very beautiful. Jicho jichoo
haha we madam, kumbe kaumri kameenda age kidogo eeh..
heshimaaa ✋
 
Wewe umesikia hayo maneno mawili tu??--- basi na wewe una masikio mabovu au matamshi yako ni mabovu katika baadhi ya maneno ya kiingereza.

Mfano neno World alitamka "wold" na neno Worth alitamka "woth", hukusikia??.
Pia alikuwa ma tatizo na neno " reiterate"
Halafu akasema " this my fast (first)visit to Uganda since I was made Head of State.
Lakini hii siyo tatizo. Ni kama Komla Dumo wa BBC Africa.
Mpaka ikitokea mispronunciation inayoleta shaka kama anafahamu màana ya neno.
 
Ubishi siyo kuhusu accent au pronunciation. Ni mashaka tu kwamba Rais ni illiterate na kwamba labda watu walifanyaambo "faster faster" kumuapisha.

Kwa sababu " faster faster" ni maneno ambayo yanasemwa na kondakta illiterate wa dala dala. Kwa nini Mheshimiwa Rais naye aseme,"katika carrier yangu mambo yalikwenda faster faster?"
 
That is nothing but a colonial hangover !

Ningeshangaa sana kama Uzi huu usingevamiwa na wasiokijua ' Kiingereza ' na najua mtajitokeza wengi tu.

Ninachojua tu ni kwamba duniani kuna Lugha nyingi na nzuri ila hakuna ambayo hadi hivi leo imeweza kuwa ni Kiungo ' Kikuu ' cha Mataifa yote duniani iwe Kiuchumi na hata Kidiplomasia kama cha Kiingereza.

Kama Mchina, Mrusi, Mjerumani na Mchina pamoja na Jeuri zao zote za kuwa ' Super Powers ' ulimwenguni na Lugha zao pia ni Kubwa lakini bado hao hao wanakizungumza Kiingereza Wewe Mpuuzi Mmoja wa Kiswahili usiye na mbele wala nyuma ni nani ukipinge?

Itatuchukua muda mrefu sana na huenda pia hata isitokee kwa Mataifa mengi duniani Kuachana na Lugha ya Kiingereza kwani kama kuna Mafanikio makubwa ambayo nchi ya Uingereza ilipata tokea Kipindi cha ' Colonialism ' ni kuhakikisha Lugha yao si tu inaendelea kutumika bali pia inapendwa na kuendelea Kuaminiwa na Vizazi na Vizazi.

Kama Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere pamoja na kutowakubali Wazungu ( hasa kwa Sera zao na Matendo yao kwa Waafrika ) lakini Mwenyewe kwa Mdomo wake ( na Clips zipo Mitandaoni ) alikiri kuwa Kiingereza ni Lugha muhimu, siyo ya Kuepukwa duniani na ya Kibiashara zaidi.
 
Back
Top Bottom