Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

Rais Samia: Tulifika uchumi wa kati tukarudishwa, tupambane turudi tulikokuwa

Kwani marekani hakuna maskini japo ni taifa taifa tajiri duniani, unataka pesa ziwe zinakuja mfukoni mwako bila kufanya kazi acha upumbavu wa kifikra.

Waliotuweka uchumi wa kati mwaka 2019 ndio waliotuondoa Feb 2022.
Hujajibu swali langu.
ulifaidika nini kwa kuwa uchumi wa kati?
 
Uchumi wa kati unaoneka kama nadharia tu kwani haiakisi halisi ya WaTZ. Ukweli uchumi wa kati sio nadharia as such bali inaakisi vigezo ambavyo kimataifa hutumika kuonyesha uchumi umefikia hapo. Kwenye chumi ambazo hazisimami kwenye ( concrete foundation) mfano sera madhubuti sisizoweza kuchezewa na viongozi ndio nchi zinazoweza kuwa na maendeleo endelevu na yenye tija. TZ katiba yake imejengwa kumzunguka mtu sio wananchi ni vigumu sana kuwa na maendeleo ya kudumu. Kila Rais anaekuja anabomoa yaliyopita anaanza upya. Utawala huu unaelekea kuipeleka nchi kwenye matumaini ila bila kua na sera madhubuti juu ya maendeleo yetu na kulindwa na katiba hatufiki popote.Atakuja Rais mwingine wa CCM na kuuwa kila kitu. Tatizo letu sio hatujui tunachotaka bali ni nani ataongoza, hili ndio mchawi wetu. Kuwa CCM ndio chama pekee kinachoweza kuipeleka nchi mbele wengine wote tupa kule. Kwa gharama zozote hata kuharibu uchumi lazima CCM itawale hili ndio jinamizi letu. Mipango yetu yote tupa kule tuwekeze kule wananchi watakapo tupa kura wala sio kwenye sector zitakazo tukwamua kiuchumi.
 
Hebu tuone sector ya kilimo wakati wa kikwete tulisikia sera za kilimo kwanza, wakati wa Magufuli kimya kilimo zero na kupelekea kuuwa kilimo cha korosho na mazao mengine. Jana nilimsikiliza Waziri wa kilimo akiongea kuhusu ku-finance kilimo kwa makofi mengi. Je sera ya kilimo kwa sasa inasemaje? Je financing ndio tatizo kuu la kilimo cha tanzania? Anyway, mimi sio mtaalamu wa kilimo ila napendekeza let us go to the bottom of the issues in agriculture na sio sera za majukwaani na matamko. Nchi haipaswi kuendeshwa kwa mihemko ya kisiasa.
 
Kumbe yeye ndio alitangaza?Nilijua ni WB? So rais wa nchi akitangaza tu kuwa nchi ipo uchumi wa kati na WB nao kwenye taarifa zao wana update?
Kaka kuna watu wasiopenda kabisa kushugulisha akili zao,ni shida mno kuelewesha watu kama hao.
 
Mnashangilia vitu ambavyo havipo kama Nchi yaani Nchi haina uwezo wa kuwa na mafuta ya wiki moja tuu mnazungumzia uchumi wa kati Nchi gani iliyo uchumi wa kati ikawa ina vyanzo vya maji kama Tanzania harafu wananchi wake wengi wanakosa maji safi na salama..mimi nadhani mngejikita kwenye ubora wa maisha ya Watanzania kuliko hizo sifa zisizostahili hata mkiwekwa Dunia ya kwanza wakati ni masikini itawasaidia nini?
 
Miradi mikubwa ndio inayotoa ajira, miradi mikubwa ndio inayoweza kutoa uhakika wa upatikanaji wa huduma muhimu kama nishati nk ambazo ndio economic indicators ambazo hutumika na mashirika hayo ku rank Mataifa kwenye maendeleo, we zuzu😎.
huo upuuzi mwingine ulioandika hapo sijui kuhusu fedha za madawa ya kulevya sijui viungo vya albino,sijui hata ulitaka kusema nini maana inaonekana hata kuandika vitu kama mtu anayejitambua huwezi,poor you😎
Poor me???!! Asante sana!
Ila ninachojua PATO la taifa hupimwa na mojawapo ya formula hii;
GDP= C+I+GE+NE
Ili pato la taifa (GDP) liongezeke lazima hizi variables (C, I, GE & NE) ziongezeke au mojawapo iongezeke
Miradi yote ya kimkakati imeleta impact kubwa sana kwenye pato la taifa,
Awamu ya mauaji ya albino BIASHARA HARAMU ilishamiri sana! Hata ikapelekea waziri mkuu Pinda kulia bungeni, madawa ya kulevya yalishamiri sana , biashara hii haingii kwenye pato la taifa.
Miradi yote hii iliajiri vijana wengi sana hasa mafundi!, tembelea bandarini wakopanua bandari, madaraja yanayojengwa!
Umeme haukukatikatika kama sasa, hivyo uzalishaji ulikuwa wa uhakika!
Sasa hapo uzuzu wangu uko wapi?
 
Mnashangilia vitu ambavyo havipo kama Nchi yaani Nchi haina uwezo wa kuwa na mafuta ya wiki moja tuu mnazungumzia uchumi wa kati Nchi gani iliyo uchumi wa kati ikawa ina vyanzo vya maji kama Tanzania harafu wananchi wake wengi wanakosa maji safi na salama..mimi nadhani mngejikita kwenye ubora wa maisha ya Watanzania kuliko hizo sifa zisizostahili hata mkiwekwa Dunia ya kwanza wakati ni masikini itawasaidia nini?
Economic development NA economic growth ni vitu viwili tofauti
 
🙌 Yule mshamba kumbe alijipatia wafuasi wengi hivi!!!
hii si opinion ya mtu. Kama hujui ni nani anayetangaza kuwa nchi fulani iko kwenye uchumi level gani basi ukae kimya. Halafu it may not be fair kuwa kwenye kundi tukufu la great thinkers kama hujui elementary things.
 
sababu za kuporomoka zinafahamika, wala sio Tanzania tu bali ni dunia nzima.

Mardhi ya Uviko19 ni sababu kuu, sasa vita n.k.
Hivyo tupambane tutafika zaidi ya pale tulipo kuwa.
 
Dah, nimesikiliza hapo kwenye uchumi. Mama anasema tulifika uchumi wa kati sababu ya Mungu na si mtu. Hivi kweli kuna mtu asiyejua kuwa kila jambo hutokea kwa mapenzi ya Mungu ila na wewe lazima ufanye bidii. au ndio marehemu wanazidi kumchapa. Safaro ni ndefu sana kwa hali hii
 
Nakumbuka kipindi kile tunajisifu tumeenda uchumi wa Kati, ITV walimuhoji mchumi Prof Lipumba akasema tumepanda uchumi wa Kati lakini ni Kwa kiwango kile Cha chini kabisa kwamba tukiyumba kidogo tunarudi tulipokuwa. Na kweli yametokea.
 
Tanzania bado ipo uchumi wa kati.
 
Back
Top Bottom