Rais Samia tembelea Ujenzi wa Nyerere Hydroelectric Dam

Rais Samia tembelea Ujenzi wa Nyerere Hydroelectric Dam

Ila kuna wakati nyie raia mnakuwa nyanokho sana! Umeme mbona UK fresh tu? Wapi huko ambako mnakaa gizani masaa yote?
Wewe mkuu unayetutukana ovyo nikuulize swali dogo tu!

Hivi una upana kiasi gani hadi kuiishi Tanzania nzima kwa wakati mmoja na kuona kama nchi nzima hakuna mahali umeme unakatika?

Au wewe ni house maid wa kigogo ambako hawapewi mgao wa Umeme?
 
Umeongea jambo ambalo wengi hawalijui.

Kigogo14 anaogopwa na mama.

Maana anajua siri zao nyingi tokea uhai wa JPM.

Ndio maana Kigogo14 anakuwa na Over confidence.
 

Attachments

  • 20220324112148.mp4
    1.1 MB
Jamani like limradi ni kubwa sana, na linaendelea vizuri, pale ni full mazege lazima yapewe muda wa kukauka vizuri
 
Inasikitisha sana.Kutokana na hali inayoendelea hapa nchini Ninashauri kiongozi mkuu wa serikali ajiuzulu ili kupisha kiongozi mwingine mwenye uwezo zaidi
 
Mh Rais wa JMT.

Jana wakati ukizindua na kukabidhi nyumba kwa wakazi wa Magomeni Quarters.

Ulikaririwa ukisema kwamba,watu huko mitaani wanaongea kwamba miradi mikubwa ya kimkakati iliyoanzishwa na JPM huenda haitakamilishwa.

Lakini ukautumia mradi ule wa Magomeni Quarters kama uthibitisho wa kauli yako, kwamba miradi yote itatekelezwa na kukamilika kwa sababu ni mojawapo ya ilani ya CCM na serikali yake.

Kisha ukasema "unawasamehe kwa sababu hawajitambuwi"

Sasa swali la wananchi wengi liko kwenye mradi mkubwa wa kimkakati wa ujenzi wa bwawa la umeme wa kutumia nguvu za maji huko mto Rufiji. Nyerere hydroelectric Dam.

Huu mradi ulikuwa umeanza kwa kasi kubwa chini ya serikali ya awamu ya Tano, ambapo wewe ulikuwa makamu wa Rais.

Haukuwa ukipita muda bila kuona kiongozi mwandamizi wa serikali akitembelea site ile ili kujiridhisha kwamba mambo yanakwenda kama yalivyopangwa. Pamoja na kuhimiza bidii ya kazi iendelee.

Ilifikia mahali tena ndani ya bunge, ambapo serikali kupitia waziri uliyemuondoa alitamka bungeni kwamba ujenzi ule ungekamilika kwa tarehe ambayo aliitaja na ilikwishapita.

Lakini tangu ulipoingia madarakani na kufanya mabadiliko ya serikali yako, ambapo umetuwekea waziri Makamba. Umeanza utaratibu wa porojo na ahadi ambazo hazieleweki.

Mara tumemsikia akisema kuhusu kukosekana winchi ya kunyanyulia milango ya maji ya bwawa husika. Akiahidi winchi hiyo kuletwa toka nje.

Baadae wabunge walimbana bungeni ili atowe majibu ya kueleweka lakini akaishia kuwajibu taarabu "kwamba kama shida ni uwaziri wake na urais wako Watasubiri sana"

Baada ya hapo kero ya umeme kukatika imeendelea kwa kasi ile ile ya mwaka 2010 - 2015.

Waziri husika anaendelea na Porojo zake tena kwa kejeli za hapa na pale.

Yeye kwa sasa amegeuka kuwa kama Marketing Minister wa wizara ya Nishati.

Kila uchao yeye ni kusaini mikataba mipya ya mabilioni ya walipa kodi za watanzania. Mikataba ambayo kwa ujumla wake ina utata mtupu, mara Software nk.

Hivi majuzi alikuwa Houston kule Marekani akitafuta soko la gesi yetu ya LPG. (Na huko pia ndio nyumbani kwa Richmond PLY).

Mheshimiwa katika hotuba zako pia hatukusikii ukiongelea lolote kuhusu hizi kero za Umeme.

Sasa basi...tunakuomba utembelee huo mradi ili uweze kusimamia kile ulichokiongea kwa watanzania hiyo jana pale Magomeni.
Rufiji ni karibu sana na Dar es salaam na ni suala la Day trip tu.

