Rais Samia: Tozo zitaendelea kuwepo

Rais Samia: Tozo zitaendelea kuwepo

pesa ya tozo ndo hiyo anaitumbua kwenye kupuyanga royal tour
 
Sikatai wanajitahidi ila wapunguze matumizi serikalini pia waangalie mali asili ili kupunguza makali ya maisha.Mfano kama mafuta ya kula kuna nchi zina mafuta ya kula mengi kwa nn wasiagize huko kuliko kucha wananchi tunalia tu mkuu.Mkuu pia nchi haijengwi siku moja sasa hivi kuna cahangamoto ya corona lakini serikali inamiladi mkubwa ambayo inatakiwa hela nyingi ndo maana wanatubana kwa nn wasiangalie ile ya muihimu tu ndo iendelezwe kupunguza makali ya maish.
Ni kweli ila kwenye mafuta ya kula yaliyopanda zaidi ni ya alizeti mengine ya viwandani bei zina nafuu japo zimepanda pia toka mwaka juzi kwa kusukumwa zaidi na aluzeti.

Kujitosheleza mafuta kuongezeka ila sasa hata wazalishaji wa ndani wanaangalia kwenye soko zuri,akina baresa,Azam naona mafuta yao mengi wanapeleka nchi za Sadc sasa huenda huko returns ni kubwa kuliko soko la ndani na huwezi mzuia ni biashara huru na Hawa wanachangia pia upungufu.

Ishu ya miradi mikubwa unfortunately Mwendazake alishaianzisha hawawezi kuitelekeza itakuwa hasara mara mbili,hata hayo mandege yako kwenye plani zao.

Sema hivi serikali iangalie tuu zaidi jinsi ya kurahisisha biashara,kupunguza matumizi yasiyo ya lazima Serikalini kama kuwa na mataasisi meeengi kila mtu anatoza kodi kwenye biashara moja.

Mambo ya rasilimali ndio mpaka upate wawekezaji wa nje au ndani na kuanza kuona matunda yake it takes time.Kwa mfano bomba la EACOP ndio wako hatua za awali wanalipa fidia na kuanza hatua za awali matunda yake ni baada ya 2025.Hivyo hivyo na kwenye migidi mingine ambayo Serikali imetangaza ujenzi utaanza ya dhahabu,rare earth metals, Mchuchuma na Liganga,nickel na Cobalt nk.

Ndio maana Rais alisema hata kama kweli hifadhi kuna mali itafutwe namna ya kuvunwa Ili zitoke zisaidie unafuu sasa hii inahitaji mda.

Na uchumi ulianguka kweli Magu alikimbiza investors serious so naamini baada ya miaka 2 nafuu itapatikana hasa mazao ya kilimo yakirudi kwenye bei zake za awali.Pia nimeona serikali wanamalizia mazungumzo na South Africa Ili parachichi zipate soko kule hasa msimu wa low season maana inatofautiana na kwetu.

Na namna ya mwisho ni mikopo nayo unfortunately tuko uchumi wa kati hakuna kubebwa unapigwa riba za kibiashara na payback period ni fupi hapo ndio hatari sasa thus why unaona wanasema laxima tujichage.
 
Mkuu Popolation growth na public social service ni vitu vinavyotakiwa kukuwa kwa pamoja, ni bahati sana kama unaishi mijini ni ngumu kuona au kusikia kuna baadhi ya shule watoto wanatembea 10km+ kufuata elimu kila siku. Shule nyingine madarasa yanabeba wanafunzi 100+ , ni miaka 60 sasa baada ya uhuru. Kuna wazazi / wagonjwa wanatembea km 15+ kufuta huduma za matibabu, wazazi wanajifungulia njiani, tuacheni kubeza jitihada hizi japo najua matokeo hayawezi kuonekana ndani ya miezi miwili/ mitatu...

Tumekuwa tukilalamika serikali haiajiri, sasa itahajiri vipi wakati haijengi shule mpya, haiongezi madarasa, haiongezi huduma za afya kwa kupanua na kuongeza vituo vya kutolea huduma???? Tujiulize ni lini tutafikia level za darasa moja kuwa na wanafunzi chini ya 40 kama hizi jitihada hazifanyiki.

