Magufuli alikuwa anasema ukweli bila kupaka mafuta wala kujikuza; niliwahi kusema kuwa Magufuli alitakiwa kufundishwa namna ya kubana baadhi ya maneno, kwani kuwa anasema ukweli wote ndiko kulikomfanya achukiwe na watu wa Kikwete. Makosa ya Kikwete alikuwa anayasema na mazuri pia alikuwa anayesema, kwa mfano aliposema kuwa Kikwete alipenda ile flyover ya Tanzara ijengwe ingawa haikujengwa, yeye ataijenga. Hapo kulikuwa na ukweli na ukweli. Ukweli wa kwanza ni kuwa wazo la flyover ya Tazara ni la kutokea serikali ya Kikwete, ukweli wa pili ni kuwa serikali ya Kikwete hakujenga, ila serikali yake itajenga. Ni vivyo hivyo pia kwenye ujenzi wa Terminal 3 ambayo miaka ya mwisho ya utawala wa Kikwete ujenzi ule ulikuwa hauendelei kwa vile wakandarasi walikuwa wanataka kujitoa kwa kukosa malipo.