Badala ya kumuachia Makamba akitufunga kamba zake kila uchao.

Jambo hilo litawapa ahueni wananchi na kuwaondolea taharuki waliyonayo kuhusu kusuasua kwa mradi huo muhimu kwa uchumi wa Taifa letu.

Kero ya umeme ni kubwa kwa wananchi na inagusa sehemu kubwa ya uchumi wa wapiga kura wako.

Picha za hivi karibuni zilionyesha kama hakuna kikubwa kinachoendelea
[emoji116]
View attachment 2162472View attachment 2162473View attachment 2162474View attachment 2162475View attachment 2162476
Pole mkuu! JNHPP huenda ukakamilika, lakini kwamba huo mradi utakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme nchini hicho ni kitendawili! Tatizo kubwa ni uhaba wa maji kutokana na tabia nchi!
 
Pole mkuu! JNHPP huenda ukakamilika, lakini kwamba huo mradi utakuwa ufumbuzi wa matatizo ya umeme nchini hicho ni kitendawili! Tatizo kubwa ni uhaba wa maji kutokana na tabia nchi!
Piga hesabu za Megawatts 2100 ukiongeza na zilizopo kwa sasa kisha ugawanye kwa mahitaji ya nchi na unaobaki tunauza nje.

Hayo mabadiliko ya tabia nchi ni masuala ya Natural justice na tutakabiliana nayo kwa wakati wake huko mbeleni.

Pia hata maji yakipungua kwa msimu,kitakachopungua sio Megawatts zote 2100 kwa wakati mmoja bali wastani fulani kidogo ambacho hakitaweza kuathiri matumizi ya ndani.

Wataalamu walikwishalitambua hilo kupitia tafiti za kina kabla ya mradi kuanza.
 
Hii gas kwa nn haitumiki Tanzania kwa matumizi ya nyumbani?
 
Kama anapata muda kwenda kufungua maji Chalinze atakosaje muda kwenda kwenye mradi mkubwa tena wa kimkakati kama Ujenzi wa bwawa la umeme lenye kuleta faida kubwa ya Kiuchumi kitaifa.

Hao woote uliowataja ndio hao waleta porojo kama wewe.
Be serious!

commonmwananchi
10101

Hela ipo ya huo mradi? Wakati wa Magufuli kulikuwa na kelele za propaganda kuliko uhalisia wa huo ujenzi. Uongo ulikuwa mwingi na ww na wenzako mkauamini. Sasa hivi kinachoendelea ni ukweli, hivyo kwakuwa ulizoea kuamini uongo, ukweli unapowadia unahisi kuna uzembe.
 
Waziri ni mpigaji na haaminiki kwa wananchi.

Kwani Chalinze kwenye kufungua Maji hatukuwa na waziri wa Maji?

Kule Magomeni Quarter's hatukuwa na waziri wa Ujenzi?

Sasa hivi kwenye uzinduzi wa Tanzanite Bridge,hatuna waziri wa Ujenzi?

Kipi chenye afya kati ya kukagua mradi na maendeleo yake au kuja kuzindua baada ya ujenzi?

commonmwananchi
10101

Ni kiongozi yupi wa ccm unaweza kusimama mbele ya wananchi bila mbeleko ya vyombo vya dola ukasema anaaminika na wananchi?
 
Eti mradi ulikuwa unaenda kwa kasi kubwa! Wewe ni mpumbavu uliyekuwa huna uwezo wa kuchanganua propaganda na uhalisia enzi za jiwe

Fuatilia maelezo ya serikali ya awamu ya 5 juu ya kujaza maji bwawa ni lini, utaona muda waliosema ulipita jiwe akiwa bado hai na hawakusema lolote

Mtu mtafiti kidogo tu atagundua ilikuwa haiwezekani kujenga bwawa lile kwa unadhubuti na umakini kwa muda uliosemwa.

Watanzania tunsojielewa hatutaki kukuru kakara za kijnga, ujenzi hafifu Halafu kesho bwawa libomoke liue Watu kwa mafuriko na matrilioni ya ujenzi yapotee kisa tunataka kuonesha tuna kasi.

Mtu yeyote apite Magufuli hostel UDSM aone zile nyufa kila mahali, kisha apite zile hostel za Nyerere alinganishe.
Tuache ujinga wa kukurupuka
 
Back
Top Bottom