Najua tozo zinaumiza, ila nikikumbuka nachangia maendeleo ya nchi yangu napata nguvu ya kuendelea kuchangia. Tukumbuke hata misaada tunayopata kutoka nchi marafiki ni kodi / tozo za wananchi wao. Kwa nini tuunung'unike kwa tozo zinazokwenda kuboresha elimu/ afya / maji na barabara za nchini mwetu?
Miaka 60 ya uhuru story ni zile zile? shule, madarasa, vituo vya afya na mara zote zimekuwa ni kampeni za kujenga utafikiri hii nchi imeanza kuwepo leo....kwa hiyo ni lini tutafikiria hata kurusha satellite yetu angani kama hadi leo tunatumia akili na nguvu nyingi kujenga shule, madarasa, matundu ya vyoo, zahanati....
 
Unauliza kama mpumbavu,ziishw uzazi umepungua? Huku ni Ulaya ambako kuna growth rate ni ndogo au hamna kabisa?

Watu kama nyie mlipomaliza kujibu mitihani mkaoshia hapo hapo,uwe unafuatilia hata nchi zingine,juzi tuu hapo unaona akina Biden wanahaha kupotosha mabilioni ya fedha kwenye sekta ya Afya sasa sijui kama huko kulikoendelea hizo kampeni ziliisha?

Maendelea yataisha siku watu wakitoweka Duniani
Miaka 60 ya uhuru story ziwe zile zile za kujenga shule, madarasa, matundu ya vyoo, zahanati kwa emergency, kwa hiyo akili zako na hao punguani wenzako ndo zimeishia hapo kwamba maisha ni kujenga madarasa na matundu ya choo, hopeless!
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
VAT,madini, uvuvi , madini,na kodi mbali mbali fedha zake zinakwenda wapi?

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Miaka 60 ya uhuru story ni zile zile? shule, madarasa, vituo vya afya na mara zote zimekuwa ni kampeni za kujenga utafikiri hii nchi imeanza kuwepo leo....kwa hiyo ni lini tutafikiria hata kurusha satellite yetu angani kama hadi leo tunatumia akili na nguvu nyingi kujenga shule, madarasa, matundu ya vyoo, zahanati....
Wamekuja viongozi / utawala mwingine kwa approach tofauti lakini tunabeza juhudi zao, hatuwezi kutoka hapa tulipo bila kukubali tulikosea huko nyuma. Support yetu ni muhimu naimani kufunga mkanda kwa mwaka mmoja tutaona manufaa ya hizi tozo. Sidhani hata kama CDM / NCCR / ACT watakamata dola tutapata mseleleko kwenye hizi kodi na tozo. Serikali yoyote makini hukusanya na huitaji fedha ili kuwaletea wananchi wake maendeleo ya kweli.
 
Bajeti iliyopitishwa 80% ni kwa matumizi ya kawaida na 20% ndio kwa ajili ya Maendeleo, Sasa ikiwa bajeti kubwa inaenda kulipa mishahara na posho alafu ndogo kabisa ndio inaenda kwenye Maendeleo huoni ni kukwama huko?
Mnasema watu walipe tozo na Kodi, mbona hamsemi pia serikali ipunguze matumizi yasiyo ya lazima?
 
Mimi ningeomba uanishe matumizi yasiyo ya lazima,
 
Hivi bila hizo tozo wasingejenga hayo madarasa na vituo vya afya? Hawa watawala hawana mbinu nyingine ya kupata hela zaidi ya kuwakamua watu with multiple taxations left, right & center?
 
Miaka 60 ya uhuru story ziwe zile zile za kujenga shule, madarasa, matundu ya vyoo, zahanati kwa emergency, kwa hiyo akili zako na hao punguani wenzako ndo zimeishia hapo kwamba maisha ni kujenga madarasa na matundu ya choo, hopeless!
Huna akili ndio maana unaishia kulaumu huna suluhu? Wewe ulivyo mbumbumbu unachokiona serikali inafanya ni madarasa tuu? Huo ni mfano ndio maana una poor reasoning
 
Nasema hivi Samia hadi 2025 atavunja rekodi na kuifunika ya mwendazake kabisaa.

Saizi mataga walichobaki nacho ni kusema eti Magu aliweza bila tozo,ukiwaambia aliweza nini miaka 6 unakuta hakuna kilichokamilika miaka yote hiyo zaidi ya kuvuruga uchumi,kuua,kusumbuana na wapinzani,kuteua na kufukuza,kufika,kutukana na kukunja ndita,wizi na kupiga watu propaganda za tunajenga kwa pesa zetu wakati kumbe ni full mikopo.

