Rais Samia: Tuko vizuri kisiasa lakini mwenzetu mmoja anaendelea kutafakari, Tunaendelea kupokea matakwa yake

Nadhani wasipotumia 'tactical problem' yao ya kumtumia Dpp kujifanya hana nia ya kuendelea na kesi, Lissu anaenda kuwavua nguo.

Mashahidi wote wa mchongo ashawagaragaza na mbinu yao hii ya kuchomekea nayo imetupiliwa mbali kulaleki!

Nini kimebakia mahakama kuu sasa, kwenda kuandika hukumu?
 
Lisu rudi kundini tujenge nchi pamoja kuendelea kusota gerezani ni kutusononesha vijana tunaotegemea maono yako kwaajili ya kizazi hiki na cha baadae
Kwanini ushauri huu hukuutoa tangu mwanzo?

Kubwabwaja baada ya kuona kila dalili za jamaa kashinda, ni unafiki.

Na je kusota kwake gerezani ni kwa matakwa yake?
 
Mkuu, wewe ni mvumilivu sana na ni mfano wa kuigwa.

Mimi siwezi kuvumilia hoja kutoka kwa watu wasiotafakari na kuweza kujenga hoja zenye mantiki.

Watu wanaofanana na mazombie ama robots, mie siwezi nshawafuta wote.
 
Ni naona hivi. Hao walioko hapo ndo wapo kwa maslahi yao, hao wasiokuwepo ndo wapo kwa maslahi ya nchi huko walipo.
Waliopo gerezani hawakujipeleka.
 
"Tunaendelea kupokea misukumo yake, condition zake, matakwa yake. Tunaendelea na ndio mambo yanavyoendeshwa kwenye nchi." Mmmh! CcM mmekusanya vyama "RAFIKI" kama mnavyojitambulisha wenyewe mkitegemea mtamdhibiti huyo mwenzenu mnayemsubiri huku mmemkaba koo! Akija mtakubaliana nyie na hoja zenu ambazo tayari mmeziandaa na kukubaliana kisha mtavunja kikao na kuzipitisha hoja zenu huku mkimtengenezea lawama kuwa amevuruga kikao.
 
Wakivunja sheria hakuna atakayewaacha kisa wao ni Chadema.
Uko wapi ugaidi wa Mbowe?, ......na wa Lwakatare je,.......
Tanzania haipo hivi kwa bahati mbaya, bali kwa matokeo ya yanayofanyika na yasiyofanyika ikiwa yalitakiwa kufanyika.
 
Du! Au mimi ndio sielewi au nimepoteza kumbukumbu hata sijui. Hivi Tanzania bado tuna MARAIS wastaafu au tuna RAIS mstaafu?!

Nimemsikia mkuu wa nchi akisema MARAIS wastaafu wakati kumbukumbu zangu zinaniambia tuna RAIS mstaafu. Maana wengine wameshatangulia mbele za haki.

Kwa mantiki hiyo huyo mstaafu ndio kashauri jinsi ya maridhiano huko Zanzibar na sasa inakuja zamu yetu watanganyika!?
 
Huyo ni makamu wake kampuga kijembe wala sio lissu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…