Rais Samia: Tulikaa kikao na Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kujadili mkopo. Iko wapi nafasi ya Baraza la Mawaziri?

Rais Samia: Tulikaa kikao na Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kujadili mkopo. Iko wapi nafasi ya Baraza la Mawaziri?

Mama anaonekana kutokuwa na confidence. Ogopa sana watu wasiokuwa na confidence wakiwa na madaraka. Kuna tozo, makusnyanyo ya kodi yameongezeka, mikopo kwa wingi, serikali inatumia pesa hizo namna gani. Kulikuwa na mmoja alidai anataka kukodi crane kwa gharama karibu sawa na kujenga daraja la wami.
Aliyemtangulia alikuwa na confidence iliyopitiliza, Matokeo yake akawa anaogopwa mpaka watu wanashindwa kufanya kazi kwa amani.
 
Hii nchi usalama wa taifa inahitaji kujipanga wamtafute mtu mwenye uwezo katika maswala ya uchumi kwa viwango vya Kimei ashike usukani wampangie baraza la mawaziri wenye taaluma watu wafanye.

CCM aina watu wenye sifa ya kutuongoza yaani raisi anasema wazi kwa lugha nyingine waziri wake alimwambia makusanyo ya sasa kulipa madeni ni shida kukopa zaidi ni kujiongezea mzigo.

Kuacha mkopo wa interest free wa tsh 1.3 trillion kwa nchi maskini ni ufala, lakini una mipango gani ya kuongeza makusanyo hapo ndio shida ilipo. Huku bandarini kumevuja, TRA umewaambia walegeze.

Kukopa kulipa ni short term solution kumudu hiyo situation unahitaji kuongeza makusanyo that’s the only out of jail card.

Busara mama asigombee 2025 hana uwezo wa kuendesha nchi na raisi sana kuongopewa she is clueless on just about everything hana abc ya jambo lolote.
Makusanyo yanaongezwa kwa tozo za simu, ambazo pia zinalalamikiwa. Tatizo wabongo wanataka kwenda mbinguni lakini kifo wanakiogopa.

Mama anafaa sana kuwa kiongozi, hana ukatili, anayo fairness. Anajua kuongea na wasio watanzania, hana majivuno yasiyo na kichwa wala miguu na anayo convincing power ya kufikia muafaka baada ya mazungumzo mazito kwa faida ya Tanzania.
 
Kwa vile marehemu alikuwa anakosea ni sawa mama nae kufuata nyayo hizo hizo?

Kwa hiyo hata kumfunga Mbowe ni sahihi pia?

Hivyo vichwa mmejaza makamasi tu?
Ni sahihi sababu alifikia stage akaanza kukosa adabu wazi wazi
 
Nikiendelea na uchambuzi wa hotuba ya juzi ya Rais Samia, kuna sehemu alisema walikaa kikao cha watu watatu, yaani yeye Rais, Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kuhusu kufanya maamuzi juu ya masuala mkopo na hali ya nchi kwenye ukopeshwaji!

Kauli hiyo imenitia mashaka? Nimejiuliza iko wapi nafasi ya baraza la mawaziri kwenye kufanya maamuzi magumu kama hayo kwa maslahibya nchi?

EB979EFE-B677-4DE4-B023-C1F843043433.jpeg
 
Makusanyo yanaongezwa kwa tozo za simu, ambazo pia zinalalamikiwa. Tatizo wabongo wanataka kwenda mbinguni lakini kifo wanakiogopa.

Mama anafaa sana kuwa kiongozi, hana ukatili, anayo fairness. Anajua kuongea na wasio watanzania, hana majivuno yasiyo na kichwa wala miguu na anayo convincing power ya kufikia muafaka baada ya mazungumzo mazito kwa faida ya Tanzania.
Fairness ya kuongeza majobless na kurudisha ada, tozo na inflation?
 
Ndio majukumu ya waziri wa fedha. Ni kila sekta kabla hayajafanyika maamuzi makubwa waziri husika hukaa pamoja na rais na katibu mkuu kiongozi.
Hoja ni je bunge hushirikishwa? Najua kwenye hatua za mwanzo wanaweza kuwa hata watu wawili au watatu. Ila wakisha-draft kila kitu bunge hushirikishwa? Na kama linashirikishwa mbona Ndugai analalama sasa hivi?
 
Mbona ushaanza mahepehepe kama ndugai..! Ile ni issue tu ya Rais ameibua kwa maslahi ya Tanzania na vile bado haijatiki vizuri amesema tu kuna good commitment ya hao jamaa waliopelekewa hizo barua, sasa mambo yakiwa sawa italetwa huko baraza la mawaziri kama kutakuwa na haja hiyo? saivi ukiita baraza la mawaziri waende kujadili nini kwenye jambo hilo?? piriad

kuna mambo unatakiwa kutumia kichwa chako japo kwa dakika 1, Samia ni rais mwanamke lakini yule mama ana uzoefu wa nchi sana ni mzuri sana ni mbunifu ana mawazo chanya sana ingawa wabongo wengi hawakumfahamu yule mama walifikiri atajipakatisha tu kwenye makochi ya Ikulu
🚮
 
Hoja ni je bunge hushirikishwa? Najua kwenye hatua za mwanzo wanaweza kuwa hata watu wawili au watatu. Ila wakisha-draft kila kitu bunge hushirikishwa? Na kama linashirikishwa mbona Ndugai analalama sasa hivi?
Ndugai hakutegemea huu muitikio wa Rais Samia na wanachama wa CCM. Alidhani kila kitu kitakuwa kama mazoea yalivyo.
 
Makusanyo yanaongezwa kwa tozo za simu, ambazo pia zinalalamikiwa. Tatizo wabongo wanataka kwenda mbinguni lakini kifo wanakiogopa.

Mama anafaa sana kuwa kiongozi, hana ukatili, anayo fairness. Anajua kuongea na wasio watanzania, hana majivuno yasiyo na kichwa wala miguu na anayo convincing power ya kufikia muafaka baada ya mazungumzo mazito kwa faida ya Tanzania.
Hivi unajua implication ya kauli yake mbele ya lenders yakuwa wametumia mkopo kulipa deni na waziri alimshauri kwa sasa uwezo wa makusanyo kulipa madeni shida.

Trust me if you know anything about public finances and national debt management ile ni kauli ya ovyo mno kutamkwa na kiongozi wa nchi; ni kama kujiwashia green light kwa IMF/WB hali yetu tete huku.

Hajui ata madhara ya kauli zake, kwa nchi.
 
Kikao cha mawaziri huwa kinaitishwa baada ya kwanza waziri wa sekta husika kukaa na rais na katibu mkuu kiongozi na kujadili kipi kitaongelewa. Ni preliminary meeting,

Suala likiwa ni la wizara ya michezo atakaa na waziri wa michezo na katibu mkuu kiongozi wakishaafikiana ndio kinaitishwa kikao cha mawaziri wote.
Rais kasema alikaa na nani?wewe unaeleza taratibu, bibi yeye anaeleza kilichofanyika. Kwa akili ya kawaida kuonyesha alipata idhini asingetaja hako kakikao bali angetaja kikao cha baraza
 
Back
Top Bottom