Rais Samia: Tulikaa kikao na Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kujadili mkopo. Iko wapi nafasi ya Baraza la Mawaziri?

Rais Samia: Tulikaa kikao na Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kujadili mkopo. Iko wapi nafasi ya Baraza la Mawaziri?

Nikiendelea na uchambuzi wa hotuba ya juzi ya Rais Samia, kuna sehemu alisema walikaa kikao cha watu watatu, yaani yeye Rais, Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kuhusu kufanya maamuzi juu ya masuala mkopo na hali ya nchi kwenye ukopeshwaji!

Kauli hiyo imenitia mashaka? Nimejiuliza iko wapi nafasi ya baraza la mawaziri kwenye kufanya maamuzi magumu kama hayo kwa maslahibya nchi?
Utuambie kwanza mpaka anakopa 29t Marehemu JPM alikuwa anakaa na nani?
 
Hoja ni kwamba deni limetuelemea na Hilo linajulikana wazi!Hiyo ndio hoja kuu!
Tunakopa kulipa mkopo maana Kwa mapato yetu hatuwezi!
Deni litaendelea kupaa,subiri mpaka mwezi wa 6 utaona deni limefika wapi!
Hapa si mlikuwa mnasema TUNAJENGA KWA KODI ZETU??
 
Kwanini Ndugai hakuanza kuhoji mikopo iliyokuwa inakopwa kwa siri bila bunge kuhusishwa na manunuzi ya ndege nakadhalika pasipo muhuri wa bunge ama kujadiliwa? Kwanini aanze kuhoji wakati huu tena mkopo wa wazi kabisa ambao umma umefahamishwa pamoja na matumizi yake kuwa ya wazi.

Hapo ndipo wenye akili wanapohoji uhalali wa Ndugai kuhoji mkopo wa sasa tena wa 1.3 tr nakuacha mikopo kibao ya awamu ya tano iliyokopwa gizani.

CAG katika ukaguzi wake alibaini kutoonekana kwa matumizi ya zaidi zaidi ya 1.5 trilion lakini Ndugai hakuhoji badala yake CAG aliondolewa kinyume cha sheria.
 
Afanye apendavyo duuh[emoji3]
Ndio apendavyo.

Kama ambavyo wengine walifanya wapendavyo wanafki kama ninyi mkakaa kimya kwa kigezo cha anayefanya ni mzalendo 'kweri' kweri.
 
Sio kila jambo linahitaji kikao cha baraza la mawaziri. Sasa ikiwa kila jambo kihitaji baraza la mawaziri iko wapi nafasi ya Rais kufanya maamuzi sahihi kwa mujibu wa katiba kwa mustakabali wa taifa.

Kwa katiba iliyopo Rais ana maamuzi makubwa mno na hakuna chakumfanya. Katiba mpya ni moja ya suluhisho la matatizo kama haya.
 
Hoja ni je bunge hushirikishwa? Najua kwenye hatua za mwanzo wanaweza kuwa hata watu wawili au watatu. Ila wakisha-draft kila kitu bunge hushirikishwa? Na kama linashirikishwa mbona Ndugai analalama sasa hivi?
 
Hoja ni je bunge hushirikishwa? Najua kwenye hatua za mwanzo wanaweza kuwa hata watu wawili au watatu. Ila wakisha-draft kila kitu bunge hushirikishwa? Na kama linashirikishwa mbona Ndugai analalama sasa hivi?
Bunge linatakiwa lishirikishwe kuidhinisha mikopo? Kwa kifungu kipi cha katiba?
 
Kikao cha mawaziri huwa kinaitishwa baada ya kwanza waziri wa sekta husika kukaa na rais na katibu mkuu kiongozi na kujadili kipi kitaongelewa. Ni preliminary meeting,

Suala likiwa ni la wizara ya michezo atakaa na waziri wa michezo na katibu mkuu kiongozi wakishaafikiana ndio kinaitishwa kikao cha mawaziri wote.
Nafasi ya bunge ni ipi katika kuidhinisha mikopo?
 
Kwahiyo akili yako inaishia hapo? Katiba inapozungumzia wajibu mkuu wa bunge ni kuisimamia serikali na kuishauri unadhani ililenga nini? Kwahiyo mpaka katiba itamke kwamba miongoni moja ya wajibu wa bunge ni kuidhinisha mikopo?

Sifa mojawapo ya katiba ni "bravity" kwa maana huzungumzia mambo kwa ufupi sana bali sheria nyinginezo ndo huweka mambo kwa undani wake.

Pia katiba moja ya sifa yake ni kwamba inaeleza mambo in general. Kwahiyo kitendo cha katiba kueleza tu kwa ujumla kwamba miongoni mwa majukumu makuu na muhimu ya muhimili wa bunge ni kuisimamia serikali. Inaisimamiaje serikali no kama hivi mambo ya kujadili na kupitisha ama kuikataa bajeti ya serikali kwa maslahi mapana ya wananchi.
 
Nikiendelea na uchambuzi wa hotuba ya juzi ya Rais Samia, kuna sehemu alisema walikaa kikao cha watu watatu, yaani yeye Rais, Katibu Mkuu Kiongozi na Waziri wa Fedha kuhusu kufanya maamuzi juu ya masuala mkopo na hali ya nchi kwenye ukopeshwaji!

Kauli hiyo imenitia mashaka? Nimejiuliza iko wapi nafasi ya baraza la mawaziri kwenye kufanya maamuzi magumu kama hayo kwa maslahibya nchi?
Na nafasi ya bunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi kwenye masuala ya kulitia taifa madeni ya riba za ajabu ajabu ni ipi?! Wabunge walipewa fursa ya kukubali au kukataa kukopa kwa ajili ya Zanzibar halafu deni tulipe sisi?!
 
Nafas ya Bunge pia haipo alaf anaenda kumshambulia ndugai , na wengine wanashangilia what a shame
Makamu wa Raisi na yeye hana nafasi yupo kama naibu waziri tu
 
Nafasi ya Ndugai iko wapi hapa? hii akili ndogo inayotuongoza itatupeleka pabaya zaidi, na ndio sababu Ndugai alihoji juu ya hii mikopo.

Matokeo yake badala ya kujibu hoja ya Ndugai kwa kujua amekosea akaona dawa yake amkodishie kikundi cha mipasho toka mikoani wakamsute ikulu.
Anahoji ktk kikao cha wagogo wakati ana nafasi ya kutumia kamati ya fedha na mipango iliyopo chini yake kuweni na AKILI ni yatima
 
Back
Top Bottom