Rais Samia: Tuzo hii ya Babacar Ndiaye alistahili Hayati Dkt. Magufuli

Huyu mama ni mjanja...anajua kusoma alama za nyakati.
 
Mama amekuwa mkwelj. Angelikuwa yule chizi angejitukiza yeye.

Nakumbuka jiwe alikuwa anamsagia kunguni Kikwete ili sifa zote zibaki kwake.
Magufuli alikuwa anasema ukweli bila kupaka mafuta wala kujikuza; niliwahi kusema kuwa Magufuli alitakiwa kufundishwa namna ya kubana baadhi ya maneno, kwani kuwa anasema ukweli wote ndiko kulikomfanya achukiwe na watu wa Kikwete. Makosa ya Kikwete alikuwa anayasema na mazuri pia alikuwa anayesema, kwa mfano aliposema kuwa Kikwete alipenda ile flyover ya Tanzara ijengwe ingawa haikujengwa, yeye ataijenga. Hapo kulikuwa na ukweli na ukweli. Ukweli wa kwanza ni kuwa wazo la flyover ya Tazara ni la kutokea serikali ya Kikwete, ukweli wa pili ni kuwa serikali ya Kikwete hakujenga, ila serikali yake itajenga. Ni vivyo hivyo pia kwenye ujenzi wa Terminal 3 ambayo miaka ya mwisho ya utawala wa Kikwete ujenzi ule ulikuwa hauendelei kwa vile wakandarasi walikuwa wanataka kujitoa kwa kukosa malipo.
 
Mama amekuwa mkwelj. Angelikuwa yule chizi angejitukiza yeye.

Nakumbuka jiwe alikuwa anamsagia kunguni Kikwete ili sifa zote zibaki kwake.
Gazeti la Mawio lilifungiwa mwaka 2017 kisa lilikuwa linamsema vibaya Kikwete na ndipo Magufuli akatoa tamko kuwa "Wastaafu Waachwe wapumzike sio kila siku kuwasema".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fact ni kuwa mkataba wa ujenzi wa Flyover ya TAZARA uilwekwa saini mwaka 2015 na utawala wa JK kabla hata ya uchaguzi mkuu uliomuingiza Magufuli madarakani
 
Kwa mara ya kwanza mama amekiri UKWELI hadharani.

Ila kwa ile team ROHO MBAYA leo itakuwa siku mbaya sana kwao.
 
Kikwete kaharibu sana hii nchi baada ya kuigeuza Ikulu pango la walanguzi
Na bado alikuwa anaingilia kwapani kama nchi ya ufaransa na makoloni yake wananchi walikuja juu sasa naona kaingia chimbo kama vile hayupo mkwere noma.
 
Asante kwa Kukiri kuwa hiyo Tuzo ya 'Abubacar Ndiaye' uliyopokea inayohusiana mno na Maendeleo ya Miundombinu si yako bali ni ya Hayati Rais Dkt. Magufuli na ungejisifia ( ungejipongeza ) ni yako kutokana na Juhudi zako ningekushangaa kuliko Maelezo ila nashukuru ulijishtukia Mwenyewe.

Hata hivyo nalaumu Watu wako wa Itifaki kwani kwakuwa walikuwa wakijua kuwa Baba ( Champion ) wa Miundombinu Tanzania alikuwa ni Hayati Rais Dkt. Magufuli basi ili kuleta maana zaidi na kuipa Heshima na maana ingependeza katika 'Ziara' yako hiyo ungesafiri na Mkewe ( Mjane ) Mama Janet Magufuli au hata Yule Mwanae mkubwa ( Bonge ) wa Kiume kama muwakilishi wa Familia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…