Mama hawezi kwenda hiyo njia kwa sababu kwanza tayari amerekebisha uchumi japo kwa kiasi ndio maana mapato ya bandari yameongezeka,Mazao ya wakulima yameongezeka,Kazi kila kona nk sasa kama vipato vya watu vimeongezeka kwa nini asiweke tozo kiasi za kuchangia maendeleo?

Ukienda njia ya mikopo utaishia kuwa kama Zambia,Kenya,Ghana nk kumbuka mikopo ya Sasa sio ya ki LDC bali uchumi wa kati masharti magumu ya kibiashara.
kiongozi nakubaliana na wewe kabisa na namuomba Mungu amnyoshee katika mipango na maono yake......jana katika kata ninayoishi kulikuwa na kikao kizito cha kuamua wapi ijengwe (yaani fedha tayari imeshatinga). wenyeviti na wajumbe wamerumbana vya kutosha mwishowe jibu limepatikana. huku chini tayari watu wameanza kuona kitu, hilo nakuhakikishia kabisa. hivi vikebehi na vimatusi vya kishamba vipo humuhumu mitandaoni na vinasikika sana sababu kuna hofu fulani hivi yenye mchanganyiko wa wivu na chuki.

kiongozi, mambo yanakwenda, hakika nakuambia na yanaelekea kwenda zaidi kwa kasi. niko sehemu fulani inayozalisha korosho.....huo mwamko si wa kitoto, hususani baada ya kuambiwa kuwa kuna kampuni la kimarekani nalo limeshajitosa kuzihitaji. pia nimeona shinyanga wanunuzi na wakulima wa dengu nao wakifurahi. nchi inachangamka taratiiibu na tutaelewana tu....hifadhi koment hii.

jana mama ametumia ujanja wa hali ya juu sana kisaikolojia (hili ni kwa waelewa lakini); ametinga kwa gwajima. bila malumbano, amemnyenyekea vizuri tu kiasi hata cha kuwauliza waumini/wafuasi wake 'mtachanja hamchanji?'! kwa kujitutumua kwa kutumia ujanja wa zamani, baadhi wakajibu 'hatuchanjiii', kama ambavyo clip moja inayosambazwa kwa nguvu na kasi kubwa inavyosuggest. hapo ndipo mama alipopataka.......bila hiyana na taratiiibu akatoa maelezo kidogo kuhusu uchanjaji na uhuru wa uamuzi katika hilo.

mataga wamefurahi kweli na, kwa uono hafifu wa kimihemko, wanakesha wakiporomosha mathreads meengi ya kumsifu gwajima na 'ujanja' wa baadhi ya wanakawe wa kujibu kuwa hawatochanja. walichosahau sasa ni kuwa mama ametumia mwanya huo kuyatimiza malengo yake kiulaiiini kabisa....AMEWEKA WAZI KUWA TOZO LAZIMA TULIPE KWA AJILI YA MAENDELEO YETU NA KILA MTU SASA AMEELEWA. KATIKATI YA FURAHA YAO YA KUSADIKIKA YA GWAJIMA, AMEUWEKA MSIMAMO WA TOZO KIROHO SAFI NA SOTE TUMESHAELEWA SASA. Kama kuna mtu anafikiria ni gwajima aliyeshinda pale basi atakuwa ana matatizo ya kijinsia!!!!!

namtabiria makubwa huyu mama!

kama ingekuwa ni mpiga kelele nyingi, ndani ya miezi minane yake tungekuwa tunaelezwa mengi sana.
 
Baba Askofu Benson Lwakalinda Bagonza anauliza

NAOMBA MSAADA

Nahitaji msaada wenu wasomaji wangu:

1. Hivi mwizi akikuibia hela yako halafu akaitumia kukununulia nguo au chakula, kosa la wizi linakuwa limeisha?

2. Mwizi akikuibia shilingi 100 ukapiga kelele akakurudishia 30 na kubaki na 70, unapaswa kumshukuru kuwa ni mwema?

3. Na kiongozi wako akikukuta unafanya biashara ili upate fedha ya kulipia karo na matibabu, akafunga biashara yako na hela akakunyanganya na kukujengea zahanati na shule, anakuwa amekutendea haki?

