Tunampongeza sana rais wetu na ni jambo zuri sana kuona rais wetu anapata sifa ndani na nje ya nchi.
Niwe mkweli kwamba,watu wengi wanadhani kuongea kiingereza au lugha nyingine ya nchi za ulaya ni usomi ,na asiyejua kuongea lugha hizo si msomi
huu mtizamo sio sahihi,kwa watu ambao wapo karibu na wachina au wakorea hata wajerumani wapo wengi wataalam ila hawajui kiingereza kabisa,nimewasahau warusi na wajapan ambao mpaka wanagundua vitu vingi vya kutisha ila ukiwasemesha kiingereza wanakuangalia kama kituko. Natamani watanzania tuondokane na ushamba huu,tujifunze na upande wa pili wa ulimwengu.