Rais Samia: Tanzania siyo masikini, tumeshindwa tu kutumia rasilimali vizuri

Kwa hizi mboga mboga tuwe matajiri..? Siku wakikubali mawazo ya wengine wakalisha wataona namna ya kuinua nchi yetu sote hii
 
Hii nchi ni tajiri lakini utajiri unaporwa na matajiri wa ndani na nje

Matokeo yake tuna matajiri wa kutupwa (filthy rich) na masikini wa kutupwa

Kwa hiyo si suala la tafsiri kama unavyotueleza!

By the way Mheshimiwa snow kwa Kiswahili ni barafu au theluji. Tafadhali jivunie lugha yetu!!
 
Umaskini ni mpana na wenye marefu mengi, njia ya kwanza kabisa kuuondoa umaskini ni mfumo wa elimu , ikwepo sera nzuri ya elimu, halafu hizi propaganda za vyama vya siasa na uzingativu kwenye u serious badala ya burudani na michezo tunaweza kupiga hatua ya kwanza ya njia ya njia ya kuuondoa umaskini.
 
lakini tuna mapungufu kwenye kuvitumia hivi na kuleta maisha bora kwa kila mtu"-

Angesema ukweli tu hapo kuwa akili ndio shida
 
Ccm Shikamoo. Kazi ipo mitano tena
 
Ukiwa na maliasili nyingi lakini kuna umasikini wa akili wa kuitumia hiyo maliasili, wewe bado ni masikini.

Umasikini wa akili ndiyo mkubwa kuliko wote.

Hilo nalo mkaliangalie.
Hili nalo mkalitizame.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…