TOZO TOZO
LUKU LUKU

VYOTE NI KANDAMIZI. HATULIPI KWA HIARI BALI MNACHUKUA KWA NGUVU. MIILI YETU MNAYO, MIOYO TUMEBAKI NAYO.
 
Baba Askofu Benson Lwakalinda Bagonza anauliza

NAOMBA MSAADA

Nahitaji msaada wenu wasomaji wangu:

1. Hivi mwizi akikuibia hela yako halafu akaitumia kukununulia nguo au chakula, kosa la wizi linakuwa limeisha?

2. Mwizi akikuibia shilingi 100 ukapiga kelele akakurudishia 30 na kubaki na 70, unapaswa kumshukuru kuwa ni mwema?

3. Na kiongozi wako akikukuta unafanya biashara ili upate fedha ya kulipia karo na matibabu, akafunga biashara yako na hela akakunyanganya na kukujengea zahanati na shule, anakuwa amekutendea haki?

TOZO TOZO
LUKU LUKU

VYOTE NI KANDAMIZI. HATULIPI KWA HIARI BALI MNACHUKUA KWA NGUVU. MIILI YETU MNAYO, MIOYO TUMEBAKI NAYO.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi eneo la Tegeta Mkoani Dar es Salaam amesema Tozo zitaendelea kuwepo na hataki kuficha hilo

Amesema, "Tuliweka tozo kwenye mambo ya fedha za mitandao, yamepigiwa kelele sana, nimesikia. Nimekaa na Wataalamu tumepunguza 30%. Miezi miwili tuliyoanza nayo tumekusanya kama Bilioni 60 na zimepelekwa kujenga Vituo 220 vya Afya"

Ameongeza, "Januari tuna wimbi kubwa la Watoto wanataka kuingia Sekondari, lakini wapya wanaoingia Darasa la Kwanza. Hakuna wa kutujengea ni sisi wenyewe. Fedha zitakazokusanywa Septemba na Oktoba zitaenda kujenga madarasa zaidi ya 500"
Marehemu aliamuru kuanzishwa kwa wakati mmoja shughuli/miradi mingi inayohitaji fedha nyingi.
Marehemu aliharibu mahusiano ya kiuchumi na Nchi za nje. Wawekezaji wakaogopa kuja kuwekeza nchini.
Marehemu hakutengeneza na kuimarisha Mifumo ambayo ingetumika kufanikisha shughuli zilizopangwa, na kadhalika.
Kwa jumla, marehemu alivuruga Mifumo yote ya kiuchumi. Nchi ilikuwa inakwenda kuanguka kiuchumi.
Rais SSH amekuta hali hiyo mbaya. Tumsaidie. Tumuunge mkono. Nchi ni yetu sote. Na kwa sasa, tunapaswa kuungana na viongozi wetu kuinusuru Nchi. Lakini katika hili tunapaswa kwenda pamoja bila kubaguana. Isionekane wapo watu hawaguswi na hali hizi.
Kwa mfano, posho na marupurupu ya wabunge yanatakiwa yapunguzwe, iwapo tumedhamiria.
Serikali ipunguze matumizi ktk mambo mengi kadhaa; Kwa mfano, isitishe pia mipango kama huu wa ununuzi wa ndege, ununuzi wa magari ya gharama kubwa kwa viongozi waandamizi wa Serikali ktk ngazi zote, na kadhalika. Wananchi wote wahusike ktk kuijenga Nchi bila kujali cheo cha mtu. Wananchi wa kawaida waheshimiwe. Kuna tabia isiyofaa ya Serikali kutowajali kama ipasavyo wananchi wa kawaida. Inawadharau. Hata wawakikishi wa wananchi (madiwani na wabunge) hawawajali na kuwaheshimu wananchi, wanaiheshimu na kuiogopa Serikali isivyo haki. Lakini hatushangai kwa sababu wengi hawakuchaguliwa bali, aidha, walinunua wapiga kura, au, Serikali iliwasaidia kuiba kura; sasa, wawape heshima na kuwatetea wananchi kwa kigezo kipi?!
Amani na ustawi wa Taifa iwe kipaumbele. Tujifunze kutoka Guinea. Tujifunze Zambia. Mambo yanabadilika. Watu wanabadilika.
Marehemu Samora aliwahi sema, ... Unaweza kuwadanganya watu sana, lakini, huwezi kuwadanganya siku zote. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom