Rais Samia, tengua uteuzi wa Waziri Makamba na Bodi nzima ya TANESCO. Au na wewe una maslahi na kinachoendelea?

Na maji ya kujaza hilo libwawa lao sijui yatatoka wapi na haya mabadiliko ya tabia nchi yasiyotabirika
 

Huwezi kupata majibu tofauti ya tatizo iwapo unatumia njia zile zile kulitatua!!!
 
Na maji ya kujaza hilo libwawa lao sijui yatatoka wapi na haya mabadiliko ya tabia nchi yasiyotabirika
Ndio mpaka Mungu apende.Lazima serikali iwe na umeme wa vyanzo ambavyo havitegemei Hali ya hewa hata pindi Bwawa likikamilika maana itafika mahali nalo litaathirika tuu regardless of how big is the dam..

Hilo Bwawa litakuwa na maana tuu kama kuna mvua kinyume chake ni useless.
 
Mkiambiwa jengeni uchumi na miundombinu imara mnaleta siasa zenu za wizi wa chaguzi na kuteuana, haya miaka zaidi ya sitini ya uhuru bado mnasumbuliwa na matatizo ya maji, umeme, madarasa, zahanati na vituo vya afya hadi mnakopea pesa.....hovyo kabisa.
 
Kwani washamba wako bado wapo madarakani?

Si chama kimerudi kwenye mikono salama?
Baraza la mawaziri la Magufuli bado lipo kwa zaidi 90%.Kwahiyo huwezi kuwaondoa kwenye lawama hizi.
 
Teuzi ya January Makamba imebuma mapema mno, unasubiri mambo yaharibike kwa kiwango gani ndio uchukue hatua?
Hivi jibu la utatuzi wa matatizo haya ni kutengua? Kwani ni lini mlimshauri Makamba J. abadili jambo fulani ili matatizo yaishe akakataa ushauri wenu huo? Kama una ushahidi mliwashuri wateuliwa hawa wabadili mambo ili maboresho yatekelezeke ulete hapa jamvini; kama hauna ushahidi huo, basi wakutenguliwa kwanza kabla ya wateuliwa ni wewe mleta mada!
 
Huu ni mtihani mkubwa kwa Rais Samia S H. Ana uamuzi wakunyoa au kusuka. Atahuzunika sana baada ya uchaguzi wa 2025. Hata kama atapita, lakini ukweli katika masanduku ya kura ataambiwa na wapambe wake. Nia ni kumuonyesha jinsi walivyofanya kazi kubwa kumuokoa japo alikuwa anaanguka. Fadhila zitahitajika.

Huzuni kubwa zitampata Mama Samia.
 
kwa sasa kisingizio kimekua mvua akati tangu mwezi wa 9 alipoteuliwa kila siku umeme ulikatika na alipoulizwa sababu alidai repair, kama tatizo lilikua ukame why hakusema?
 
Hivi kwa plant ya uzalishaji umeme pale Kidatu, unasemaje maji yamepungua wakati mto Ruaha unaingia kila siku?
Watu wasiwe wanafiki. Wawe wawazi kama alivyokuwa JPM. Waseme kwamba wanatengeneza frasturation ya supply ili kutengeneza uhalali wa kuja na maamuzi yao.
 
CCM haijawahi kushindwa
 
Kubebwa tu jina baba yake.
Tuambie hizo wizara alifanya kipi Cha maana?
"Kipi cha maana" unamaanisha nini? Una Mfano wowote kwenye wizara yeyote ambapo kimefanyika "kipi cha maana"? Kabebwe na wewe kama ni rahisi kubebwa
 
kwa sasa kisingizio kimekua mvua akati tangu mwezi wa 9 alipoteuliwa kila siku umeme ulikatika na alipoulizwa sababu alidai repair, kama tatizo lilikua ukame why hakusema?
Repair zimeanza kufanyika alipoingia, hata kwenye taarifa ya TANESCO ya jana wameelezea vituo ambavyo wanarepair ili kuongeza umeme kwenye grid ya taifa, then Ukame umeingilia hapa kati na kulifanya tatizo liwe worse! Inashangaza kidogo kumchukia mtu ambaye hata hamumfahamu zaidi ya kumuona kwenye TV na magazetini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…