Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dk Faustine Ndugulile itaelekezwa kwa Mtanzania mwingine mwenye sifa.
Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu, Desemba 2, 2024 katika hafla maalumu ya kuaga mwili wa Dk Ndugulile iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Soma pia: Mkurugenzi mkuu WHO amlilia Faustine Ndugulile
"Wanadamu tunapanga yetu, lakini Mungu anatupangia, Dk Ndugulile ameiweka nchi pazuri lakini Mungu amechukua kilicho chake. Tutaingia tena kwenye mashindano tutatafuta Mtanzania mwenye sifa atakayeweza kushindana na ulimwengu, tutaingia tena na tutaweka mtu mwenye sifa ileile kutuwakilisha," amesema Rais Samia.
Rais Samia amesema amepokea salamu nyingi za pole kutoka ndani na nje ya nchi, huku akiwashukuru viongozi waliofika kumuaga Dk Ndugulile hasa kutoka WHO.