MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Kuna ile sheria ya kikokoto kipya kilichoibua vurugu mpaka bosi wa nssf alitenguliwa madaraka
kwa sasa NSSF wamejiamulia wenyewe kutumia hiyo sheria pasipo kauli ya Rais je huu siyo ubabe
Watu wa sekta binafsi wanaumizwa na kikokotoo hicho au mnataka watu waingie barabarani na mapanga
Tumieni utu na kufuata utaaratibu acheni upumbavu kauli ya Rais ni sheria kwa nini hamjamuuliza Raisi aliyepo sasa ili wananchi wamsikie yeye anasemaje?
HAYA YALISEMWA NA HAYATI MAGUFULI
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemaliza mjadala kuhusu ukokotoaji wa mafao uliotokana na kanuni mpya za Sheria ya Hifadhi ya Mifuko ya Jamii ya mwaka 2018, baada ya kuamuru utumike utaratibu wa zamani katika kipindi alichokiita cha mpito hadi mwaka 2023.
Uamuzi huo utawanufaisha watumishi wa umma huku wale wa sekta binafsi walio katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakiendelea kupata asilimia 25 kama ilivyokuwa awali.
Akizungumza jana na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), mifuko ya hifadhi za jamii ya PSSSF na NSSF na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Ikulu Dar es Salaam, Rais Magufuli aliagiza kurejeshwa kwa utaratibu wa zamani wa wastaafu serikalini wa kupewa mafao ya mkupuo ya asilimia 50 badala ya asilimia 25 iliyopendekezwa katika kanuni hizo mpya.
Alisema hatua hiyo haitarajiwi kuyumbisha mifuko hiyo kwa kuwa hadi mwaka 2023, wanachama 58,000 wa mifuko hiyo ndiyo watakaokuwa wamestaafu.
Kabla ya kutoa uamuzi huo uliopokewa kwa shangwe na viongozi wa vyama vya wafanyakazi ambao walisimama na kuimba pamoja na Rais Magufuli wimbo wa mshikamano wa wafanyakazi, mkuu huyo wa nchi alisema, “Kustaafu siyo dhambi, bali ni heshima. Mfanyakazi anayefanya kazi yake hadi anastaafu bila kufukuzwa lazima aheshimike.”
Alitolea mfano wa mwalimu ambaye katika kipindi chake cha utumishi ameshika chaki hadi zikamsababishia madhara mbalimbali lakini inapofika kustaafu anawekewa masharti ya kuchukua fedha zake.
Advertisement
“Umefundisha miaka 40 tena watu mbalimbali wengine ni wakurugenzi wa NSSF na lakini hawa mliowafundisha wanakupangia namna ya kuchukua fedha zako,” alisema.
“Unasema mimi nazihitaji hizi nina wagonjwa wanataka kutibiwa, unaambiwa hapana huwezi ukazichukua zote.”
Alihoji, “Mstaafu anaambiwa fedha nyingine atunziwe ili aendelee kuishi nazo katika kipindi cha maisha yake! Wanaopanga hivyo wamejuaje kama mhusika anataka kuishi wakati fedha zake anaziona zinavyotumika kwenye miradi isiyo na tija?
“Si umpe sasa hivi akafie mbali, mbona wakati anachangaia hukuniambia? Leo nimemaliza unaniambia nikae nitapata polepole. Haiingii akilini kwa mtu yeyote hata kwa hawa waliotayarisha hii.
“Ukweli kabisa lazima tufikirie haya mambo tunayotakiwa kuyafanya ungefanyiwa wewe ingekuaje? Hiki ndicho kitu cha msingi tunachotakiwa kukibeba.”
Alisema jambo hilo halileti maana, ingawa anafahamu lengo mahsusi la wahusika kwamba endapo fedha hizo zikitoka kwa mkupuo, mifuko ya hifadhi itakufa na baadaye haitaweza kujiendesha.
Hata hivyo, Rais Magufuli alisema mifuko hiyo ikibadili mwelekeo na matumizi yake yakawa mazuri itaweza kujiendesha na sanjari na kuwalipa wastaafu.
Bosi SSRA atenguliwa
Saa chache baada ya kutangaza kusimamisha kikokotoo kipya cha pensheni kwa watumishi wa umma, Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jana usiku imeeleza kuwa uteuzi wa mkurugenzi mpya utafanywa baadaye.
Mapema jana, akizungumza na viongozi wa wafanyakazi Ikulu, Rais Magufuli alieleza pamoja na mambo mengine kutorishishwa na jinsi baadhi ya mifuko ya hifadhi ya jamii ilivyokuwa na matumizi mabaya ya fedha za wanachama ikiwamo kuanzisha miradi mikubwa isiyokuwa na tija akitolea mfano ule wa NSSF wa Dege Eco-Village wa Kigamboni aliosema haufai.
“Nafahamu kuna hifadhi ya moja jamii sitaitaja imetumia Sh1.3 bilioni kwa mwaka kwa ajili ya kuchapisha kalenda na matangazo. Nyie wanachama hamuwezi kujua kama fedha zenu zinatumika ovyo. Hifadhi hiyohiyo imeajiri walinzi binafsi wanaowalipa Sh2 bilioni kila mwaka wakati wangeajiri wale Suma JKT wangelipa chini ya Sh1 bilioni kwa mwaka.”
Mbali na hilo, aliitaka hifadhi hiyo kupunguza gharama za uendeshaji wa mifuko kwa kuwa hivi sasa ipo miwili tu hivyo hakuna sababu ya kushindana.
Alitoa maagizo akitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuboresha daftari la wastaafu ili kuondoa wasio na sifa wanaolipwa.
“Nina uhakika kama kumekuwa na watumishi hewa, wanafunzi hewa, pembejeo hewa, mishahara hewa, mbolea hewa... basi hatuwezi kukosa wastaafu hewa. Wenyeviti, watendaji, Regulator (mdhibiti- SSRA) na wizara husika msimamie hili pasiwepo na wastaafu hewa.”
Pia aliitaka mifuko ya hifadhi za jamii kupunguza matumizi ya ovyo, ili fedha za wastaafu zilipwe kwa mkupuo badala ya kuanza kuzungumza masuala ya fomula wakati mifuko yenye ina matumizi mabaya.
Madeni
Rais Magufuli pia alizungumzia suala la madeni akisema awali, Serikali ilikuwa haijachangia fedha katika mifuko hiyo takribani Sh 1.2 trilioni lakini kutokana na kukusanyaji mapato kwa ufanisi, ilianza kuchangia mifuko hiyo na kumaliza madeni hayo Machi mwaka jana