Hizi drama za corona zinasisimua na kuchekesha sana.
Miezi michache nyuma, kulizuka wimbi kubwa la vifo vya viongozi wakubwa na watu mashuhuri, tukaambiwa wamekufa kwa corona.
Muendelezo wa vifo ulichachamaa mpaka ukamkumba Rais John Magufuli. Naye "tukaaminishwa" amefariki kwa corona kinyume na taarifa rasmi ya daktari.
Tangu alipofariki Rais Magufuli, hatusikia tena kuhusu vifo vya vigogo wa serikali.
Tukaambiwa corona imeenda likizo (annual leave) na kwamba itarejea kwa makali hapo baadae.
Pamoja na drama zote hizi za kuigiza, sisi wakazi wa Kariakoo siku zote tunasongamana na hakuna hata mmoja aliyeugua japo mafua ya bahati mbaya.
Hata yale mabarakoa sijayaona. Watu wanadunda tu.
Hakuna cha wimbi wala mawimbi. Kila siku watu wapo tu na wanaendelea na maisha yao wakiwa na afya zile zile.
Tukaambiwa linakuja wimbi sijui la pili. Wenyewe wanaita ati "second wave".
Hilo wimbi nalo likaja likatukuta vile vile na likaondoka likatuacha vile vile.
Hivi sasa tunaambiwa kuwa hilo wimbi limekimbilia India. Likipiga "rivasi" linarudi tena Tanganyika likiwa na maguvu mengi.
Bibi samia anatueleza habari za chanjo. Bila shaka ziko mbioni kuja.
Najiuliza, hizo chanjo anamdunga nani?
Sisi wakazi wa Kariakoo na kwingineko, wala hatuna ugonjwa wowote ule.
Tunapoelezwa kuhusu chanjo, tunahamaki!
Wale wajuzi wa corona hebu mtueleze, hizo chanjo mnamdunga nani?
Mnawadunga hawa hawa watu ninawaona wakiwa na afya tele kila siku?
Ama kuna wagonjwa mahali ambao hatujaambiwa kuhusu taarifa zao?