Rais Samia: Tanzania siyo masikini, tumeshindwa tu kutumia rasilimali vizuri

Wakuu,

“Umasikini ni tafsiri, mtu anaweza kuja Tanzania akasema Tanzania ni nchi masikini, lakini ni tafsiri, inategemea vigezo gani ametumia. Mimi ukiniambia Tanzania ni nchi masikini ninakukatalia, ninakwambia Tanzania siyo masikini, sisi ni matajiri mno, tuna rasilimali, tuna maji, tuna ardhi nzuri, tuna kila kitu, lakini tuna mapungufu kwenye kuvitumia hivi na kuleta maisha bora kwa kila mtu"- Rais Samia.

Soma Pia: Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali la mwanahabari mwandamizi Absalom Kibanda katika mkutano wake na wahariri pamoja waandishi wa habari, uliofanyika huko nchini Brazil baada ya kushiriki mkutano wa G20.

Swali la mdau: Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mwanzoni kabisa mwa utawala wa Kikwete alishiri kwenye mkutano huko Ubelgiji. Katika mkutano ule nafikiri aliulizwa na wandishi wa habari. Nikisema wandishi simanishi hawa Makanjanja na Machawa wa bongo
Jk aliulizwa : kwann Tanzania ni maskini
Jk alijibu : hatamimi/yeye hajui kwann Tanzania ni maskini.
Hao ndiyo ccm na hao ndiyo maraisi wa Tanzania
 
Wakuu,

“Umasikini ni tafsiri, mtu anaweza kuja Tanzania akasema Tanzania ni nchi masikini, lakini ni tafsiri, inategemea vigezo gani ametumia. Mimi ukiniambia Tanzania ni nchi masikini ninakukatalia, ninakwambia Tanzania siyo masikini, sisi ni matajiri mno, tuna rasilimali, tuna maji, tuna ardhi nzuri, tuna kila kitu, lakini tuna mapungufu kwenye kuvitumia hivi na kuleta maisha bora kwa kila mtu"- Rais Samia.

Soma Pia: Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali la mwanahabari mwandamizi Absalom Kibanda katika mkutano wake na wahariri pamoja waandishi wa habari, uliofanyika huko nchini Brazil baada ya kushiriki mkutano wa G20.

Swali la mdau: Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Umesema vyema Rais wangu...You always are very honest, lakini sisi hatujakuzwa kuwa hivyo!
 
Embe moja au Nazi moja kwenye supermarket kule Cologne Ujerumani au London inauzwa dola 50, ni wachache wenyeji wanaweza kulinunua hilo tunda.

Vipi hapa Bongo kwa siku tunakula maembe mangapi au nazi ngapi tunaweza kuzitumia bila hata kuwazia?.

..kwa maoni yangu Raisi Samia alijifanya hamnazo wakati kujibu swali la Absalom Kibamba.

..kama Raisi anaamini kwa dhati kwamba Wahadzabe wana maisha bora kuliko Wazungu / Mabeberu wa G20 basi hakupaswa kuwa Rio De Jeneiro, alipaswa kuwa Dodoma au Singida wanakoishi Wahadzabe.

..kuhusu bei ya maembe, na nazi, ktk maduka ya Mabeberu inabidi kujiuliza kipato cha mwananchi wa kawaida kikoje ktk nchi hizo. Bila shaka bei hizo zinaendana na vipato vyao, hivyo ukubwa na imara wa uchumi wa nchi husika.

..Hata jibu lake kuhusu kujua kusoma na kuandika limeonyesha jinsi Raisi asivyoijua dunia na masuala mbalimbali ya kimataifa.
 
Marekani na Russia mataifa yenye ushawishi wa kila aina, marais wao wanafanya ziara Tanzania wanakaa siku tatu.

Hakuna nchi duniani yenye kuweza kuishi kama kisiwa, binadamu tunategemeana sana.

Rais kaongelea utajiri wa asili aliyoimba Mungu na huo ndio unaomfanya binadamu atoke sehemu moja na kwenda bara jingine.
 
..Raisi amesema Wahadzabe ndio wenye maendeleo na utajiri wa kweli. Kwamba vipimo vya maendeleo vya kimataifa sio sahihi.
 
Umasikini wa akili unasababisha hata ile maliasili iwafaidishe wengine.
Ni afadhali kuwa masikini wa mali kuliko kuwa masikini wa akili.
Tajiri wa akili atapata mali kutoka kwa masikini wa akili.
 
