Rais Samia: Tumetoa Sh. bilioni 700 kwaajiili ya ruzuku ya mbolea | Uzalishaji wa mazao ya chakula umefikia Tan 22.8.

Rais Samia: Tumetoa Sh. bilioni 700 kwaajiili ya ruzuku ya mbolea | Uzalishaji wa mazao ya chakula umefikia Tan 22.8.

Jesusie

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
1,543
Reaction score
791
Dar es Salaam, Tanzania – Uzalishaji wa mazao ya chakula nchini umeongezeka kutoka tani milioni 17.1 mwaka 2021 hadi kufikia tani milioni 22.8 mwaka 2024, ongezeko linaloashiria jitihada za Serikali na wakulima kuongeza tija na kuhakikisha usalama wa chakula nchini.

Aidha, Serikali inaendelea na uboresha wa kiwanda cha Minjingu, ili kuongeza uwezo wake wa uzalishaji na kuboresha ubora wa mbolea zinazozalishwa. Pamoja na ruzuku ya Sh. bilioni 708.6 iliyotolewa kwa upatikanaji wa mbolea, jitihada hizi zote zinachangia moja kwa moja katika kuimarisha uzalishaji wa chakula na kukuza ukuaji wa uchumi wa taifa. Hatua hizi zinaonesha wazi kwamba Serikali inachukua hatua madhubuti kuhakikisha kilimo kinaendelea kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa.
 
Back
Top Bottom