Rais Samia: Tuko vizuri kisiasa lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari, Tunaendelea kupokea matakwa yake

Rais Samia: Tuko vizuri kisiasa lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari, Tunaendelea kupokea matakwa yake

Kuna sehemu mmezuiwa kuendelea na hao mashost zenu 18?
Sisi tuna watu
Ndio kinakwenda kutokea Chadema sio nchi ni moja wapo ya vyama vya siasa tu vilivyosajiliwa hapa nchini.
 
Leo majira ya mchana maamuzi ya maombi ya marejeo ( Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu Antipas Lissu, katika mahakama ya rufaa yamesoma na Lissu ameshinda.

Sasa ni mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia kwenye kesi ya uhaini, au waifute na kumwachia huru Tundu Antipas Lissu.

Kumbuka hata tukirudi na kuendelea na kesi hii ya uhaini mahakam kuu lakini ushahidi wake muhimu ulishakataliwa na mahakama.


Kwa sababu tuna elimu mbalimbali na uwezo wetu wa kufikiri unapungua jinsi pressure zinavyoongezeka, basi tena kama unavyoona.....

Natamani ije siku tutengeneze pool ya viongozi watarajiwa kama China. Isiwe mpango wa mtu na mtuwe kupeana uhalali mgumu
 
Yohana 8:44-46 ...
44:Ninyi ni watoto wa baba yenu shetani; kwa hiyo mnapenda kufanya maovu kama yeye. Tangu mwanzo yeye alikuwa muuaji na hana uhusiano wo wote na mambo ya kweli; kwa maana hana asili ya kusema lililo kweli. Shetani anapodanga nya anadhihirisha asili yake kwa kuwa yeye ni mwongo na ni baba wa uongo. 45;Lakini mimi nawaambia yaliyo kweli ndio sababu ham uamini maneno yangu! 46;Ni nani kati yenu anayeweza kuonyesha kuwa mimi nina dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona basi hamnisadiki?
 
Lisu rudi kundini tujenge nchi pamoja kuendelea kusota gerezani ni kutusononesha vijana tunaotegemea maono yako kwaajili ya kizazi hiki na cha baadae
Ww ni maku kweli, sasa makosa ya lissu ni yapi??
Badala umlalamikie huyo kilaza anayemuogopa lissu majukwaani hadi kumpa kesi ya mchongo we unamuona lissu ndiye mkosaji??
Yaani awaombe msamaha watu walimkosea?! Waliomuweka ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa?!
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMAG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU
 
well done Dr. Samia Suluhu Hassan,
unafanya kazi nzuri sana ya kuwatumikia wananchi na waTanzania wote.

Tupo nyuma yako na tutallinda taifa letu kwa wivu mkubwa, kwa nguvu na gharama yoyote ile.

huyo moja hata asikusumbue, ni kibaraka huyo ametumwa tunamjua vizuri sana 🐒
Kuna muda huwa natamani wewe na Lucas Mwashambwa niwaweke kwenye ignored list lakini naona maisha bila kuwa na watu kama nyie yanakosa radha flani hivi. Huwa nasoma mabandiko yenu huku nacheka. Mpaka unajiuliza huyu kiumbe katoka wapi 🤔.
Lakini anyway mimi ujinga wenu sometimes unanitolea stress, big up kwenu watu tunawadharau nyie mnapiga buku7.
 
Huyu mama bhana 😂
Anapokea matakwa yake huku mhusika akiwa ndani au sio
Anapokeaje matakwa ya mtu mwenye kesi ya uhaini! Kwa hiyo na mimi nikiwa na kesi kama hiyo atakuja kupokea matakwa yangu. Hapo moja kwa moja unaona ni kesi ya mchongo. Wanatafuta pa kutokea, mara DPP Mahakama imekataa kuongeza ushahidi, mara huyu katolewa kwenye kesi ya Ugaidi kapewa uhujumi uchumi. Kifupi wanatafuta pa kutokea na washauri ndiyo watu kama Bashite na Lucas Mwashambwa lazima wapoteane.
 
Rais Samia katika kikao na vyama vya siasa leo Julai 30, 2026 amesema hali ya kisiasa nchini inaendelea kuwa nzuri, akibainisha kuwa licha ya hali hiyo, bado kuna upande mmoja ambao unaendelea kutafakari msimamo wake kuhusu masuala ya kisiasa

Kwa upande mwingine kisiasa kama mnavyoona tuko vizuri."

Tuko vizuri lakini mwenzetu mmoja bado anaendelea kutafakari."

Tunaendelea kupokea misukumo yake, condition zake, matakwa yake. Tunaendelea na ndio mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi."


Soma Pia: Rais Samia: Wananchi hawaitaji vurugu. Kwenye Siasa za chuki na mivutano maendeleo hutoweka

Hata sielewi mtu wa aina hii walimwokotaokotaje katika ngazi zote hadi kufikia huku?
 
Kweli huyu tobo kisu ni haambiliki ;

Wenzake wote wapo hapo kwa maslahi ya nchi Chama chake tu ndio kikwazo.

Wao ndio wenye umuhimu kuliko wengine, wasikilizwe wao tu kwenye kila jambo.

Wasitucheleweshe kwenye mambo mazuri ni kuwaacha wabakie hivyo walivyo na ukaidi wao.
hakuna kitakachopunguza uduni wa maisha yako.
Kila unapoandika chochote humu, uduni wako unajitokeza mbele zaidi kama kielelezo halisi cha maisha yako yalivyo.
 
Back
Top Bottom