Rais Samia: Tozo zitaendelea kuwepo

Rais Samia: Tozo zitaendelea kuwepo

Wewe upo kisiasa mimi siko huko. Mama kasema ukweli, nchi yetu itajengwa na sisi wenyewe, watoto wetu tumewazaa wenyewe na tutawasomesha sisi wenyewe. Hiyo ya kutegemea mfadhili nao ulikuwa upumbavu tu kama upumbavu mwingine, na pia ni laana kuishi kwa kudra za watu wengine.
Siasa ndio zimetuleta hapa huwezi kuukimbia ukweli. Hata jukwaa hili ni la siasa na ndio maisha yetu . Siasa safi huleta maisha nafuu, siasa mbovu hule TOZO na Dhiki.
TOZO ni UFISADI na Haramu. Wananchi kwa nini waumizwe.
Miaka 60 Nchi inaongozwa na GENGE la CCM ikiwa na Raslimali chungu mzima, ziko wapi, wameiba kina Magufuli raslimali zote.

Sasa tunaumiza wananchi mnawaita wanyonge na mnawataka wawe wazalendo. Huku watawala toka enzi za Mkapa , Kikwete na Magufuli wakifanya wizi wa raslimali. na Samia sasa anaona aumize tu wanyonge.
CCM imepoteza uhalali wa kuongoza Nchi. Anachofanya Samia na WAHUNI wenzie ni UGAIDI.
 
😁😁😁
20210825-161245.jpg
 
Hivyo vituo vinajengwa wap?
Alafu mmekusanya bilion 48 au 60..
 
Siasa ndio zimetuleta hapa huwezi kuukimbia ukweli. Hata jukwaa hili ni la siasa na ndio maisha yetu . Siasa safi huleta maisha nafuu, siasa mbovu hule TOZO na Dhiki.
TOZO ni UFISADI na Haramu. Wananchi kwa nini waumizwe.
Miaka 60 Nchi inaongozwa na GENGE la CCM ikiwa na Raslimali chungu mzima, ziko wapi, wameiba kina Magufuli raslimali zote.

Sasa tunaumiza wananchi mnawaita wanyonge na mnawataka wawe wazalendo. Huku watawala toka enzi za Mkapa , Kikwete na Magufuli wakifanya wizi wa raslimali. na Samia sasa anaona aumize tu wanyonge.
CCM imepoteza uhalali wa kuongoza Nchi. Anachofanya Samia na WAHUNI wenzie ni UGAIDI.
Mnachekeshaga mashabiki wa vyama vya siasa!

Nshakwambia kama mtoto umemzaa mwenyewe msomeshe mwenyewe basi. Huo ndio ukweli haijalishi unapenda au unachukia CCM na magenge mengine yanayojiita vyama vya siasa. Siasa safi ni kusema ukweli na kusimamia ukweli. Ukweli humweka mtu huru.

Sasa wewe unataka kuniambia kwamba tungeogozwa na NCCR ya mrema au CUF ya lipumba enzi za Mkapa ndio maisha yangekuwa safi? Au kwamba Mbowe angeshinda urais ile 2005 ndio maisha yangekuwa bora kuliko Kikwete wa CCM?
 
Eti vituo 20.
Si wauze ndege zilizopo kiwandani wajenge vituo kibao
 
Namwonea huruma Rais Samia. Namwunga mkono katika mengi. Aliponikwaza ni kwenye kesi ya kumbambikia Mbowe. Lakini najua siyo maagizo yake.

Naelewa shida kubwa ya upungufu mkubwa wa fedha aliokutana nao kutokana na sera mbaya za uchumi alizokuwa amezianzisha marehemu.

Rais Samia hana namna, la sivyo mambo mengi yatasimama. Wakati tukiendelea kutozana ili kuokoa jahazi, juhudi kubwa zielekezwe kwenye kubadilisha sera na sheria ili zivutie na kuimarisha uwekezaji.
wakati anatoka madarakani kikwete kulikua na uhaba wa pesa pia je, nae alikua na sera mbaya za kiuchumi?

hili taifa linaumwa kuanzia viongozi hadi wanananchi
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
Swali fikirishi je tozo za simu kitakuwa chanzo cha uhakikka cha ingizo la fedha
 
Hivi anashindwaje kusema kuwa alikuta bwana yule amemaliza pesa kwenye miradi yake isiyopangiliwa
 
Hivi ni kweli kabisa kwamba serikali imeshindwa kabisa kutengeneza vyanzo vya mapato, ila kwa kutumia tozo?! Maana nimemwona Chemba anasema wana mpango wa kuanzisha tozo ya huduma za kimtandao!! Na hizi tozo anaziongelea kama vile wananchi wamezikubali, ila anajua fika huu ni wizi/ujambazi mtupu. Shame on her!
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
i
 
Tunaomba vunja baraza la mawaziri na kumteu waziri mmzoefu wa fedha
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
Punguzo la TOZO linaanza kutumika lini mbona bado hazijapungua??
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"

Super mama. Kazi na iendelee.
 
Kwahiyo hao walio maliza la saba hawakuwa na viti madawati wala madarasa ya kusomea? Tuliwaambieni munapiga vita shule binafsi
 
Hivi hiyo 30% ishaanza kufanya kazi au bado tunaibiwa?
 
wakati anatoka madarakani kikwete kulikua na uhaba wa pesa pia je, nae alikua na sera mbaya za kiuchumi?

hili taifa linaumwa kuanzia viongozi hadi wanananchi
Kikwete alipoingia alikuta hazina ina akiba ya $5 bilioni. Huyu amekuta account ikiwa na zero balalnce.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
Safi Sana napenda Rais mkweli mda wa propaganda wakati pesa inatakiwa ulienda na Mwendazake.

Tozo ziko pale pale na lazima Nchi isonge mbele na kitu kizuri matokeo yanaonekana ila kwa wajinga unaachana nao na kuwapuuza.
 
Back
Top Bottom