Wakuu,

“Umasikini ni tafsiri, mtu anaweza kuja Tanzania akasema Tanzania ni nchi masikini, lakini ni tafsiri, inategemea vigezo gani ametumia. Mimi ukiniambia Tanzania ni nchi masikini ninakukatalia, ninakwambia Tanzania siyo masikini, sisi ni matajiri mno, tuna rasilimali, tuna maji, tuna ardhi nzuri, tuna kila kitu, lakini tuna mapungufu kwenye kuvitumia hivi na kuleta maisha bora kwa kila mtu"- Rais Samia.

Soma Pia: Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali la mwanahabari mwandamizi Absalom Kibanda katika mkutano wake na wahariri pamoja waandishi wa habari, uliofanyika huko nchini Brazil baada ya kushiriki mkutano wa G20.

Swali la mdau: Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Yaani yeye ndio anatambua kwamba Tanzania sio nchi masikini? Yaani Magufuli alikua na makamu mtu hawako kwenye masafa sawa kwa kiasi kikubwa. Njia ya magufuli ilikua kutumia utajiri wa nchi ili kuiwezesha kufanya watu wake tajiri. Hilo lilihitaji usimamizi makini na ujasiri. Mama yeye kuingia akageuka kukopa na kuombaomba tu kwa benki ya dunia na nchi za magharibi. Benki ya dunia na IMF ni biashara ya nchi za kibeberu. Wanakukopesha kwa miradi wanakuletea au ile wanaona inanufaisha maslahi ya nchi za magharibi. Misaada nayo unapewa kama hongo kwa vigogo serikalini. Ni aina ya misaada inapigwa juju kwa juu. Unaambiwa eti msaada kuimarisha utawala bora au lishe kwa watoto wachanga. Hakuna kitu hapo. Hela zinaishia kununua magari ya mradi na posho kwa wageni kubwa kubwa waliyoleta mradi.
 
Wakuu,

“Umasikini ni tafsiri, mtu anaweza kuja Tanzania akasema Tanzania ni nchi masikini, lakini ni tafsiri, inategemea vigezo gani ametumia. Mimi ukiniambia Tanzania ni nchi masikini ninakukatalia, ninakwambia Tanzania siyo masikini, sisi ni matajiri mno, tuna rasilimali, tuna maji, tuna ardhi nzuri, tuna kila kitu, lakini tuna mapungufu kwenye kuvitumia hivi na kuleta maisha bora kwa kila mtu"- Rais Samia.

Soma Pia: Jinsi Rais Samia alivyouliza maswali magumu kwenye mkutano wa G20

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akijibu swali la mwanahabari mwandamizi Absalom Kibanda katika mkutano wake na wahariri pamoja waandishi wa habari, uliofanyika huko nchini Brazil baada ya kushiriki mkutano wa G20.

Swali la mdau: Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Africa ina viongozi wa hovyo sana, uko na position ya kubadili mambo Tena unalalamika, hatuna viongozi kabisa
 
..Raisi amesema Wahadzabe ndio wenye maendeleo na utajiri wa kweli. Kwamba vipimo vya maendeleo vya kimataifa sio sahihi.
Ule ni mfano tu katika kujenga hoja kwamba vigezo vya utajiri na umaskini hutegemea na taasisi/mtu/nchi au kiongozi fulani kwa mtazamo wake.

Jaribu kuelewa hoja kwa mapana yake usijikite kwenye upande mmoja mdogo wa hoja nzima.
 
..Raisi aliambiwa Tz ni masikini, yeye akajibu kwamba ni tajiri kwasababu ya rasilimali.

..Raisi akaenda mbali na kutoa mfano wa Wahadzabe kwamba sio masikini, na vigezo vinavyowaweka ktk kundi la masikini sio sahihi.

..Wakati huohuo Raisi haishi kama Wahadzabe, bali maisha yake yanalandana na haohao anaowasema wana vigezo potofu kuhusu umasikini.

..Wahadzabe hawatumii landruiser V8 au kuwa na misafara yenye gari ya kinyesi, bundiki za rashasha, helikopta ya ulinzi....
 
Nimesoma mpaka comment ya tatu sijaona mkimtaja Magufuli.

Magufuli ndio ilikuwa kauli yake kwamba Watanzania si maskini tumechezewa muda mrefu.

Tusiwe tunamsahau Magufuli kwa mazuri machache yake mana na mama naye ameanza hiyo kauli kwa sababu amegundua kuna mapapa mapigaji yana nguvu naona hata yeye mwenyewe anayaogopa. Hayo mapapa ni mpaka nguvu ya umma ichachamae ndiyo yatashtuka.
Kusema hata kichaa anaweza sema, hata samia na uwezo wake tunaoujua kaweza sema!

Swali ni je baada ya kugundua hayo ndani ya miaka 6 au 7 ya uongozi wake alichukua hatua gani?
 
Back
Top Bottom