Wanabodi,
Hii ni Nipashe ya Leo
View attachment 2428894
View attachment 2428861
Kwa Maslahi ya Taifa" ya leo inajikita kwenye Ibara ya 18 ya Katiba kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, yetu ya JMT ya mwaka 1977, kuanzia Ibara ya 18 – 24, katiba yetu imetoa haki zifuatazo:
18. Uhuru wa Maoni.
19. Uhuru wa mtu kuamini dini atakayo.
20. Uhuru wa mtu kushirikiana na wengine.
21. Uhuru wa kushiriki shughuli za umma.
22. Haki ya kufanya kazi.
23. Haki ya kupata ujira wa haki.
24. Haki ya kumiliki mali.
Haki hizi sio hisani sio huruma, sio option, kusema zinaweza kutolewa au laa!, haki hizi ni stahili, zinapaswa kutolewa na kuheshimiwe na Watanzania wote ikiwemo serikali na viongozi, na taasisi zote. Kwa leo nitajikita zaidi kwenye Ibara ya 18, inasema
18: Uhuru wa Maoni Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 6"
(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa kutoingiliwa kati mawasiliano yake.
(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala muhimu kwa jamii.
Haki hizi na uhuru huu wa kutoa maoni, unakwenda sambamba na mipaka ya kawaida ya uhuru, yaani hakuna uhuru usio na mipaka, mwisho wa uhuru wako ni pale uhuru wa mtu mwingine unapoishia. Huu uhuru wa kutoa mawazo yako, unapaswa kuheshimiwa na wote, hata kama hukubaliani na mawazo hayo, na wewe pia unapaswa kuheshimu uhuru, maoni na mawazo yaw engine, hata kama hukubaliani nayo
Leo nimejikita kwenye ibara hii, kufuatia juzi kati hapa, kuna mtu ametoa mawazo yake kuhusu jambo fulani, mtu huyo ameshambuliwa kila kona kwa kushukiwa kama mwewe anavyotaka kunyakua kifaranga cha kuku, wengine wakimbeza, wengine wamdhihaki na wengine hata kufikia kiwango cha kumtukana na kumdhalilisha!
Kilichopelekea mtu huyo kushambuliwa, ni kwa sababu tuu amekosoa jambo fulani!. Kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa
Toka enzi za Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete na Rais Magufuli, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki iwe na haki ya kusifu tuu na kupongeza tuu, lakini kukosolewa iwe nongwa, ni kosa, ni dhambi!.
Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia katika mkutano wa 47 wa wanasheria Afrika Mashariki uliofanyika mkoani Arusha, amesema haya kuhusu kushirikisha watu/taasisi ambazo ziko dhidi yake
"Sasa mimi nikijua wewe ni dhidi yangu nitakushirikishaje? Siwezi kukushirikisha, si ndiyo!"
Kukosoa serikali, sio kosa, wala ukosoaji, sio uadui, sio chuki, na sio dhidi ya serikali, ukosoaji wa serikali ni differing opinion ambao pia ni haki na unalindwa na katiba.
Paskali