Hakuna asiyejua kuwa mikutano hii ilipigwa ban kimagumashi na mapolisi kushikilia bango na bado haki hii kikatiba imebamizwa kwa visingizio hivi na vile.
Tunahitaji Rais Samia autangazie umma kuwa haki hii ipo wazi na vyama vifanye mikutano yake kwa raha mustarehe bila ya kubugudhiwa, tupo kwenye nchi huru, muhimu mipaka ya uhuru huo uzingatiwe kwa mujibu wa sheria.
Wananchi wanahitaji mihemko ya wakati ule wa mikutano nchi ilichangamka na wananchi kujiona wapo huru. Wananchi wengi ni wakulima inapokuwepo mikutano ya vyama vya siasa kunakuwepo na kama kasehemu cha kujiliwaza.
Tusikae kwenye nchi huru kama wafiwa mikutano huru ya kisiasa ni tochi kwa serikali iliyopo madarakani. Na bora pia nikiongezea katika kila Mkoa uwepo au iwepo sehemu ya kajiuwanja kadogo hapo paruhusiwe free speech za kisiasa kwa mtu yeyote yule aweze kusema yaliyo rohoni mwake bila ya kuguswa na sheria ya aina yeyote ile, mtu amalize joto lake hapo, ila inakuwa ni sehemu hio tu kama kwa kila mkoa au wilaya, aina hio huwa na kufanyika kwenye sehemu chaguliwa tu na ni tofauti na ile mikutano ya kichama. Nafikiri huko Ulaya zipo sehemu hizo.