Rais Samia: Tanzania siyo masikini, tumeshindwa tu kutumia rasilimali vizuri

Watanzania wengi wakiwa wanajisifia utajiri wa nchi yao watataja ardhi, mito, madini, wanyama, watataja kila kitu.

Lakini hawataji akili za watu. Human capital.

Kwa sababu hawathamini akili za watu.

Na huyu rais naye kapita humohumo.
Na hiyo shida inaanzia mfumo wa elimu mpaka huku juu kabisa. Human capital is underrated sana
 
Aliyoyasema yashasemwa, yaani hakuna jipya alilolisema bali ni kusindika tu Yaliyoshasemwa.

'sisi sio masikini' ~
 
Tatizo letu lilianzishwa na Nyerere kukumbatia umasikini
Umasikini ni nini mpaka ukumbatiwe?

Sema Tatizo la umasiki ni la kwako, ni lako.

Si wengine tunatambua mchango wake Mkubwa kwenye bara hili na hata Duniani-Umasikini haukuwepo
 
Nimesoma mpaka comment ya tatu sijaona mkimtaja Magufuli.

Magufuli ndio ilikuwa kauli yake kwamba Watanzania si maskini tumechezewa muda mrefu.

Tusiwe tunamsahau Magufuli kwa mazuri machache yake mana na mama naye ameanza hiyo kauli kwa sababu amegundua kuna mapapa mapigaji yana nguvu naona hata yeye mwenyewe anayaogopa. Hayo mapapa ni mpaka nguvu ya umma ichachamae ndiyo yatashtuka.
 
..Anadai Wahadzabe ni matajiri, kwa sababu wanakula matunda ya mwituni.
Embe moja au Nazi moja kwenye supermarket kule Cologne Ujerumani au London inauzwa dola 50, ni wachache wenyeji wanaweza kulinunua hilo tunda.

Vipi hapa Bongo kwa siku tunakula maembe mangapi au nazi ngapi tunaweza kuzitumia bila hata kuwazia?.
 
Kwahiyo ameji discolify kuwa hawezi kusimamia nchi
 
Watanzania wengi wakiwa wanajisifia utajiri wa nchi yao watataja ardhi, mito, madini, wanyama, watataja kila kitu.

Lakini hawataji akili za watu. Human capital.

Kwa sababu hawathamini akili za watu.

Na huyu rais naye kapita humohumo.
Akili mingi ukizionyesha ni lazima pia ukubaliane na walioshika mpini namna wanavyotaka wao !
Ukionyesha una mawazo tofauti na wao unahesabika sio mwenzao so utashughulikiwa !
Wakikusamehe watakuharibia reputation yako kwa namna watakayoona wao inafaa !
Akili kubwa zitathaminiwa pale tu zitakapokuwa zikiwaimbia mapambio Watakayokuwa wanataka kuyasikia wenyewe na si vinginevyo 😳🙄 !
 
C wawataje , umma uingie mzigoni wanaogopa nini?
 
Mheshimiwa yuko sahihi hapa, hili taifa si masikini hata kidogo. Tatizo letu kubwa ni kuwa na viongozi vilaza haswa marais waliopita ukimuondoa Magufuli tu na Nyerere. Unapokuwa na utawala mbovu katika nchi na kuwa na teuzi za "kipendeleo" bila kujali wasifu ama uwezo wa mtu husika lazima tu utafeli kuongoza nchi. Karibia kila waziri aliyepo madarakani ni mchawi kwa sasa, wanaroga ili wapate teuzi ama wasitumbuliwe waendelee tu kuiba na kuzorotesha maendeleo ya nchi. Wasaidizi wa Mama ukimuondoa Majaliwa, karibia ya wote ni vilaza tu, hawafanyi kazi yoyote, wao kazi kuropoka tu lakini vitendo zero, tufafika kweli jamani?
 
Ipo siku umma utaingia mzigoni na hapatakuwa na kuwatuliza.
 
Tumeshindwa sababu ya uongozi wake mbaya na wa hovyo kabisa
 
Usimtoe huyu huyu ni tatizo kubwa haswa
 
Inatakiwa tukope matrilioni na matrilioni kisha zote tuziingize katika miundombinu ya Kilimo cha umwagiliaji Nchi nzima na Umeme na Usafirishaji na Viwanda. Kwisha habari. !
Ukitaka pesa nyingi ya kuingiza mtaji Kwa wananchi au kujenga bwawa la umemea hupewi mkopo, pesa ya kumaliza sgr yote ukiomba word bank hupewi, wanajua ukipata pesa mingi utajitegemea na hutaenda tena kutembeza bakuli.

Ila ukiomba pesa kujengea vyoo mashuleni unapewa🤔

Wanatumia gharama kubwa kusafiri na mafuta Kisha wanapata mkopo mdogo ambao hautusigezi popote zaidi ya kuzidisha ugumu wa MAISHA kutokana na riba kubwa itokanayo na riba kubwa wanazotuwwkea.

Tunahitaji Magu mwingine, atayetafuta pesa za maendeleo Si za mambo ya ajabu ajabu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…