Rais Samia: Tanzania siyo masikini, tumeshindwa tu kutumia rasilimali vizuri

Rais Samia: Tanzania siyo masikini, tumeshindwa tu kutumia rasilimali vizuri

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,


“Umasikini ni tafsiri, mtu anaweza kuja Tanzania akasema Tanzania ni nchi masikini, lakini ni tafsiri, inategemea vigezo gani ametumia. Mimi ukiniambia Tanzania ni nchi masikini ninakukatalia, ninakwambia Tanzania siyo masikini, sisi ni matajiri mno, tuna rasilimali, tuna maji, tuna ardhi nzuri, tuna kila kitu, lakini tuna mapungufu kwenye kuvitumia hivi na kuleta maisha bora kwa kila mtu"- Rais Samia.

Soma Pia: Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali la mwanahabari mwandamizi Absalom Kibanda katika mkutano wake na wahariri pamoja waandishi wa habari, uliofanyika huko nchini Brazil baada ya kushiriki mkutano wa G20.

Swali la mdau: Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
 
Tanzania kuna Umaskini wa Akili nzuri.

"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa Watu weusi kwenye mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu hawana akili nzuri, endapo kama tungewajumuisha basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini Leo hii."

Pieter W. Botha, aliyekuwa Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi.
 
Watu tunashindwa kujilisha mpaka tuombe nje, hatuwezi kulipa mishahara mpaka tukope, huo utajiri wetu upo wapi, Sisi ni maskini wa vipato, ndio maana mkoa wa Dar pekee ndio unatoa asilimia 80 ya pato, kwengine huko, ni shida, kipato cha mbongo kwa siku ni chini ya buku mbili! Hapo kama sio u maskini ni nini? Elimu duni, ajira hakuna, zilizopo, salary 300K!
 
Back
Top Bottom