Rais Samia: Uchaguzi Mkuu wa 2020 ulifanyika vizuri sana

Rais Samia: Uchaguzi Mkuu wa 2020 ulifanyika vizuri sana

"Tena kwa kiwango kikubwa sana" amesisitiza mcha Mungu huyo!

Binafsi namuunga mkono kwa nguvu zote:

Ila kilikuwa Kiwango kikubwa sana Cha kuiba kura, kupiga na kuwatoa nje mawakala wa Vyama pinzani, pia kupita bila kupingwa!
Mtu mwongo namna hiyo, anayebambikia watu kesi, unamwita mcha Mungu? Unamaanisha mungu wa Baali?

Hakuna Mungu wa kweli pale, zaidi ni unafiki wa kutaka kuonekana ni muumini ilihali matendo ja kauli zimejaa ushetani
 
Yuko sahihi

Mh.Rais SSH yuko sahihi mno

Mh. Trump alikuwa ni Rais na alilalamikia RAFU ZA WAZI ZA WAPINZANI. Hii ina maana ya kwamba hata WAPINZANI huwa wanacheza RAFU na Wakati mwingine huwafanikisha kuingia IKULU.

✓Yale mabegi ya KURA FEKI kule KAWE na kwingineko ilikuwa UJANJA MTUPU uliosukwa na "jamaa" ili KUICHAFUA CCM, NCHI NA SERIKALI YAKE.

#SiempreJMT
#NchiKwanzaKablaYaYeyote
#KaziIendelee
Wahi Milembe hospital. Hapa ni kwaajili ya walio wazima.
 
Mungu asingewaibisha wote waliovuruga uchaguzi mkuu maana tuliomba.
Majibu yakapatikana jiwe,sabaya, chalamila, polepole, bashiru, bashite wote chali.
 
Ujumbe huu mzito ameutoa leo alipokuwa akipokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa 2020 iliyoandaliwa na NEC kwenye viwanja vya Ikulu

=====

Rais Samia amewapongeza Watanzania kwa kushiriki kikamilifu kuanzia zoezi la uandikishaji, kupiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu huo ambao chama chake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mshindi wa urais na kuzoea karibu majimbo na kata zote.

“Hakuna shaka, yeyote aliyeshuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka jana alishuhudia jinsi ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango kikubwa sana,” amesema Rais Samia.

Bi Kidude ni noma
 
Waangalizi kutoka nje walisemaje vile, maana huwa wanajitahidi kuwa fair.
 
Ujumbe huu mzito ameutoa leo alipokuwa akipokea Taarifa ya Uchaguzi mkuu wa 2020 iliyoandaliwa na NEC kwenye viwanja vya Ikulu

=====

Rais Samia amewapongeza Watanzania kwa kushiriki kikamilifu kuanzia zoezi la uandikishaji, kupiga kura na kushiriki uchaguzi mkuu huo ambao chama chake Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa mshindi wa urais na kuzoea karibu majimbo na kata zote.

“Hakuna shaka, yeyote aliyeshuhudia uchaguzi mkuu wa mwaka jana alishuhudia jinsi ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango kikubwa sana,” amesema Rais Samia.

Off course, Maza lazima awasifu kwa kufanya kazi vizuri kwa jinsi walivyoelekezwa. Lakini time is ticking na mwisho lazima utakuja.
 
Ama kweli msema kweli Ni mpenzi wa Mungu, kinyume chake Sasa ni motoni.
 
Back
Top Bottom