Rais Samia tunakuomba hutubia taifa, omba radhi, fanya maamuzi magumu ya kuvunja mkataba huu nchi ipone

Acha porojo!!
 
Ccm imechelewa sana kuondoka madarakani na haya ndio madhara yake.

Chama kimoja hakiwezi kutawala zaidi ya nusu karne hiyo ni dalili ya nchi husika kuwa na watu wajinga kupindukia.
Nadhani iko haja kwa Deep State ya Tanzania iwe na vyama viwili au hata zaidi ambavyo watakuwa wanavipa Mihula ya kukaa madarakani kama ilivyo Amerika baina ya Republican na Democratic,
Miaka 8 au saa nyingine 4 wanapokezana kwa manufaa ya taifa.
 
....... Lakini kati ya hivyo ccm isiwepo, yenyewe inatakiwa ife kabisa, imeiletea hii nchi hasara kubwa sana.
 
Jukwaa zito sana hili..Sikujua..Hili jukwaa Lina watu wa kila aina ,wazee Kwa vijana ,Wasomi Kwa Wasio wasomi..Walio ktk mfumo na vitengo vya nchi..

Waandamizi,Wastaafu,Waliotumbuliwa na walioenguliwa..Ndugu,jamaa na marafiki ,Mashehe ,Maaskofu,Makadinari..Waliovuliwa magamba na waliokatwa mikia..
 
Mama hapendi kusoma
Sio hapendi kusoma, ni mvivu balaa si unawajua tena waswahili kwa kuridhika...ashaitwa mh presdaa ana shida gani tena wakati maisha kashayapatia?!.
 
Nimegundua wengi wanaoposti ujinga dhidi ya DP World ni wafanyakazi wa bandari na wanufaika wengine wa ufisadi uliopo pale bandarini.
 
Nimegundua wengi wanaoposti ujinga dhidi ya DP World ni wafanyakazi wa bandari na wanufaika wengine wa ufisadi uliopo pale bandarini.
Mkuu Mzee Kijana, hii ni vita nzito huyo GSM halipi kodi hapo bandarini anapitisha mizigo na anakwenda kutengeneza super profit kwani halazimiki kushusha au kupandisha bei ya bidhaa ya mwisho. Hujiulizi awamu ya sita kwanini maduka mengi ya vifaa vya michezo yameongezeka!.

Aliye nyuma ya GSM ni familia ya JK, aliyemuweka Mwigulu Nchemba wizara ya fedha na katibu mkuu hazina yaani pay master general ni JK.

Usitegemee urahisi wao wa kupata pesa wanaoufurahia awamu hii eti wakazipokea kwa tabasamu hizi habari za Rais Samia kutaka awe anasoma kinachofanyika kule bandarini akiwa ikulu. Ni ujumbe kwa GSM na biashara zake kwamba wajiandae na mabadiliko yanayokuja.

Kuna vita nzito ya watu wa JK wanaopambana ili DPW asifunge mitambo yake pale bandarini, usishtushwe na hawa wanasheria uchwara wa humu JF, usishtushwe na yule Mwabukusi, wote hao ni wapokea mshahara wa GSM na matawi yake ya ufisadi.
 
Waandike tu maumivu. Hakuna kurudi nyuma. Operesheni ondoa mafisadi bandarini lazima iendelee.
 
Waandike tu maumivu. Hakuna kurudi nyuma. Operesheni ondoa mafisadi bandarini lazima iendelee.
Wanakuja kuzichota akili za wanaosoma mada za humu ndani. Tunaweza kufikia hata pato la trilioni 26 kwa mwaka, tunaweza kabisa kujitegemea kwa pato la ndani tu kama alivyosema Kagame enzi zile za JK.
 
Wanakuja kuzichota akili za wanaosoma mada za humu ndani. Tunaweza kufikia hata pato la trilioni 26 kwa mwaka, tunaweza kabisa kujitegemea kwa pato la ndani tu kama alivyosema Kagame enzi zile za JK.
Umesema kweli Mkuu. Mapato mengi ya bandari yanaishia mifukoni mwa watu. Mbaya zaidi mafisadi wa bandari hawatosheki ni wizi mwanzo mwisho. Naunga mkono Serikali kuwapa DP World bandari tena ikibidi wapewe zote tu. Baada ya bandari tuangalie na TRA nako kunahitaji mabadiliko makubwa sana.
 
Ajiuzulu tu atatuuza. Mwenyewe anatafuta hela tu.
 
Mkuu ni vita nzito ya kiuchumi yale yale aliyokuwa akiyasema marehemu JPM ndio haya yanayotokea hivi sasa.

Na kama JPM alisema mara kwa mara tumuombee, Samia anaipigana hii vita akiwa mpole na mkimya.
 
Litapita tu hili na bandari hairudi tena. Hakuna haja kuomba msamaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…